JAVASCRIPT - somo la 2: Jisi ya ku print output ya code za javascript.

JAVASCRIPT - somo la 2: Jisi ya ku print output ya code za javascript.

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript.

JAVASCRIPT OUT PUT

Hapa tutajifunza namna ambavyo unaweza kuonyesha matokeo ya code javascript. Yaani ilikwamba hizo code ulizoandika zionyeshe matokeo yanayotarajiwa. Kama umejifunza kuhusu PHP tunatumia print ama echo. Sasa vipi kwenye javascript nini tutatumia. Endelea na somo hili hadi mwisho.

 

Kabla hatujaendelea na somo zaidi, naamini unatumia text editor. Kama unatumia simu unaweza kutumia trebEdit. Kama unatumia komputa unaweza kutumia sublime text. Unaweza pia kutumia notepad, notepad plus, ama text editor yeote. Hakikisha pia una ufahamu kuhusu html angalau basic level.

 

Ni njia zipi javascript hutumia kuonyesha output

Kuna njia 4 ambazo hutumika kwenye javascript kuonyesha output. Njia hizo ni:-

  1. Kwa kutumia innerHTML

  2. Kwa kutumia document.write()

  3. Kwa kutumia window.alert()

  4. Kwa kutumia console.log()

 

  1. Kwa kutumia innerHTML  propert

Property hii hutumika kwa ajili ya ku badili maudhui ya kwenye html element, ama ku modify maudhui, ama kuweka maudhui mapya kwenye elemeny ya html. Mara nyingi hutumika kwenye element <p> lakini inawekza pia kutumika kwenye <div> na maeneo mengine.

 

Hii hutumika katika kufikia element za HTML. kwanza utahitajika element husika kuipa id, kisha utatumia hiyo id ili uweze kuifikia kwa kutumia javascript.

Mafano:

 

<!DOCTYPE html>

<html lang="swa">

<body>

<p id="mfano"></p>

 

<script>

   document.getElementById("mfano").innerHTML = 'haloo javascript';

</script>

 

</body>

</html>

Kwanza element p tumeipa id ya mfano <p id="mfano"></p> Hii inamaanisha maudhui ya kwenye element p yatapatikana baada ya id ya mfano kufikiwa kwenye javascript. Ili kuweka id kwenye html element ni kama unavyotaka kuweka html attributes. Utaanza kuweka tag ya element mafano <p kisha itafata attribute id <p id itafuatiwa na alama ya = <p id = thamani ya id yaani value itakuwa ndani ya alama hizi “” kisha funga element yako <p id="mfano"></p>   Baada ya hapo kinachofuawata ni kuweka code za javascript.

 

Tambuwa kuwa code zote za javascript huwekwa ndani ya tag za javascript. Tag za javascript ni <script> hii ni ya kufungua na </script> hii ni ya kufunga. Sasa kinachofuwata ni kuitumia id ili kuweza kupata matokeo ya javascript.

 

Hapa tutatumia document.getElementById() ili kuweza kuifikia id ya element yetu. Kwenye mabano hapo weka id yetu ambayo ni mfano document.getElementById("mfano") baada ya hapo kinachofuata ni kytumiaproperty ya innerHTML  ili kuweza kuipa maudhui mapya elemebt yetu. Inafuata alama ya = kisha maudhui yako utaweka hapo. Kama ni string yaani mkusanyiko wa herufi na namba ama herufi tupu maudhui hayo yatakuwa ndani ya funga na fugua semi “”. Mfano wetu juu hapo tunataka kuonyesha maneno haloo javascript. Hivyo itakuwa document.getElementById("mfano").innerHTML = 'haloo javascript'; Kma ingelikuwa namba tungeweka document.getElementById("demo").innerHTML = 5 + 6;              

 

Angalia mfano:-

<!DOCTYPE html>

<html lang="swa">

<body>

<p id="mfano"></p>

<div id="mfano2"></div>

<script>

   document.getElementById("mfano").innerHTML = 'haloo javascript';

   document.getElementById("mfano2").innerHTML = 5 + 6;

</script>

</body>

</html>

...

Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: JavaScript Main: ICT File: Download PDF Views 500

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

JAVASCRIPT - somo la 17: condition statement za if else, else if kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 17: condition statement za if else, else if kwenye javascript

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu condition statemant. Darasa hili ni moja katika madarasa muhimu programming. Katika somo hili tutajifunza kwa vitendo zaidi. Tutatumia mifano ya somo lililo tangulia.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 14: Jifunze kuhusu event kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 14: Jifunze kuhusu event kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu javascript events. Event ni neno la Kiingereza lenye maana tukio wingi wake events kumaanisha matukio. Natumia ni kila ambacho kinatokea kwenye javascript.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 11: function maalumu zinazotumika kwenye string yaani string method
JAVASCRIPT - somo la 11: function maalumu zinazotumika kwenye string yaani string method

Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.

Soma Zaidi...
Game 2: Jinsi ya kutengeneza tic toc game ya single player kwa kutumia javascript, html na css
Game 2: Jinsi ya kutengeneza tic toc game ya single player kwa kutumia javascript, html na css

Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 6: Jinsi ya kufanya mahesabu kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 6: Jinsi ya kufanya mahesabu kwenye javascript

Katika somo hili utajifunza kuhusu matendo ya hesabu ambayo ni kugawanya, kujumlisha, kuzidisha na kutoa

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 12: Function zinazotumika kwenye namba
JAVASCRIPT - somo la 12: Function zinazotumika kwenye namba

Katika somo hili utajifunz kuhusu baadhi ya function ambazo hutumika kwenye namba

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 9: Jinsi ya kuandika function kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 9: Jinsi ya kuandika function kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT -somo la 1: Kwa nini ni muhimu kujifunza javascript
JAVASCRIPT -somo la 1: Kwa nini ni muhimu kujifunza javascript

Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 15: Jinsi ya kukusanya user input
JAVASCRIPT - somo la 15: Jinsi ya kukusanya user input

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript
JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript

Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika.

Soma Zaidi...