Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.
KUKUSANYIKA KATIKA DUA.
Ni jambo la kupendeza kuomba dua mkiwa kwenye kundi. Zipo dua ambazo siku zote zinaombwa watu wakikusanyika kama dua ya kuomba mvua. Kukusanyika kwenye dua ni sunnah katika sunnah zingine. Ijulikane kuwa pindi mtu akiomba dua kisha wengine wakaitikia aamiin huenda katika waloitikia akawepo walii wa Allah ambae ikawa sababu ya dua kujibiwa.
Pia watu waliokuwepo kwenye kundi aombe mmoja na wengine waitikie aamiin na wanyanyue mikono yao. Maswahaba Allah awaridhie walikiwa wakiombeana dua na walikuwa pia wakikusanyika kayika kuomba dua. Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa pia akiwahimiza maswahaba wake kuwa katika kundi wanapoomba dua na wengine waitikie aamiin.
Amesimulia Habiib Ibn Salamah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “halikusanyiki kundi la watu na wakaomba dua wengine na wengine wakaitikia ‘aamiin’ isipokuwa Allah ataijibu dua hiyo”. (amepokea tbrany, Bayhaqy na Alhaakim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
HUU NDIO USIA WA MTUME KWA WAISLAMU
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلًا قَالَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه و سلم أَوْصِنِي.
Soma Zaidi...MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.
Soma Zaidi...Historia ya Imamu Bukhary Muandishi wa Hadithi za Mtume s.sa. w
Hii ni historia ya Imamu Bukhary pamoja na kitabu chake cha sahihul Bukhari.
Soma Zaidi...