IFAHAMU DAWA YA ISONIAZID KATIKA KUPAMBANA NA UGONJWA WA TB


image


Post hii inahusu zaidi dawa ya isoniazid katika mapambano na kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba kifua kikuu ni hatari katika jamii kwa hiyo dawa ya isoniazid ni mkombozi katika mapambano na kifua kikuu.


Dawa ya isoniazid katika kupambana na kutibu kifua kikuu.

1.  Dawa ya isoniazid ni mojawapo ya dawa inayosaidia katika matibabu ya kutibu kifua kikuu kwa sababu utibu kifua kikuu ikiwa imechanganyikana na dawa nyingine kama vile Rifampin, pyrazinamide na ethambutol, pia dawa hii utumika kwenye daraja la kwanza la matibabu ya kutibu kifua kikuu ikiwa na Rifampin, pyrazinamide na ethambutol zikiwa na muundo wa RHZE ambapo H inawakilisha isoniazid na katika daraja la pili inakuwa ni Rifampin na isoniazid ambapo muundo wake ni RH ambapo R ni Rifampin na H ni isoniazid.

 

2. Tunafahamu kabisa kwamba kifua kikuu usababishwa na bakteria ambaye kwa kitaamu huiitwa  mycobacterium tuberculosis, kwa hiyo kazi ya isoniazid ni kuzuia ukuaji wa bakteria Huyu na hatimaye bakteria usinyaa na ugonjwa hauwezi kuendelea kuwepo ikiwa dawa inatumika vizuri pia dawa hii inazuia kuzalishwa kwa Ganda la juu la mdudu huyu ambaye usababisha kifua kikuu na kwa hiyo mdudu kama Hana gamba la juu hawezi kuendelea kuwepo pia dawa hii Ina uwezo wa kuharibu protein ya mdudu Huyu protein hiyo kwa kitaamu huiitwa DNA.

 

3. Kwa kawaida aina hii ya protein ambayo inaitwa DNA ndiyo Ina mafuta ( lipis) wanga (carbohydrates) na virutubisho vyote vya mdudu Huyu anayesababisha kifua kikuu kwa hiyo kazi ya isoniazid ni kuharibu hiyo protein na hiyo protein kwa sababu Ina virutubisho vyote na ikishaharibiwa hakuna maisha ya bakteria huyo na ugonjwa upungua na hatimaye kutoweka kabisa kwa sababu ya kazi ya isoniazid. Kwa hiyo hui ndio uwezo mkubwa uliopo kwenye dawa hii ya isoniazid kwa watumiaji kuweni Ms Imani kwa sababu dawa hii ufanya mambo makubwa katika kupambana na bakteria.

 

4. Kwa kawaida na mara nyingi dawa hii huwa katika mfumo wa vidonge kwenye muunganiko na dawa nyingine na kwa hiyo umezwa na maji na pia kwa wakati mwingine inaweza kutolewa kupitishia kwenye damu na pia kwenye nyama ikiwezekana na kwa uhitaji maalumu kadri ya maoni ya wataalamu wa afya, katika dawa za kutibu kifua kikuu dawa hii ya isoniazid uuua asilimia tisini na tisa ya bakteria ndani ya siku chache kwa hiyo utumika kwenye daraja la kwanza na la pili kwa sababu ya kuua kiwango kikubwa cha bakteria kwa siku chache.

 

5. Pia dawa hii inatumika kwa wagonjwa wenye maambukizi mbalimbali ya virus vya ukimwi, hasa kwa wale ambao ndio wanaanza matibabu ingawa hawana ugonjwa wa Kifua kikuu, utumika dawa hizi Ili kuwakinga na hatari ya kuwa na maambukizi kwa sababu wagonjwa wa maambukizi ya ukimwi Wana kiwango kidogo cha kinga mwilini pia na kifua kikuu Kina tabia ya kuwapata watu wenye kinga ndogo ya mwili. Pia kwa wale wagonjwa wenye ukoma nao pia Wana tabia ya kuwa na kinga ndongo ya mwili kwa hiyo nao pia upatiwa dawa ya isoniazid Ili kuweza kuwakinga na kupata maambukizi ya kifua kikuu kwa sababu ya kuwepo kwa kinga ndongo ya mwili.

