image

Je ni kwa nini lengo la finga halifikiwi kwa wafungaji

Lengo la funga ni kuwa mchamungu sasa ni kwa nini wafungaji hawalifikii lengo hili na kuwa wachamungu.

Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi?

Amri ya kufunga imeambatanishwa na lengo lake. Lengo la funga ni kuwafanya wafungaji wawe wacha-Mungu. Lakini maswali ya kujiuliza: Ni kweli watu wanafunga vile ipasavyo? Je, watu wengi hawaanzi kufunga kwa vunja jungu ambapo baadhi ya Waislamu wanaotarajia kufunga Ramadhani humuasi Mola wao tani yao siku ya mwezi 29 au 30 Shaabani? Je, baada ya kufuturu baadhi ya Wafungaji hawajiingizi kwenye laghwi - kucheza karata, bao, mabishano, uvutaji sigara, mazungumzo ya upuuzi, na kadhalika - mpaka utakapoingia wakati wa daku? Je, siku ya Iddil-Fitri baadhi ya waliofunga hawajiingizi katika kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w) katika kiwango cha hali ya juu kwa kujihusisha na ulevi, uzinifu, kamari na ngoma za kila aina?

 


Ni wazi kuwa Waislamu wanaofanya matendo haya mara tu baada ya kufuturu au mara tu baada ya kumaliza mwezi wa Ramadhani hawakupata matunda yatokanayo na swaumu na hawakufikia lengo lililokusudiwa. Labda tujiulize tena: Inakuwaje kwa Muislamu aliyefunga kwa nia safi, akose matunda yatokanayo na funga na ashindwe kufikia lengo la funga linalotazamiwa? Hii inatokea kwa sababu Waislamu wengi wafungao wana mapungufu yafuatayo:

 


(i) Lengo la Funga Halijulikani kwa Wengi

 


Lengo la kufunga kama lilivyobainishwa katika Qur-an ni kutufikisha katika ucha-Mungu katika maisha yetu yote. Uchaji Mungu hupatikana kwa kufuata kwa unyenyekevu maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kuacha kwa unyenyekevu vile vile makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kutarajia kupata Radhi Yake na kuepukana na ghadhabu zake. Wengi wa wafungaji hawafahamu lengo la funga. Wengi wanadhania wakishinda na njaa na kiu ndio watakuwa wamemaliza kufunga kana kwamba Mwenyezi Mungu (s.w) ametoa amri hii ya kufunga ili afurahie kuona waja wake wanavyohangaika kwa njaa na kiu! Mwenyezi Mungu (s.w) ameepukana na udhaifu huo. Yeye Mwenyezi Mungu (s.w) hahitaji lolote kutoka kwa waja wake bali ni waja wanaohitajia msaada kutoka kwake kama tunavyojifunza katika Qur-an:

 


“Sikuwaumba Majini na Watu ila wapate kuniabudu. Sitaki kwao riziki w ala sitaki wanilishe.Kw a yakini Mwenyezi Mungu ndiye Mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu madhubuti”. (51:56-58)

 


Kwa hiyo Waumini wa kweli wanaofunga hawana budi kufahamu vyema kuwa swaumu si kujiingiza kwenye mateso au si mgomo wa kula na kunywa ili kumfurahisha Mwenyezi Mungu (s.w) bali ni neema ya Mwenyezi Mungu (s.w) aliyotuletea ili ituwezeshe kuishi maisha ya utu yatakayotuletea furaha na amani ya kweli hapa ulimwenguni.

 


Wafungaji wengine wamelielewa lengo la funga kuwa ni kuwapatia thawabu tu, kiasi kwamba anaposhinda na njaa na kiu kuridhika kuwa ameshapata thawabu bila ya kujali kuwa swaumu imemfikisha au haijamfikisha kwenye uchaji Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hatuna budi kukumbuka kuwa thawabu au “ujira wa matendo mema” kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ni siri ya Mwenyezi Mungu (s.w). Hatuna namna yoyote ya kujua kuwa kitendo tulicho kifanya kimetupatia thawabu au la.

 


Tunaloweza kuhakikisha ni matunda tunayotarajiwa kuyapata kutokana na amali njema tulizoamrishwa kuzitenda. Kwa mfano tutakuwa na tumaini kuwa tumepata thawabu kutokana na funga zetu endapo, funga zetu zitatufikisha kwenye lengo la kumcha Mwenyezi Mungu (s.w) katika kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku. Lakini kama baada ya kufuturu usiku tutajihusisha tena na kumuasi Mwenyezi Mungu(s.w) au kama baada ya funga ya Ramadhani tutaendelea kufuata mwenendo wa maisha kinyume na ule anaoridhia Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake (s.a.w), tujue kuwa hatukupata chochote kutokana na funga zetu bali tumeambulia njaa na kiu.

