Jinsi mimba inavyotungwa na namna ambavyo jinsia ya mtoto inavyotokea

Posti hii hasa inahusu kasoro ,utatuzi,na jinsi ya kutunga mimba kwa upande wa mwanamke na mwanaume' .itatupelekea jinsi ya kuangalia kasoro na jinsi ya kutatua hizo kasoro katika jamii zetu.

KASORO KATIKA MFUMO WA UZAZI KWA MWANAUME 

1.kutokana na hapo awali tunaongelea kuhusu kutatua kasoro katika mfumo wa uzazi kwa upende wa mwanaume na mwanamke kasoro zipo nyingi .ila tuanze na kasoro kwa upende wa mwanaume ambapo  wanaume wengi upatwa na kasoro kadhaa katika mfumo wao moja ya kasoro ambayo uweza kuwapata wanaume ni ugumba .hii ni hali ya mwanaume kushindwa kutungisha mimba .

 

Ugumba kwa mwanaume hisababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kutoa mbegu ambazo zinakuwa chache sana hivo inapelekea kupunguza uwezekano kulifikia yai la mwanamke .kasoro nyingine ni kuwa na mbegu dhaifu ambazo zina upungufu kwa mfano kukosa mikia ,kuwa na mikia miwili ,kukosa kichwa au kuwa na umbo lisilo la kawaida yaani tunasema mbegu inakuwa haina umbo mahalamu kama mbegu zingine

 

Pia inapelekea kinga ya mwili inaweza kushambulia mbegu za kiume na hivyo kupunguza idadi yake vilevile kasoro nyingine korodani ya mwanaume hazitakuwa na uwezo wa kutengeneza mbegu za kiume kutokana na magonjwa au upungufu wa homoni .kasoro nyingine ya ugumba ni mirija ya kupitisha mbegu za kiume kuziba kutokana na magonjwa ya ngono kama ,vile kaswende na kisonono kwahiyo inashauriwa tusifanye ngono zembe bila kinga itatupelekea kupata matatizo ya ugumba  .na kama utaona hizo kasoro ina bidi kufika kituo cha hospitali kabla ya tatizo kuwa kubwa.tumeweza kuona hio kasoro kwa upende wa mwanaume.

 

2. Kutokana na kasoro hizo hii ni kasoro katika upande wa uzazi wa mwanamke  kama ilivyokuwa kwa mwanaume pia na mwanamke ana kasoro zake katika mfumo wake wa uzazi mojawapo ya kasoro ni ugumba kwa upande wake na tumeona mwanaume ana ugumba pia na mwanamke anaweza kuwa na ugumba unasababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo mayai yake kushindwa kufanya kazi au kupevuka pia hali hii utokana matatizo ya utoaji wa homoni.

 

Matatizo hayo yanaweza kusababisha na tezi ya pituitari kushindwa kutoa homoni .vilevile,ovari kushindwa kutoa homoni ya oestrojeni au projesteroni ya kutosha .Adha ,ugumba unaweza kusababishwa na kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai kutokana na magonjwa ya ngono kama vile kisonono,kaswende na pangusa .

 

Magonjwa haya yanaweza kufanya mirija iwe myembamba au iwe na makovu hivyo kuzuia yai lisiweze kupita .vilevile ugumba kwa wamama  unaweza kusababiswa na uvimbe kwenye mji wa mimba ambapo hisababisha kiinitete kisiweze kujishikiza vizuri na hivyo usababisha matatizo ya mimba kutoka na hii shida ipo sana kwa wanawake kutokwa na mimba .

 

 Utatuzi wa kasoro katika mfumo wa uzazi.

Kutokana na hayo matatizo au kasoro za mfumo wa uzazi kwa mwanaume na mwanamke matatizo hayo yote yanatibika kama mtu atawahi kwenda kituo cha afya kupata matibabu na ushauri nasaha kwa madaktari pia na kumsikiliza na kwenda kuyafanyia kazi.

 

  JINSI YA  KUTUNGA MIMBA.                       1. Mwanaume na mwanamke wana huwezo wa kutunga mimba pale gameti za kike na za kiume kuungana au wengine wanasema ,zaigoti, wakati wa kujamiana mwanaume hutoa manii zenye gameti ume kutoka kwenye korodani kupitia mirija ya manii , urethra hadi uume .manii zenye gameti gameti ume huingia katika mwili wa mwanamke kupitia sehemu ya uke.mwanamke hutoa gameti uke kutoka kwenye ovari na kushuka kupitia mirija ya falopio.kama kama gameti ume zikiungana na gameti uke mimba utungwa .apo ndo jinsi mimba inatungwa kwa mwanaume na mwanamke  pia apo apo tunaweza kupata watoto

 

 Kuna njia za kupata au kutunga mimba ya pacha

1.hiii kwa jamii zingine zinaeleza kwamba ukipata pacha wawili nyie mnakuwa mna mikosi au mmeraniwa na mwenyezi mungu ambacho kitu sio cha ukweli kwahio inabidi jamii itambuwe kwamba watoto mapacha sio mikosi bali watoto mapacha wanapatikana pale.mwanamke anapojifungua mtoto mmoja kwa kila ujauzito .

 

Hata hivyo.mara chache mwanamke anaweza kujifungua wawili au zaidi kwa mpigo mmoja tu .mwanamke akijifungua watoto wawili au zaidi kwa ujauzito mmoja ,watoto hao huitwa pacha a aa. Pacha hao wanaweza kufanana au kutofanana.

 

Tuangalie kidogo apa jinsi ya mtoto kutokwa.Gameti uke kutoka kwenye ovari imebeba chembeuzi ya aina mmoja inayoitwa x hivyo,kila yai linalotoka tayari kwa kurutubishwa hubeba chembeuzi X.Gameti imebeba moja Kati ya chembeuzi za aina mbili yaani au Y endapo chembeuzi X kutoka kwa mwanaume itakutana na chembe X  kutoka kwa mwanamke.mtoto wa kike hutungwa .

 

Kama chembeucheuzi Y kutoka kwa mwanaume itakutana na chembe X kutoka kwa mwanamke .mtoto wa kiume hutungwa .hivyo basi anayehusika na upatikanaji wa jinsi ya mtoto ni mzazi wa kiume.

 

 



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/03/Wednesday - 11:40:09 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1511


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-