Jaribio la kwanza la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI

Siku moja Aladini alipokwenda kuwinda yeye na wafanyakazi wa Mfalme nyuma alikuja yule mchawi aliyemtelekeza Aladini kule mapangoni. Ukweli ni kuwa mchawi aliyekutana na waziri mkuu kule nchi za Afrika alikuwa ni yule mchawi aliyekutana na Aladini na kujifanya ni Baba mdogo na Aladini. Mchawi yule alitambua fika kuwa Aladini hawezi kutembea na ule mshumaa kwa ni ni kitu cha thamani sana. Alikuja mchawi yule katika sura ya mfanya biashara na kujifanya anabadili vitu vya zamani kwa vipya. Alipokuja kwa Aladini akajifanya anabadili mishumaa ya zamani kwa mipya. Ukweli ni kuwa alikuwa na vipande vya mishumaa vilivyo vizuri.

 

Alikuwa na mishumaa yenye rangi ya samawadi iliyo ang’avu sana, mishumaa ya rangi nyeusi na myeupe. Pia alikuwa na mishumaa ya madoamadoa. Alinukia miski mishumaa hiyo kama vile udi uluotengenezwa Yemeni. Mchawi huyu alipofika kwa Aladini akanadi sana na kuwasha mishumaa ile na kueneaharufu nzuri ya mishumaa. Hapo akasema kama ndani kuna vitu vya zamani ama mishumaa ya zamani isiyotumika mimi nabadilisha na mipya. Pale binti Mfalme kwa kuwa alishalewa na harufu ya mshumaa wa rangi wa mchawi. Mshumaa ambao haukuwaka moto ila yalikuwa ni mazingaombe. Kilevi hiki kilmfanya binti sultani kuingia nda wenda tafuta mhumaa.

 

Hatmaye akaja na kipande cha mshumaa wa ajabu. Mshumaa wa Aladini alioupata mapangoni. Yule mchaw alipoushika tu mshumaa ule kiza kinene kilitokea pale na ndani ya sekunde chache hapakuwa na chochote kile. Ilikuwa ni kana kwamba hapakuwa na kitu toka mwanza. Mchawi hauweza kuacha alama yeyote ile. Mfalme akiwa ikulu alkuwa akchungulia kwa dirishani jumba la Aladini. Lakini leo alishangaa hakuweza kuoa chochote. Muda huo huo mfalme hakuamn kumuna wzir wake. Mfalme alisalimiana na waziri kwa furaha. Lakini waziri kwa kuwa alijuwa kila kitu akaanza kumkandia Aladini kuwa ni mchawi sana na kumzulia mengineyo.

 

Mfalme akaagiza Aladini aletwe sasa hivi. Aladini alishangaa kundi la askari kumtia mbaroni na kumpekeka kwa Mfalme. “nieleze mwanangu yupo wapi, umemfanya nini na ipo wapi nyumba yako”yalikuwa ni maswali ya haraka ya mfalme. Aladini alishindwa kujibu maswali yote alioangalia hakuweza kuona jumba lake. Kwa hasira mfalme akaagiza kichwa cha Aladini kikatwe. Hapo aladini akamuomba msamaha Mfalme na kumuomba angalai siku tatu aweze kumrudisha mkewe. Na kama akishindwa akatwe kichwa. Mfalme akakubali kmpa Aladini siku saba.

 

Aladini alifika kwake na kuanza kulia sana. Kulia hakuku saidia akaenda kwa mama yake na kumueleza kila kkitu. Kisha aladini akamuita jini wa kwenye pete yake na kumuuliza kama anaweza kurudisha nyumb na mke. Jini wa pete kaeleza kuwa hawezi kurudisha chochote kilichofanywa na jini wa mshumaa. Hivyo Aladini akamtaka jini wa pete ampeleke mahali nyumba yake ilipo. Punde aladini akawa yupo dirishani kwenye nyumba yake huko maeneo ya Afrika. Masiini mke wake alikuwa akilia. Alladini alipojiridhisha kuwa yule mchawi hayupo ndani akamuita mkewe na kuzungumza naye.

 

Ladini akampatia mkewe maelekezo juu ya nini afanya na pia akamueleza vyocyote kuwa kuna mshumaa ulimpatia. Mwanamke akakiri ni kweli. Hapo aladini akamueleza mkewe siri nzima ya mshumaa. Lengo hasa la mchawi ilikuwa ni kumuuwa Aladinni na amchukuwe binti mfalme kuwa wake. Mchawi alikuwa akimsisitizia binti mfalme kuwa Aladini ameshakufa hivyo hana bidi kumkubali yeye.

 

Siku hiyo binti mfalme akaoga na kujipamba vizruri. Kisha akaweza glasi mbili za vinywaji huku akimsubiri mchawi aje. Mchawi alipokuwa alistaajabishwa na urembo wa mtoto. Mtoto akamkumbatia mchawi na kumwambia “nimekata shauri kuwa aaladini amekufa, hivyo nipo kwa ajili yako sasa, naomba tufurahie leo”. mchawi aliruka kwa furaha. Hapo binti mfalme akafukuwa bilauri ya kinywaji na kumpatia mchawi kisha wakaanza kunyweshana. Haukupita muda mchawi kakakata roho. Kumbe kinywaji kile kilikuwa na sumu.

 

Aladini alipojiridhisha kifo cha mchawi akachukuwa mshumaa, kisha akamzika mchawi. Aladini kwa kutumia jini wa mshumaa haikuchukuwa muda jumba la Aladini likarudi pale lilipo. Mfalme alifurahi sana na kwenda kumsalimia mwanaye na kumpa pole aladini. Aladini akamueleza mfalme kila kitu kuhusu mshumaa na pete. Basi maisha yakaendelea vizuri hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya tukio lolote.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1303

Post zifazofanana:-

Faida za kula bamia
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida ambazo anaweza kupata mwanadamu Kama akila bamia Mara kwa mara. Bamia huliwa Kama tunda au Kama mboga pia na husaidia vitu vingi mwilini. Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba Soma Zaidi...

Jinsi ya kupata mtoto wa kiume
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nadharia ya kupata mtoto wa kiume. Soma Zaidi...

Sababu ya maumivu ya magoti.
Posti hii inahusu zaidi sababu za maumivu ambayo yanasikika kwenye magoti, huu ni ugonjwa ambao umewapata walio wengi na bado ni kilio kwa walio wengi kwa vijana na kwa wazee, Kuna wataalamu mbalimbali ambao wameweza kugundua sababu za maumivu kwenye mago Soma Zaidi...

Mkojo usio wa kawaida huwa na vitu vifuatavyo.
Posti hii inahusu zaidi Aina ya mkojo usiokuwaa wa kawaida uwa na vitu vifuatavyo, ukiona dalili kama hizo wahi mapema hospitalini Ili upatiwe huduma. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kuharisha na sababu zake.
Kuharisha ni Hali ya kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisicho na damu Soma Zaidi...

Safari saba za sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote
Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu) Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)
Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini. Soma Zaidi...

Watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango
Post hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango, Ni watu ambao Wana matatizo mbalimbali endapo wakitumia wanaoweza kuleta madhara mbalimbali. Soma Zaidi...

Namna ugonjwa wa herpes simplex unavyosambaa.
Posti hii inahusu zaidi namna ya ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Soma Zaidi...

Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji. Soma Zaidi...