Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla.
4. Kuelekea Qibla
Kuelekea Qibla ni sharti la nne la kusimamisha swala. Katika hali ya kawaida Muumini ni lazima aelekee “Qibla wakati akiswali.Qibla ni neno la Kiarabu linatokana na neno “Qabala” lenye maana ya kuelekea sehemu au upande ambao watu huelekeza nyuso zao. Kwa mtazamo wa Qur-an, Qibla ni sehemu wanapoelekea waislamu wakati wa kuswali. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Qibla ni sehemu ya katikati inayowaunganisha waumini kuwa mwili mmoja (kitu kimoja).
“Na po pote wendako geuza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu . Na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako. Na Mw enyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda. (2:149)
Ummati wa Muhammad (s.a.w) Qibla chake ni Ka’aba, nyumba tukufu ya Allah iliyoko mjini Makkah, Saudi Arabia. Waislamu wote ulimwenguni huielekea Ka’aba wakati wa kuswali. Swala yoyote itakayoswaliwa bila ya kuelekea upande ilipo Ka’aba, pasipo na dharura inayokubalika kisheria kama vile kuwa mgonjwa, au kuwa safarini, ha is wih i.
Namna ya Kutafuta Qibla
Kukisia ulipo mji wa Makka, Saudi Arabia, ambao ndani yake iko Ka’aba ni jambo rahisi kwa kutumia utaalamu wa Jiografia. Chombo
kizuri cha kumuwezesha mtu kukisia ilipo Ka’aba ni ramani ya dunia. Utakapojua ulipo katika sehemu yoyote ya dunia utaweza kujua Ka’aba iko upande gani wa dira kutokea pale ulipo kwa kutumia jua au chombo cha dira (Magnetic Compass). Kwa mfano ukiwa Tanzania, utaelekea Kaskazini kamili, ukiwa Pwani kama vile Dar es Salaam na ukiwa bara kama vile Kigoma, utaelekea Kaskazini ya Kaskazini Mashariki.
Kabla ya Muislamu hajaanza kuswali, hasa anapokuwa mgeni wa mahali hana budi kufanya jitihada ya kutafuta Qibla kwanza. Ni vyema mtu asafiripo awe na dira (Magnetic Compass) na ramani ili vifaa hivi vimsaidie kutafuta Qibla, vinginevyo itabidi awaulize wenyeji wa sehemu h iyo.
Mtu akishindwa kabisa kukibaini Qibla baada ya kujitahidi mwisho wa jitihada zake, popote atakapoelekea patafaa, kwani hii sasa imekuwa ni dharura, huku tukizingatia kuwa “Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu”.
Na Mashariki na Magharibi ni ya Mw enyezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mw enyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na Mwenye kujua (kukubwa kabisa vile vile). (2:115)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 ai web app 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 web hosting 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Zaka ni nini? Nini maana ya zaka katika uislamu
Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri.
Soma Zaidi...sunnah za swala
Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Soma Zaidi...Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga.
Soma Zaidi...Kusimamisha swala.
Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala.
Soma Zaidi...