Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)

Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)

Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria.

Ijue dawa ya  Sp.

1. Kama tulivyotangulia kusema kwamba ni dawa ambayo ina majina mawili ambayo ni sulphadoxine na pyrimethamine ambayo uunda dawa hii ya Sp, dawa hii iko kwenye mfumo wa vidonge ambapo kila sehemu ina milligrams zake ambapo sulphadoxine ina milligrams miatano na pyrimethamine ina miilgram ishirini na tano jumla kuu ufanya miligramu mia tano ishirini na tano.

 

2. Dawa hii utumika sana kwa wanawake wajawazito na haipendekezwi kama mojawapo ya dawa za kutibu malaria kwa sasa, ila kwa wajawazito ikitokea wakapata malaria ingawa wanatumia sp matibabu yao wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya ili wawaeleze cha kufanya.

 

3. Kwa akina Mama wajawazito wanapaswa kutumia vidonge hivi vya sp pindi wanapogundua kwamba ni wajawazito kwa sababu vidonge hivi vikimezwa uenda moja kwa moja mpaka kwenye sehemu ya mwanzo ya kondo la nyuma na kuweza kuzuia wadudu wanaosababisha malaria kutoingia kwenye kondo la nyuma na kusababisha madhara mbalimbali kama vile mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, mtoto kutokuwa na afya nzuri akiwa tumboni, au mimba kutoka.

 

4. Kwa hiyo akina mama wanapaswa kujua kabisa kwamba hizi dawa ni za muhimu sana wakati wa ujauzito kwa sababu bila matumizi ya dawa hizi madhara makubwa yanaweza kutokea ambayo usababisha kukosa mtoto, au mimba kutoka, mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, haya matatizo utokea kwa sababu ya kuwepo kwa wadudu wa malaria kwenye kondo la nyuma na kusababisha uharibifu kwenye sehemu hiyo.

 

5. Akina mama wote wanapaswa kutumia dawa hizi isipokuwa wale wenye aleji na sulphur , au wanaotumia dawa ambazo kwa kitaalamu huitwa cotrimoxazole au wale wamama ambao wamegundulika na malaria kwa hiyo wanapaswa kufuata kawaida ya matibabu ya ugonjwa wa malaria kadri ya wataalamu wa afya.

 

6. Kwa hiyo akina mama wenye imani potovu kuhusu dawa hizi wanapaswa kujua kwamba dawa hizi ni za muhimu sana na kutotumia dawa hizi ni hatari sana hasa kwa afya ya mtoto.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views: 7694

Share On:

Share follows: 1 | Unique share links followed: 1
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 web hosting     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Dawa ya kutibu macho

Hizi ndio dawa za macho yenye ukavu, kuwasha ama kutoa machozi

Soma Zaidi...
Dawa ya fangasi na dalili za fangasi

hapa utajifunza dalili za fangasi, dawa ya fangasi na aina za fangasi, pia nitakujuza njia za kukabiliana na fangasi

Soma Zaidi...
Fahamu kazi ya dawa ya ampicillin inayopambana na maambukizi ya bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin

Soma Zaidi...
Dapsone na kazi zake

Posti hii inahusu zaidi dawa ya Dapsone na kazi zake, hii ni dawa ambayo utumika katika kutibu ugonjwa wa ukimwi, dawa hii ufanya kazi kwa mchanganyiko wa dawa nyingine kama vile Rifampicin na clofaximine.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya haloperidol katika matibabu ya akili

Post hii inahusu dawa ya haloperidol katika matibabu ya magonjwa ya akili, ni mojawapo ya dawa ambayo utumiwa na wagonjwa ambao wamechananyikiwa.

Soma Zaidi...
Fahamu matumizi ya Dawa iitwayo Aspirin.

Aspirini Ni dawa ya kutuliza maumivu.Majina yanayoaminika zaidi katika kutuliza maumivu sasa yanapatikana kwa njia mbadala inayookoa gharama kwa kutumia Aspirini. Aspirini inayopendwa na familia kwa miongo kadhaa, mara nyingi hutumiwa kupunguza maumivu y

Soma Zaidi...