 


(ii) Kutofahamika mahusiano baina ya funga na lengo la maisha

 


Kutofahamika kwa maana halisi ya Ibada kwa Waislamu wengi imekuwa ni kikwazo kikubwa cha kuzifanya ibada zetu kama vile kusimamisha swala, Zaka, Swaumu na Hija, zisitufikishe kwenye lengo lililokusudiwa. ‘Ibada’ ni neno la Kiarabu ambalo hutokana na neno ‘Abd’ lenye maana ya mtumwa. Kwa hiyo, katika Uislamu kufanya ibada ni kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w) kwa utii na unyenyekevu wa hali ya juu. Kutofahamika vyema maana halisi ya Ibada kumechangia sehemu kubwa ya kutofahamika lengo halisi la maisha ya mwanaadamu hapa ulimwenguni. Kama tunavyorejea katika Qur-an:

 


“Sikuwaumba majini na watu ila wapate Kuniabudu”. (51:56).
Kwa maana nyingine mwanaadamu anayetarajiwa aishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu (s.w) kwa unyenyekevu katika kuendesha kila kipengele cha maisha yake yote hapa ulimwenguni.

 


Lakini mwanaadamu ameumbwa na matashi ya kimwili na amepewa uhuru wa kuamua; anaweza kukidhi matashi yake kwa kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kuruka mipaka aliyomuwekea. Matashi haya na uhuru huu aliopewa mwanaadamu, humfanya mwanaadamu awe katika mtihani mkubwa katika maisha yake ya hapa ulimwenguni. Ama ayasalimishe matashi yake kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kumtii kwa unyenyekevu katika kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake, afaulu mtihani au ayafanye matashi yake mungu kwa kuyatii na kuyanyenyekea kinyume na kumtii na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu (s.w) afeli mtihani.

 


(iii) Miiko ya Funga haifuatwi vilivyo

 


Kila mfungaji hana budi kufahamu vyema masharti na nguzo za swaumu. Ibada yoyote haikamiliki mpaka itekelezwe kwa kufuata masharti na nguzo zote za Ibadah hiyo na pawe na kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) katika kipindi chote cha kuitekeleza. Wengi wa wafungaji hawatekelezi vilivyo miiko ya funga na kwahiyo funga zao zimeshindwa kuwapatia matunda yanayotarajiwa. Hatuna budi kufahamu kuwa Miiko ya Kufunga haiishii kwenye kujizuilia kula, kunywa na kujamii tu bali ni pamoja na kujizuilia na maovu yote aliyoyakemea Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake. Rejea Hadithi ifuatayo:

 


Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Yule ambaye hataacha lugha mbaya na matendo mabaya, Mwenyezi Mungu (s.w) hana haja ya kuona kule kuacha kwake chakula na kinywaji chake (Mw enyezi Mungu (s.w) hakubali funga yake)” (Bukhari).

 


Ni wangapi wanaofunga huku wanasengenya wengine, wanasema uwongo, wanafitinisha na kugombanisha watu na huku futari yao na daku inapatikana kwa njia za haramu? Ni wangapi wanaofunga ambao hufanya maovu mengine kuliko haya? Ni wazi kwamba funga zao haziwapatii faida yoyote mbali na kushinda njaa na kiu.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 791


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kujitwaharisha najisi kubwa najisi ya mbwa na Nguriwe
Soma Zaidi...

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Sifa za kuwa maamuma kwenye swala na namna ya kumfuata imamu
Post hii inakwenda kukuelezea sifa za kuwa maamuma na taratibu za kumfuata imamu. Soma Zaidi...

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Soma Zaidi...

Swala ya Istikhara na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara Soma Zaidi...

Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutwaharisha Aina mbalimbali za Najisi katika uislamu
Katika somo hili utakwedna kujifunza jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi kwa mujibu wa mafundiso ya Mtume Muhammad (s.a.w) Soma Zaidi...

Aina za twahara na aina za najisi
Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh Soma Zaidi...

haya ndiyo mambo yanayaribu swala na yanayobatilisha swala
Soma Zaidi...

Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Soma Zaidi...

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga
Soma Zaidi...

Nguzo za udhu ni sita
Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu. Soma Zaidi...