picha

JAVASCRIPT - somo la 3: sheria za uandishi wa code za javascript yaani syntax za javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript.

 

Katika somo hili utajifunza kanuni za kuandika code za javascript ama javascript statement.Lamda kwanza nianze kukujuza maana ya hili neno statement. Ni kuwa kwenye program ya kikompyuta kuna code amabazo ni maelekezo ambayo kompyuta hupewa ili kufanya jambo fulani. Sasa hizi code ama haya maelekezo ndio huitwa statement.

 

Katika somo hili utajifunza kanuni za kuandika hizi statement. Kanuni hizi zitaweza kukuongoza kwa ufupi uweze kugunduwa kama kwenye code zako kuna tatizo. Na kama lipo nini kimesababisha. Hivyo tutajifunza syntax ya javascript.

 

Kabla hujasonga mbele zaidi na somo hili, nikujuze kuwa javascript statement inaweza kuwa na vitu hivi Values, Operators, Expressions, Keywords, na Comments. Value ni thamani ambazo zinaweza kuwa ni thamani za variable, operator ni alama za kihesabu kama + kumaanisha jumlisha, Expression ni mkusanyiko wa variable, value na operator, na comment hapa ni sehemu ambayo programmer ama mtu anayeandika hizo code kuweka kumbukumbu zake, ili baadaye aweze kukumbuka.

 

Kanuni za kuandika javascript:

  1. Matumizi ya semicolon (;)

Weka alama hii ya semicoloni mwishoni mwa ststement yako. kwa mfano:

Mfano: 1

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

   let x, y, z;

   x = 5;

   y = 6; 

   z = x + y;

 

   document.getElementById("demo").innerHTML =

       "The value of z is " + z + ".";

</script>

 

</body>

</html>

Hapo juu utaona mwishoni mwa kila msitari kuna alama ya semicolon. Pia unaweza kuunganisha statement nyingi katika msitari mmoja na kutenganisha kwa semicoloni. 

Mfano 2

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

   let x, y, z; x = 5; y = 6; z = x + y; document.getElementById("demo").innerHTML = "The value of z is " + z + ".";

</script>

 

</body>

</html>

Matokeo ya statement ya kwanza, na ya pili ni sawa, ijapokuwa hii ya pili ina mistari kidogo ya code, ni kwa saabu imeunganishwa pamoja na kutengenishwa kwa alama ya semicolon kwa kila statement.

 

  1. Kuruka nafasi wakati wa uandishi (White Space):

Ni kuwa wakati unaandika huwa tunaruka nafasi, huwenda zikawa nyingi ama moja. Sasa katika javascript nafasi ambayo itahisabika kwenye code ni moja tu, hizo ambazo umeongeza javascript hazita zitambuwa na hasita athiri matokeo ya code zako. 

 

Hivyo unaweza kuruka nafasi kadiri uwezavyo, ili kuweza kuboresha muonekano wa code zako. Angalia mifano ya code hizo hapo chini majibu yake ni sawa.

Mfano 3

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

    document.getElementById("demo").innerHTML = "haloo javascript";

</script>

 

</body>

</html>

Mfano wa 4

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

    document.getElementById        ("demo").       innerHTML             =           "haloo                   javascript";

</script>

 

</body>

</html>

  1. Urefu wa msitari wa code

urefu wa msitari wa code hauwezi kuathiri matokeo ya code. Hata hivyo inashauriwa usizindi chara">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2023-10-19 Topic: JavaScript Main: ICT File: Download PDF Views 1245

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

JAVASCRIPT - somo la 4: Jinsi ya kuandika variable kwenye javascript

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 15: Jinsi ya kukusanya user input

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.

Soma Zaidi...
Game 1: Jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawili kwa kutumia html, css na javascript

Katika post hii utakwenda kujifundisha jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawii kwa utumia html, css na javascript

Soma Zaidi...
Game 3: Mchezo wa kufikiria namba kwa kutumia javascript

Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 11: function maalumu zinazotumika kwenye string yaani string method

Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 18: Jinsi ya kutumia switch case kwenye javascript

Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 19: Jinsi ya kutumia loop kwenye javascript

Katika somo hilibtutakwenda kujifunza kuhusu loop. Katika programming tunaposema loop tunamaanisha ile hali ya program ku excute code zaidi na zaidi. Tofauti na kurudia rudia kuandika statement moja kwa ajili ya kupata matokeoa hayohayo basi unapotumia lo

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT -somo la 1: Kwa nini ni muhimu kujifunza javascript

Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.

Soma Zaidi...
Game 2: Jinsi ya kutengeneza tic toc game ya single player kwa kutumia javascript, html na css

Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 7: Jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu.

Soma Zaidi...