Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?

Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?

Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?


Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislam kwa sababu zifu atazo:
Kwanza, elimu ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua Mola wake vilivyo na kumuabudu ipasavyo kwa unyenyekevu kama Qur-an inavyothibitisha:



'... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalam (waliozama katika fani mbali mbali)' (35:28).


Pili, elimu iliyosomwa kwa mrengo wa Qur-an ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa Ulimwenguni. Khalifa ni mja anayetawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) kwa kufuata kanuni na sheria zake. Nabii Adam (a.s) aliwathibitishia Malaika kuwa ana uwezo wa kuutawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) baada ya kuelimishwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) na kuahidiwa mwongozo kutoka kwa Allah (s.w).



Tatu, kutafuta elimu ni Ibada maalumu ya hali ya juu kuliko Ibada zote. Kwa mujibu wa Qur-an Swala ni Ibada maalumu ya hali ya juu na ni dhikri kubwa au zingatio kubwa juu ya Allah (s.w)


' Hakika swala humzuilia (mja) na mambo machafu na maovu na ni dhikri kubwa kwa Allah (s.w)' (29:45).



Pia katika Hadith Mtume (s.a.w) amesisitiza: 'Nguzo kubwa ya Dini (Uislamu) ni swala, mwenye kusimamisha swala kasimamisha Dini na mwenye kuacha sw ala kavunja Dini.'
Hivyo kwa mujibu wa Qur-an na Hadith sahihi za Mtume (s.a.w), swala ni Ibada yenye hadhi ya juu kuliko Ibada zote mbele ya Allah (s.w); lakini bado Ibada ya kutafuta elimu inachukuwa nafasi ya juu zaidi kuliko swala kwani swala haiwezi kusimama bila ya kuwa na ujuzi stahiki.
Nne, mwenye elimu ananafasi bora ya kumuabudu Mola wake inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake kama inavyosisitizwa katika Qur-an:


'... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu' (35:28)
Pia Qur-an inasisitiza juu ya umuhimu wa elimu kwa kuuliza:


' Je, waweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.' (39:9)
Kimsingi wanaojua wanatarajiwa wafanye mambo kwa ufanisi zaidi kuliko wasiojua. Kwa msingi huu Allah (s.w) anasisitiza tena katika aya ifuatayo:



'Mwenyezi Mungu ataw ainua (daraja) w ale w alioamini miongoni mwenu, na waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote' (58:11)
Hivyo, kutokana na aya hizi (35:28, 39:9 na 58:11) tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wana daraja zaidi kuliko waumini wengine kwa sababu wanao uwezo zaidi wa kuona dalili za kuwepo Allah (s.w) na utukufu wake kwa undani zaidi, jambo ambalo huwapelekea kumuogopa Mola wao na kumuabudu inavyostahiki katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao kama inavyobainika katika aya zifuatazo:


'Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonesha kuw epo Allah (s.w) kwa wenye akili. (3:190)


Ambao humkumbuka Mw enyezi Mungu w akiwa wima, wakiwa wamekaa na wakiwa wamelala. Na hufikiri (tena) umbo la mbingu na ardhi (wakasema) Mola wetu! Hukuviumba hivi burebure tu. Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu ya moto.' (3:190).
Pia kutokana na aya hizo tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wanao uwezo mkubwa wa kufanya mambo kwa ufanisi jambo litakalowapelekea kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 368

Post zifazofanana:-

JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Zabibu
Soma Zaidi...

TAHARUKI YA MFALME WA BAGHADANI
Soma Zaidi...

KISIWA CHA UOKOZE CHA PILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nilikwenda mpaka nikakuta misitu minene na nisijuwe pa kuenda. Soma Zaidi...

HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

MAAJABU YA VIUMBE
MAAJABU YA VIUMBE Dunia ina maajabu sana lakini viumbe wana maajabu pia. Soma Zaidi...

Faida za kula Karoti
Umeshawahi kula karoti mbichi, ama ya kupikwa, je unazijuwa faida zake? soma makala hii Soma Zaidi...

Msafara wa vita vya Tabuk Dhidi ya Warumi
Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A. Soma Zaidi...

vyakula vya kuongeza damu, dalili zake na sababu za upungufu wa damu
Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu Soma Zaidi...

Kitabu Cha Afya na Lishe
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...

WAQFU WAL-IBTIDAAI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...