JINSI AMBAVYO MGONJWA ANATAKIWA ASWALI


image


Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake.


Swala tano za Faradh katika Nyakati za Dharura

Amri ya kusimamisha swala tano imeambatana na nyakati makhususi kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

 

“Basi simamisheni swala Kwa hakika swala kwa waislamu ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi” (4:103)
Hivyo swala ya mja haitakubaliwa iwapo ataiswali nje ya wakati wake makhsusi. Hapana “kadha” katika swala.

 


Pamoja na amri ya kuiswali kila swala ya faradhi katika wakati wake makhsusi, Allah (s.w) aliye Mwingi wa Rehma haikalifishi nafsi yoyote katika kuipa amri zake ila huitaraji kila nafsi itekeleze amri hizo kwa kadiri ya uwezo aliyoijaalia kuwa nao. Mara kwa mara katika kutufahamisha huruma zake juu yetu, Allah(s.w.) anakariri:

 


“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila yaliyosawa na uwezo wake...” (2:286)
Baada ya kutoa ruhusa ya kutofunga wagonjwa na wasafiri, wakati wa mwezi wa Ramadhani na badala yake walipe “kadha” siku walizokula anatudhihirishia Rehma zake kwa kutufahamisha:

 

“... Mw enyezi Mungu anakutakieni yaliyo m epesi, w ala hakutakieni yaliyo mazito...” (2:185)
Pia baada ya kutoa ruhusa ya kutayammam, baada ya kukosa maji, au kwa ajili ya maradhi au mtu anapokuwa safarini, katika Sura ya 5 aya ya 6, Allah (s.w) anamalizia kwa kusema:-

 

“... Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)

 

 

 

“.. .Na ka m a m kiw a w agonjw a (mm eka tazw a ku tumia m aji) a u mm o safarini au mmoja wenu ametoka msalani (chooni) au mmewagusa(mmewajamii), wanawake - na msip ate maji basi ukusudieni (tayamamuni) udongo safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mwenye kusamehe (na) Mw enye kughufiria ”. (4:43)

 


“... Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi kusudieni (tayammamuni) udongo ulio safi na kuupaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)

 


(2) Iwapo mgonjwa hajimudu na hana wa kumtwaharisha kwa maji au kwa udongo itabidi atayammamu kifikra na kuswali hivyo hivyo. Hili ni sahali kwa kauli ya Allah (s.w):

 

“Hapendi Allah kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu”. (5:6)

 


(3)Mgonjwa anaruhusiwa kuswali akiwa amekaa na kuelekea Qibla iwapo ana uwezo huo, vinginevyo ataelekea popote pale kwa kadiri ya uwezo wake. Atarukuu na kusujudu katika hali hiyo ya kukaa iwapo anaweza, vinginevyo atarukuu na kusujudu kwa ishara tu.
(4)Iwapo mgonjwa hawezi hata kukaa ataswali akiwa amelala kwa ubavu huku akiwa ameelekea Qibla kama ana uwezo wa kufanya hivyo, vinginevyo ataelekea popote pale. Pia kama hawezi kulala kwa ubavu atalala chali. Kama hawezi kulala chali ataswali kwa ishara akiwa amelala vyovyote vile awezavyo.

 

(5) Pia mgonjwa anaruhusiwa kuchanganya swala kama msafiri (rejea swala ya msafiri) kama hivyo ndivyo hali ya mazingira ya ugonjwa inavyotaka.
Kutokana na tahfifu hizi, ugonjwa si udhuru wa kumruhusu mtu asiswali swala ya faradh kwa wakati wake hata kama mgonjwa huyo atakuwa mahututi kitandani akiwa nyumbani au hospitalini maadamu bado ana akili timamu.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Je ni zipi nguzo za uislamu, na ni ngapi nguzo za uislamu?
Post hii itakujuza maana ya uislamu na nguzo zake. Soma Zaidi...

image Umuhimu wa uchumi katika uislamu
Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu. Soma Zaidi...

image Utaratibu wa kuzuru makaburi na dua zinazosomwa wakati wa kuzuru kaburi
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika katika kuzuru kaburi la muislamu. Soma Zaidi...

image Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke katika jamii
Unadhani mwanamke kupewa mahari kitendo hiki kinaweza kushusha hadhi yake? Soma Zaidi...

image Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kukaa itiqaf na taratibu zake
Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kumuandaa maiti baada ya kufa
Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki. Soma Zaidi...

image Watu wanaolazimika kufunga mwezi wa Ramadhani
Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani. Soma Zaidi...

image Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa
Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii. Soma Zaidi...

image Vipi utapata uchamungu kupitia funga
Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu. Soma Zaidi...