Ifahamu dawa ya kutibu kifua kikuu

Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.

Ifahamu dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.

1.'1.Rifampsini ni mojawapo ya dawa ambayo imo kwenye daraja la kwanza katika matibabu ya kutibu kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba ni bakteria anayesababisha kuwepo kwa kifua kikuu, kwa hiyo dawa aina ya Rifampin inapotumika kitu cha kwanza ni kuharibu protein ambayo inaitwa DNA ni protein ya bakteria kwa hiyo bakteria huyo anakuwa Hana uwezo wa kuishi tena na ugonjwa uweza kuishia hapo kwa sababu DNA iimeshaharibiwa.

 

2. Katika matibabu ya kifua kikuu dawa hii kwa kawaida haitibu yenyewe kama yenyewe Bali huwa na mchanganyiko na madawa mengine ambayo ni isoniazid, pyrazinamide na ethambutol na dozi yake huwa na muundo wa RHZE ambapo, R ni Rifampin, H ni isoniazid, Z ni pyrazinamide na E ni ethambutol kwa hiyo dawa hizo utumika zote kwa pamoja katika matibabu ya kwanza ya kifua kikuu na katika matibabu ya pili Rifampin huwa na isoniazid na muundo wao huwa ni RH ambapo R ni Rifampin na H ni isoniazid .

 

3. Kwa kawaida dawa ya Rifampin utolewa kwa muundo wa vidonge yaana umezwa kwa maji. na ni mara chache mno Kuna Rifampin ambazo utolewa kwenye mishipa ya damu, katika dawa zote za kifua kikuu dawa hii ya Rifampin ndio iliyo na nguvu zaidi na usaidia katika kupambana na bakteria ambaye kwa kitaamu huiitwa TB bacill na pia dawa hii utumika katika daraja la kwanza na la pili katika matibabu ya kutibu kifua kikuu pia ni dawa yenye nguvu kwa sababu uua bakteria wote walio sugu na wote wanaaoanza mashambulizi .

 

4. Dawa hii pia huwa na maudhi madogo madogo katika kutumia, maudhi hayo ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, kuharisha, maumivu ya kichwa,na pia kuwepo kwa homa pia Kuna baadhi ya watu ambao huwa na viupele wanapokuwa wanatumia dawa hii ya Rifampin pia dawa hii inaweza kabisa kusababisha kupunguza kwa kwa kiasi cha aina ya protein ambayo Kwa kitaamu huiitwa platelate ,na pia kwa wakati mwingine kwa watumiaji wa dawa hii usababisha kupungua kwa kiwango cha damu kuganda .

 

5. Kiwango cha kupunguza kwa damu kuganda kwa kitaamu huiitwa clotting factors hali inayosababisha kupunguza kwa damu mwilini na kusababisha  hali Fulani ambayo Kwa kitaamu huiitwa Anaemia,na maudhi haya hayatokei kila mara ni mara chache na kwa watu wachache kwa hiyo watu wasiogope kutumia dawa hii kwa sababu ni sehemu ya matibabu .

 

6. Pia dawa hii inaweza kutumiwa na watu wote ila kwa wale ambao wanatumia uzazi wa mpango wenye vichocheo vya progesterone na oestrogen hawapaswi kutumia dawa hii kwa sababu dawa hii inaingiliana na hizi homoni na kusababisha kushika kwa mimba kwa sababu dawa hii ya Rifampin Ina nguvu kuliko hivi vichocheo kwa hiyo kwa wale wanaotumia dawa za kifua kikuu na pia wanatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango wanapaswa kuomba ushauri kwa wataalamu wa afya kwa sababu wanaweza kupata mimba bila kutegemea au wanashauliwa kutumia njia nyingine za uzazi wa mpango kwa sababu ni nyingi.

 

7. Pia na akina Mama wenye maambukizi ya kifua kikuu na wamegundulika siku za mwisho karibia na kujifungua na kwa bahati mbaya na watoto au mtoto aliyezaliwa na yeye ana maambukizi ya kifua kikuu, kwa hiyo mama ataendelea na dawa na mtoto ataanzishiwa  Rifampin kwa hiyo mama hapaswi kumnyonyesha mtoto kwa sababu atamzidishia dozi au nguvu ya dawa itakuwa kubwa yaani dawa inayopitia kwenye maziwa  ya mama na dawa anayokunywa mototo. Kwa hiyo mtoto huyo  hapaswi kunyonya.

 

8. Pia katika matumizi ya dawa hii ni vizuri kabisa kupata ushauri wa daktari dawa hii haipaswi kutumika kiholela na ikitokea mtumiaji wa dawa amepata maudhi yakawa yasiyo ya kawaida ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya kwa ushauri zaidi na pia kubadilishiwaa dawa kwa sababu katika matibabu ya kutibu kifua kikuu Kuna dawa za daraja la kwanza na la pili.

 

9. Pia kwa akina Mama wajawazito ni vizuri kabisa kupima kifua kikuu mapema Ili kuanza dawa mapema kuepuka na tatizo la kuambukiza mtoto na kusababisha mtoto kushindwa kunyonya kwa sababu maziwa ya mama ni ya muhimu na lazima kabisa kwa sababu mtoto asiponyonya ndicho chanzo cha utapiamlo na kidumaa kwa mtoto.

 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/16/Friday - 10:03:07 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 581

Post zifazofanana:-

Namna ya kuwasaidia wagonjwa wa vidonda vya tumbo
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa wa vidonda vya tumbo, ni njia ya kuwasaidia wagonjwa waliopata madonda ya tumbo Soma Zaidi...

Mambo yanayochangia Ili dawa kuingia kwenye damu vizuri
Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia Ili dawa iingie vizuri kwenye damu, na mambo yanayoweza kusababisha dawa kuingia au kutoingia vizuri kwenye damu. Soma Zaidi...

Zijue kazi za ovari
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa ovari kwenye mwili wa mwanamke. ovari ni sehemu ambapo mayai ya mwanamke hutunza, kwa hiyo kila mwanamke huwa na ovari ambayo husaidia kutunza mayai. Soma Zaidi...

Chanzo cha kiungulia
Post hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa kiungulia, kiungulia ni kitendo cha kupanda kwa gesi kutoka kwenye tumbo mpaka kwenye mdomo,hali uwasumbua wengi na kusababisha hali isiyo rafiki. Soma Zaidi...

Faida za nazi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nazi Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat Al-Kawthar
Sura hii ni miongoni mwa Sura fupi sanya huwenda ndiosura yenye aya chache kuliko sura zote katika Quran. Soma Zaidi...

Watu walio hatarini kupata fangasi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya watu walio hatarini kupata fangasi Soma Zaidi...

Siku ya sita ya wageni
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito faida na hasara zake Soma Zaidi...

Faida za kula apple (tufaha)
Posti hii itakwende kukueleza kuhusu faida za kula apple na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...

fahamu vitamini A na kazi zake
Je na wewe i katika wale ambaowanahitaji kujuwa kuhusu Vitamini A, kazi zake na vyakula vya vitamini A. post hii inakwenda kukujuza zaidi pamoja na historia ya vitamini A. Soma Zaidi...

Mzunguko wa mwezi kwa mwanamke
Posti hii inahusu zaidi mzunguko wa mwezi kwa mwanamke, ni mzunguko ambao huchukua siku ishilini na nane kwa kawaida Ila lla ubadilika kulingana na mtu, Ila ngoja tuangalie siku ishilini na nane tu. Soma Zaidi...