Ijue timu ya upasuaji

Ijue timu ya upasuaji

Posti hii inahusu timu ya upasuaji hii ni timu ambayo inahusika katika chumba cha upasuaji, kwa sababu ya kutunza usafi na usalama chumba hiki kinapaswa juwa na timu ya watu wanne na walio na elimu kuhusu kazi hiyo.

Timu ya upasuaji.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa upasuaji ni hali ya kurekebisha sehemu fulani kwenye mwili au kutoa kiungo chochote kwenye mwili au kusafisha kutokana na uchafu ulio kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo kazi hii inahitaji usafi wa hali ya juu kabisa ili kuweza kuepuka Maambukizi kutoka kwenye mwili wa binadamu kwenda kwa mgonjwa kwa hiyo wafuatao ni wahudumu kwenye chumba cha upasuaji.

 

2. Mhudumu wa kwanza ni yule anayefanya usafi kwenye chumba cha upasuaji.

Huyu mhudumu sifa ya kwanza anapaswa kuwa ni  nesi aliyesajiliwa na kupata mafunzo kutokana na kazi hiyo kwa hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa chumba kinakuwa kwenye hali ya usafi na hakuna vumbi yoyote ambayo inakuwepo kwenye chumba hicho na kuhakikisha kuwa kuna hewa inayopaswa kuwepo kwenye chumba hicho cha upasuaji.

 

3. Mhudumu mwingine ni msafisha vifaa vya upasuaji.

Tunajua wazi vifaa vinavyotumika kwenye upasuaji ni vifaa ambavyo utumika kwa mgonjwa mmoja na mwingine kwa hiyo mhudumu huyu anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu kusafisha vyombo hivyo kwa hiyo kabla ya kufanya upasuaji anapaswa kuhakikisha kubwa vyombo vyote vipo na vinafanya kazi kwa hiyo vyombo hivyo visiposafishwa vizuri usababisha maambukizi kwa mgonjwa.

 

4. Mtoa huduma ya  usingizi.

Huyu ni mmojawapo ambaye anapaswa kutoa dawa ya usingizi kufuatana na mda ambao dawa inapoisha kwenye mwili wa mgonjwa kwa hiyo huyu ndiye anapaswa kuwaambia wafanya upasuaji kutumia mda ili upasuaji uishe kabla ya dawa kuisha kwenye mwili kwa hiyo huyu pia uhakikisha kuwa mgonjwa anapumua vizuri na mapigo ya moyo yako sawa na kuhakikisha kuwa  upasuaji unaenda vizuri.

 

5. Mfanya upasuaji au kwa jina lingine ni daktari.

Huyu ni mhusika mkuu wa upasuaji ambaye ndiye anakuwa ana utaalamu katika upasuaji kwa sababu anakuwa na ujuzi kwa hiyo wahudumu wengine wanapaswa kumsaidia sana kwa sababu ya shughuli kubwa aliyonayo kwa hiyo huyu anapaswa kuwa na ujuzi wa kutosha kabisa

 

 

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views: 2146

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 ai web app     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

utaratibu wa lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
AINA ZA VYAKULA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Sababu za Upungufu wa Nguvu za Kiume

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali inayomtokea mwanaume kushindwa kupata au kudumisha nguvu ya uume inayotosha kwa ajili ya tendo la ndoa. Tatizo hili linaweza kuwapata wanaume wa rika tofauti, ingawa huonekana zaidi kadri umri unavyoongezeka. Sababu zake zinaweza kuwa za kiafya, kisaikolojia, kimazingira au mtindo wa maisha. Watu wengi huona aibu kuzungumzia tatizo hili, lakini kitaalamu ni hali inayoweza kutibika endapo chanzo chake kitagunduliwa mapema.

Soma Zaidi...