Jifunze jinsi ya kumsaidia mwenye kifafa
Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid
Dalili za kifafa
Kifafa kina dalili ambazo huonekana na mtu ukiziangalia unajua kuwa Ni mojawapo ya kifafa na dalili hizo Ni pamoja na;
1.mwenye kifafa lazima ataonyesha dalili ya kupoteza fahamu ; yaani hawezi kusikia,hawezi kuona, hawezi kusikia maumivu kwa huo muda yaani hatakuwa na ushirikiano wowote ule (unresponsive).
2.lazima atupe au kurusha rusha mikono na miguu,pamoja na kichwa kukigeuza geuza na huo muda mauvu anakuwa hasikii kabisa.
3.kuchanganyikiwa kwa mda
4.mate yenye mchanganyiko wa mapovu kutoka Mdomoni kwa huo muda aliopata kifafa( udenda)
5. Mwenye dalili za kifafa huwa anaduwaa kipindi kifafa kinamtokea.
Sababu za kifafa
1.kurithi; kifafa huweza Kurithi kutoka kizazi hadi kizazi.
2.magonjwa ya kuambukiza Kama vile ukimwi,au uti wa mgongo huweza kusababisha kifafa.
3.madhara kwenye ubongo; Kama vile maji kujaa kwenye ubongo, uvimbe kwenye ubongo, bacteria na virusi vinavyoshambilia ubongo husababisha kifafa pia.
4. Kichwa kuumia (head injury) mfano ukipata ajali ya kichwa pia husababisha kifafa.
Huduma ya kwanza kwa mwenye kifafa
Kifafa huweza kutibiwa nyumbani na kupona Kama hakijawa sugu au ikiwa Ni kifafa kilichopo na huwa mnamfanyia huduma ya kwanza anapona , namna ya kumpatia huduma ya kwanza kwa mwenye kifafa;
1.hakikisha sehemu aliyoangukia Ni Safi na Haina vitu vya kumuumiza ili anapopata fahamu asiwe na maumivu ya kuchomwa na kitu .
2.mgeuze mgonjwa alale upande (kiubavu) ili akicheua,akimeza mate au kutapika asipate shida maana yanaweza kurudi kwenye Koo la hewa na kumsababishia shida nyingine au yanaweza kumkaba.
3.mwekee kitu kilaini kwenye kichwa ili awe vizuri (comfortable).
4.mkague Kama amevaa hereni,cheni,au kitu kinachoweza kumuumiza umtoe .
5.mwache mgonjwa apate hewa watu wasimzunguke maana anaweza akakosa hewa.
6.usimzuie mgonjwa kurusha miguu na mikono hauruhusiwi kumshika mwache arushe akipata fahamu ataacha.
7. Usimpatie au kuweka chochote Mdomoni mwake Mana anawaze kutapika, kukabwa, au kurudi kwenye Koo la hewa na kupaliwa.
8.kaa na mgonjwa mapaka atakaporudi katika Hali yake na umuangalie yupo katika Hali gani Kama Ni mzuri au mbaya.
9kama mgonjwa Yuko katika Hali mbaya Sana au amechuku muda mrefu zaidj ya lisaa limoja haja pata fahamu fanya mipango sasa ya kumpeleka hospitali kwaajili ya matibabu .
Mwisho; Kama mgonjwa wa kifafa ndio Mara yake ya kwanza au ameanguka akachukua mda mrefu na Kama ana Hali ya kifafa na hajawahi kwenda hospitalini kwaajili ya uchunguzi Ni vyema kumpeleka akafanyiwe uchunguzi na vipimi na ushauri zaidi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 ai web app 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Mkojo mchafu na Rangi za mikojo na maana zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Rangi za mkojo na maana zake na mkojo mchafu
Soma Zaidi...Mambo yanayoweza kudhoofisha kinga ya mwili
Kinga ya mwili inapodhoofu mwili unakuwa hatarini kupata maradhi. Je unayajuwa mambo yanayodhoofisha kinga ysbmeili?
Soma Zaidi...Zijue kazi za uke (vagina)
Uke ni sehemu ambayo imo ndani ya mwili wa mwanamke, sehemu hii ufanya kazi mbalimbali hasa wakati wa kujamiiana, kubarehe na kujifungua kwa mama.
Soma Zaidi...Namna ya kutunza nywele za mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi.
Soma Zaidi...Zijue faida za maji ya uvuguvugu.
Posti hii inahusu zaidi faida za maji ya uvuguvugu, hasa hasa maji haya ni vizuri kabisa kuyatumia hasa wakati wa asubuhi na pia wakati tumbo likiwa halina kitu, kwa hiyo zifuatazo ni faida za maji ya uvuguvugu.
Soma Zaidi...