Jinsi ya kufanya suluhu kati ya mume na mke.

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa.

Suluhu Kati ya Mume na Mke

Wanaadamu wanapoishi pamoja, kutokana na udhaifu wa kibinaadamu kukwaana na kugombana ni jambo Ia kawaida. Hivyo mume na mke ambao wako karibu sana, hawana budi kuvumiliana kwa kiasi kikubwa. Mmoja akimwona mwenzie amekasirika hana budi kutulizana na kujifanya kama mjinga. Kila mmoja hana budi kujitahidi kwa jitihada zake zote kumtendea wema mwenzake na kumpa haki zake.

 

Vile vile kila mmoja hana budi kuwa tayari kusamehe haki ndogo ndogo alizonyimwa na mwenziwe. Mwenendo huu wa kuvumiliana na kusameheana hudumisha amani na upendo katika nyumba. Hatuna budi kukumbuka kuwa kuvumiliana na kusameheana, hakuleti tu furaha na amani katika nyumba na katika jamii kwa ujumla bali pia ni matendo ya kiucha-Mungu yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:

 


"... Na wasamehe na waachilie mbali (yaliyopita). Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwingi wa rehema (basi nanyi sWkeni na sfa hizi) ". (24:22).

 

Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na ubaya huo; lakini anayesamehe na kusuluhisha ugomvi, ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu; bila shaka yeye hawapendi madhalimu.. (42:40)

 


Aya hizi zinatufahamisha kuwa kusamehe ni sababu ya mtu kusamehewa makosa yake na Mola wake na pia ni sababu ya kupata malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w). Hivyo ikitokea mume na mke wakahitilafiana na kugombana, hawana budi kujisuluhisha wenyewe kwa njia hii ya kusubiri na kusameheana kama Mwenyezi Mungu (s.w) anavyotushauri katika Qur-an:

 

Na kama mke akiona kwa mume wake kugombana gombana na kutengana tengana, basi si vibaya kwao wakitengeneza baina yao suluhu (njema wakastahimiliana bila kuachana) maana suihu ni kitu bora. Na nafsi zimewekewa ubakhili mbele (hakuna mtu anayetaka kumuachia mwingine haki yake). Na kama mkifanya mema (kuwafanyia wake zenu) na mkimcha Mwenyezi Mungu (msiwapunguzie haki zao, bila shaka Mwenyezi Mungu atakulipeni) kwani Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. (4:128).

 

Ikitokea mume na mke wenyewe wameshindwa kujisuluhisha mpaka ugomvi ukajitokeza nje, Waislamu walio karibu nao kwa urafiki, ujirani, udugu, n.k. waingilie kati na kuwapatanisha ndugu zao kabla sumu ya shetani haijaenea katika nyumba. Msuluhishaji atumie busara kubwa na ajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake katika kufanya kazi hiyo akijua kuwa hiyo ni kazi nyeti na yenye malipo makubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyosoma katika Qur-an:

 

Hakuna kheri katika mengi wanayoshauriana kwa sin. Ispokuwa (mashauri ya) wale wanaoamnisha kutoa sadaqa au kufanya mema au kupatanisha baina ya watu. Na atakayefanya hivi kwa kutaka nadhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujina mkubwa. (4:114).

 


Msuluhishi huyu akishindwa, kabla mume hajakimbilia kutoa talaka au mke hajakimbilia kudai talaka, ni vyema Waislamu hawa wakashitakie ugomvi wao kwa kadhi. Kadhi atajitahidi kuwapa mawaidha mazuri na kumkumbusha kila mmoja haki zake na wajibu wake kwa mwingine, kisha baada ya kumsikiliza kila mmoja wao kuhusiana na ugomvi wao, hatatoa uamuzi pale pale bali ataomba muda wa kupekua zaidi kesi hiyo. Kadhi atachagua ndugu waadilifu kutoka kila upande watakaomsaidia kupeleleza kiini cha ugomvi na ni nani aliye mkosea mwenziwe.

 


Kisha Kadhi atamuita mume na mke na kuwapatanisha akisaidiana na jamaa wa kwa mume na mke. Kadhi atamsihi mkosa asirejee tena makosa yake na amtake mwenziwe msamaha na vile vile aombe msamaha kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Pia aliyekosewa ataombwa amsamehe mwenzake ili naye Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na kupata ujira mkubwa kutoka kwake. Wawili hawa wakiwa na nia ya kupatana, baada ya hatua hizi, Mwenyezi Mungu (s.w) ameahidi kuwapatanisha kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

 


Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basipelekeni mwamuzi mmoja katikajamaa za mwanamume na mmoja katika jamaa za mwanamke.Kama wakitaka map atano Mwenyezi Mungu atawapatanisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa habari za sin na habani za dhahini. (4:35).

 


Ni nani mbora wa kutekeleza ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Hivyo, mume na mke wasikimbilie talaka bali wajitahidi kutafuta suluhu baina yao kwa nia njema na kwa jitihada zao zote. Ndipo waachane endapo suluhu itashindikana kabisa. Na kutokana na ahadi hii, haitashindikana endapo watakuwa wacha Mungu.
Pia kabla ya kufikia hatua ya talaka, mume na mke wanaruhusiwa kutengana kwa muda wa miezi mine. Suluhu ikishindikana katika muda huo itabidi waachane kama tunavyojifunza katika Qur-an:

 

Kwa wale wanaoapa kwamba watajitenga na wake zao, (muda wao) ni kungojewa miezi mine. Na kama wakinejea, basi Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kunehemu.Na wakiazimia kuacha (basi) Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, mwenye kujua. (2:226-22 7)

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/19/Friday - 02:35:07 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 964


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Ni nini maana ya Talaka katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha. Soma Zaidi...

Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa
Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii. Soma Zaidi...

Je ni nani mwenye haki ya kutaliki
Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye. Soma Zaidi...

Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili
Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake. Soma Zaidi...

Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi? Soma Zaidi...

Taratibu za kutaliki katika uislamu.
Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke. Soma Zaidi...

Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume. Soma Zaidi...

Zijuwe aina kuu 6 za talaka katika uislamu
Talaka zimegawanyika katika makundi mengi. Katika somo hili utakwenda kukifunza aina kuu za talaka katika uislamu. Soma Zaidi...

Aina mbili za talaka zisizo na rejea katika uislamu
Huwezi kuruhusiwa kumrejea mke endapo utamuacha kwa talaka hizi mbili. Soma Zaidi...

Ni upibutaratibu wa kuingia eda na kutoka eda
Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi Soma Zaidi...

Jinsi ya kufanya suluhu kati ya mume na mke.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa. Soma Zaidi...