Post hii inahusu zaidi dawa ya cephalosporin katika kupambana na bakteria, ni mojawapo ya kundi kati ya makundi ya kupambana na bakteria ambalo ufanya Kazi kama penicillin.
1. Dawa hii ya cephalosporin katika kupambana na bakteria huwa kwenye magroup muhimu matatu ambayo ni kundi la kwanza Lina dawa ya cephalexin, Kundi la pili Lina dawa ya cefamandole na kundi la tatu Lina dawa ya ceftriaxone na celfdimir, makundi yote matatu ufanya Kazi kwa umoja na kuweza kupambana na bakteria na kutibu magonjwa mbalimbali kama tutakavyoona hapo mbeleni.
2. Magonjwa mbalimbali ambayo utibiwa na cephalosporin na makundi yake ni kuzuia maambukizi kwenye ngozi, yaani maambukizi yabayoambatana na viupele pamoja na miwasho, kuzuia maambukizi kwenye mifupa na kwennye joint, kuzuia maambukizi kwenye mfumo wa mkojo na maambukizi ya njia za mkojo kwa kitaamu huiitwa UTI, kuzuia maambukizi kwenye tumbo,pia kuzuia maambukizi kwenye sikio hasa ndani ya sikio.
3. Dawa hii inawezekana kupitia sehemu mbalimbali kama vile kwenye mdomo au sindano za matakoni na pajani au kwa wakati mwingine upitia kwenye mishipa ya damu , pia dawa hii ikishaingia kwenye mwili inawezekana kusambaa sehemu mbalimbali kama kwenye kondo la nyuma, kwenye maziwa kwa mama anayenyonyesha,na pia kweye maji maji ambayo yapo kwenye ubongo ambayo Kwa kitaamu huiitwa cerebral Spinal fluids.
4.pia dawa hii Kuna watu ambao hawapaswi kutumia na Kuna wale wanaopaswa kuitumia kwa taahadhari, ambao hawapaswi kutumia ni wale wenye alleji na cephalosporin na kwa na wale wenye aleji Kali na penicillin, na wanaopaswa kuitumia kwa taahadhari ni wenye ugonjwa wa Figo wanapaswa kutumia china ya uangalizi maalumu au pengine wapunguziwe dozi, na wale wenye ugonjwa wa kisukari watumie chini ya uangalizi maalumu na kwa akina Mama wenye mimba na wanaonyonyesha wanapaswa kuitumia kwa taahadhari au kwa uangalizi Fulani.
5. Pia dawa hii Ina maudhi madogo madogo kwa watumiaji na maudhi hayo yakizidi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kubadilishiwaa dawa au kupewa huduma nyingine muhimu na maudhi hayo ni kama vile kizunguzungu na kutapika, maumivu ya tumbo na kichwa, upungufu wa damu kwa watumiaji.
6. Pia dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela Bali utumika kulingana na wataalamu wa afya kwa sababu unaweza kutumia ukiwa nyumbani na hujui kama haipaswi kutumiwa atimaye unajiletea matatizo ya Bure.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1312
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Madrasa kiganjani
Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo
Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo. Soma Zaidi...
Vyakula vya wanga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya wanga Soma Zaidi...
Dawa za kutibu fangasi kwenye kucha
Makala hiii inakwenda kukueleza dawa za kutibu fangasi kwenye kucha. Soma Zaidi...
Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?
Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako. Soma Zaidi...
Dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya fluconazole.
Post hii inahusu zaidi dawa ya fluconazole ni dawa ya kutibu fangasi za aina au za sehemu mbalimbali, Soma Zaidi...
Neno la awali
Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya streptomycin
Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa. Soma Zaidi...
Dawa ya vidonda vya tumbo
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...
Fahamu dawa za cyclophosphamide na mustargen.
Post hii inahusu zaidi dawa za cyclophosphamide na mustargen katika kupambana na ugonjwa wa Kansa. Soma Zaidi...
Matibabu ya ugonjwa wa uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mgonjwa wa uti wa mgongo, kwa kawaida tunajua kuwa homa hii ya uti wa mgongo usababisha na wadudu mbalimbali kama vile bakteria, virus, fungasi, sumu mbalimbali kama vile madini ya lead na arseni, na vitu kama vile Mag Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya propranolol ambayo hutibu magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo. Soma Zaidi...