 

6. Kwa hiyo sio kwamba wagonjwa wanaopewa dawa ya kifua kikuu ya isoniazid ni wagonjwa wa Kifua kikuu Bali wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa Kifua kikuu wanapewa kama kinga, kwa hiyo dawa hii inaweza kutumiwa na wagonjwa waliotayari na maambukizi ya kifua kikuu pia na wale walio katika hatari ya kupata kifua kikuu, kwa hiyo wale wenye aleji na dawa hii hawapaswi kuitumia au kwa wale wanaoanza matibabu wakiona maudhi madogo madogo yamezidi na kuwa si ya kawaida ni vizuri kuomba msaada kwa wataalamu wa afya.

 

7. Dawa hii ya isoniazid Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea wakati wa kutumia maudhi hayo ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, kuharibu, maumivu ya kichwa, kuwepo kwa homa, kuwepo kwa vidonda vidogo vidogo kwenye mwili na matumizi ya mda mrefu ya dawa hii usababisha matatizo kwenye nefron,na pengine kwenye ini na kusababisha homa ya ini na nikwa kiwango kidogo na kwa watu wachache,kwa hiyo hayo ni maudhi madogo madogo ila yakiongezeka na kuwa yasiyo ya Kawaida ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya.

 

8. Pia dawa hii haiitumiki kiholela ni kwa maoni ya wataalamu wa afya na pia kabla ya kutumia dawa hii ni vizuri kabisa kupima kwanza ugonjwa na ndipo uanze kutumia dawa hii na pia kwa wale wanaotumia dawa hii kama tiba wasijisikiea vibaya hii ni dawa ya knga hasa kwa wale walio kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa Kifua na ukoma wakumbuke kwamba wanatumia kwa mda na watapumzika kwa sababu ugonjwa huu unapona na ni wengi wametibiwa na kupona na pia waliokwisha patw ugonjwa huu ni vizuri kabisa wakazingatia matibabu kwa Sababu ugonjwa huu unatibika.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Fahamu dawa zinazotumika kwenye matibabu ya kansa
Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli. Soma Zaidi...

image Namna ya kutumia tiba ya jino.
Posti hii inahusu zaidi namna au njia ya kufanya Ili kuweza kutumia tiba hii ya jino, kwa sababu ya mchanganyiko ambao umekwisha kuwepo kwa hiyo unachumua mchanganyiko unafanya kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Matibabu ya Fangasi ukeni na dawa za fangasi wanaoshambulia uke.
Fangasi wanaweza kushambulia uke, kwa juu kwenye mashhav ya uke ama kwa ndani. Hali hii inaweza kusababisha miwasho na maumivu pia. Inaweza kusababisha michubuko na kutofurahia tendo la ndoa. Makala hii inakwenda kukujuza dawa na matibabu ya fangasi ukeni. Soma Zaidi...

image Kazi ya chanjo ya Surua
Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya Surua kwa watoto, ni Aina ya chanjo ambayo utolewa kwa watoto na kufanya kazi mbalimbali mwilini ambazo ni kumkinga mtoto asipatwe na magonjwa. Soma Zaidi...

image Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)
Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria. Soma Zaidi...

image Fahamu dawa za kisukari
Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka. Soma Zaidi...

image Kazi za Dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria
Posti hii inahusu zaidi kazi za dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria kali, ni dawa ambayo inatumika sana kutibu Malaria kali. Soma Zaidi...

image Fahamu kuhusu dawa za kifua kikuu
Post hii inahusu dawa za kifua kikuu ni dawa ambazo utumika kutibu kifua kikuu, kwanza kabisa kabla ya kuanza kufahamu dawa hizo ni vizuri kabisa kufahamu kifua kikuu nini hili kuweza pia kufahamu dawa zake. Soma Zaidi...

image Fahamu dawa za 5-fluorouracil,Tegafur na uracili
Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa. Soma Zaidi...

image Ijue dawa ya paracetamol katika kutibu maumivu
Post hii inahusu zaidi dawa ya paracetamol katika kutibu maumivu, ni dawa inayosaidia kutibu maumivu ya Kawaida kama vile aspirin. Soma Zaidi...