image

Ijue dawa ya kutibu ugonjwa wa ukoma

Post hii inahusu zaidi dawa ya kutibu ukoma,na dawa hiyo ni dawa ya Dapsoni, hii dawa usaidia kuzuia nerve zisiendelee kupoteza kazi yake pia na ngozi iendelee kuwa kawaida

Ijue dawa ya kutibu ugonjwa wa ukoma .

1. Ukoma ni mojawapo ya ugonjwa ambao uharibu nerve na mfumo mzima wa fahamu ambapo mgonjwa mara nyingi ushindwa kuhisi vitu vya hatari kama moto kwa sababu ya kuharibika kwa mfumo wa fahamu, pia na viungo kama vidole uweza kukatika yeye bila kuwa na taarifa yoyote Ile hali ambayo upelekea na ngozi ya mwili kutonawili ,kwa hiyo hata jamii uwatenga wagonjwa hawa, kwa matumizi ya dawa ya dapsoni utibu uaribifu wa nerve na kuzuia uaribifu wa ngozi na kumweka mgonjwa kwenye hali nzuri na akakubarika katika jamii.

 

2. Dawa hii kwa kawaida IPO kwenye mfumo wa vidonge na utumiwa kila kila siku kwa kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya, matibabu ya ugonjwa huu dawa uanza kutumika kidogo kidogo na baadae dozi uongezeka kuanzia mwezi wa kwanza mpaka wa pili, na matibabu yake ni marefu kidogo kwa sababu utumia takribani miezi kumi na minane na matibabu yanaweza kuendelea kwa kutegemea hali ya mgonjwa kwa sababu kuna wagonjwa ambao uanza matibabu mwanzoni mara tu wanapoona dalili Ila Kuna wale wanaoanza kwa kuchelewa na Kuna wale wanaofuatwa kutoka majumbani kwao kwa kulazimishwa Ili kuzuia kuendelea kuongezeka kwa ugonjwa.

 

3. Kwa sababu tofauti tofauti na matibabu utofautiana kwa sababu Kuna wanaopenda kupona haraka, Kuna ambao hawajali na Kuna wanaolazimishwa kutumia dawa, kwa hiyo kupona utegemea bidii ya mgonjwa kuanza matibabu na uaminifu katika matumizi ya dawa, dawa hii ikitumiwa uweza kukaa mwilini kuanzia masaa mawili mpaka masaa nane baada ya kuitumia, kwa hiyo ikitumiwa tu uenda kufanya kazi kwenye ngozi,nyama za mwili kwa kitaamu muscle na pia dawa hii inaenda kwenye ini na kweye Figo ambapo inawezekana kukaa kwa mda wa wiki tatu hivi, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wanapaswa kunywa sana maji Ili kuweza kuondoa sumu ya dawa inayokaa kwenye ini na Figo.

 

4. Dawa hii inatumika na watu wenye ukoma na pia wale ambao Wana dalili za ukoma na haujajitikeza kwa kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya na pia watu ambao hawapaswi kutumia dawa hii ni wale wenye aleji na dapson drug na pia wale ambao maudhi madogo madogo yamekuwa mengi kiasi cha kwamba hawezi kuendelea kutumia dawa hii.

 

5. Pia katika matumizi dawa hii huwa na maudhi madogo madogo kama vile kichefuchefu na kutapika, kuharisha mapigo ya moyo kwenda mbio, maumivu ya kichwa, mwili kukosa nguvu kukosa hamu ya kula,ikiwa maudhi haya yameongezeka zaidi ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya na pia maudhi madogo madogo kwa wagonjwa wa ukoma ni makubwa kidogo kwa hiyo jamii inapaswa kuwa karibu na wagonjwa hawa kuepuka tabia mbaya ya kuwanyanyapaa na kuona  kwamba sio binadamu , wanapaswa kutunzwa vizuri kwa sababu dawa wanazozitumia ni kali.

 

6. Pia kwa wale walio na matatizo ya moyo na presha wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa Ili kuweza kupata ushauri zaidi na pia dawa hizi hazitolewi kiholela holela Bali ni kwa utaratibu wa wataalamu wa afya.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1248


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Fahamu kuhusu dawa za magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa za magonjwa ya moyo, ni dawa ambazo utumika kusaidia pale moyo kama umeshindwa kufanya kazi ipasavyo. Soma Zaidi...

Dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na dawa ya maumivu ya hedhi Soma Zaidi...

Kazi za Dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria
Posti hii inahusu zaidi kazi za dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria kali, ni dawa ambayo inatumika sana kutibu Malaria kali. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za 5-fluorouracil,Tegafur na uracili
Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa. Soma Zaidi...

Dawa ya Panadol au paracetamol katika kutuliza maumivu
Posti hii inahusu zaidi kazi ya paracetamol katika kutuliza maumivu, ni Aina ya dawa ambayo utumiwa sana katika kutuliza maumivu kwa wagonjwa. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya griseofulvin
Post hii inahusu zaidi dawa ya griseofulvin ni dawa inayotumika kutibu fangasi za kwenye ngozi ambazo usababisha mabaka mabaka kwenye ngozi. Soma Zaidi...

Dawa ya fluconazole kama dawa ya fangasi
Post hii inahusu zaidi dawa za fangasi na matumizi yake kwa kutumia dawa ya fluconazole kama dawa mojawapo ya fangasi. Soma Zaidi...

Faida za vidonge vya antroextra
Posti hii inahusu zaidi faida za vidonge vya antroextra, ni vidonge kwa ajili ya mifupa, viungo na gegedu, hivi vidonge vimetumiwa na watu wengi na matokeo yake ni mazuri sana, kwa hiyo zifuatazo ni faida za vidonge hivi. Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa, ni mojawapo ya dawa kwenye kundi la beta blockers na pia uhusika katika matibabu ya magonjwa ya moyo kama nyingine. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya mucolytic dawa ya kutibu kikohozi
Post hii inahusu zaidi dawa ya mucolytic katika kutibu kikohozi kwa watu wazima na watoto. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya marcolides dawa ya kuuwa bakteria, kwenye mfumo wa hewa
Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w Soma Zaidi...