Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali.

Masharti ya Swala ya Maiti

Masharti ya swala ya maiti ni yale yale ya swala ya kawaida kwa wenye kumswalia maiti bali kwa maiti mwenyewe kuna masharti yafu atayo:
(i) Maiti awe Muislamu kwani Allah (s.w) amesema:“Wala usimswalie abadan mmoja wao (makafiri na wanafiki) yeyote akifa”. (9:84)
(ii)Maiti awe ameshaoshwa.
(iii)Maiti awekwe mbele ya wanaomswalia. Lakini pia inajuzu kumswalia maiti ambaye hayupo,swala ya ghaibu. Maiti zikiwa nyingi zitapangwa mbele za kiume zikiwa karibu na Imamu, kisha zitaswaliwa swala moja tu.
(iv)Maiti asiwe shahidi.Kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (s.a.w) watu waliokufa katika vita vya kupigania dini ya Allah (s.w) hawaoshwi wala kuswaliwa.Mtume (s.a.w) aliamuru Mashahidi katika vita vya Uhud wasioshwe wala wasiswaliwe. (Abu Daud).

 

Nguzo za Swala ya Maiti

 


Nguzo za swala ya maiti ni tofauti kidogo na zile za swala ya kawaida. Tofauti na swala ya kawaida, swala ya maiti ina kusimama tu, hakuna rukuu, sijda wala vikao. Nguzo za swala ya maiti ni hizi zifuatazo:
1. Nia.

 

2. Takbira ya kuhirimia
(Takbira ya kwanza) anavyoswaliwa katika swala ya
kawaida
3. Kusoma suratul fatiha

 

4. Kuleta takbira ya pili

 

5. Kumswalia Mtume(s.a.w) kama

 


6. Kuleta takbira ya tatu.
7. Kumuombea dua maiti
Kuleta takbira ya nne
8. Kutoa salaamu

 

Sunnah za Swala ya Maiti

 


Nguzo za swala ya maiti ni hizi zifuatazo:

 


1.Kusoma Audhubillah kabla ya Al-fatiha.
2.Kusema Amin baada ya Al-fatiha.
3.Kuyasema yote yanayosemwa katika swala hii kimya kimya, ila Imamu atatoa Takbira Nne naSalam kwa sauti. Iswaliwe jamaa na safu ziwe witri; 1, 3, 5, 7, 9, n.k 4.Kuwaombea Waislamu wote dua pamoja na maiti. Baada ya Takbira ya Nne na kabla ya Salaam kuomba dua ifu atayo:

 


“ Alahumma laatahrimn aa ajrahu, walaataftinaa ba’adahu”
“Ewe Mwenyezi Mungu, usitunyime malipo yake na usitujaribu baada yake.”
5.Kutoa Salaam ya kwanza na ya pili kwa ukamilifu wake.
6.Imamu kusimama karibu na kichwa cha maiti ya kiume na kusisima karibu na kiuno (nyonga) ya maiti ya kike.

 


Namna ya Kutekeleza Swala ya Maiti

 


Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo:
1. Maiti iwekwe mbele.
2. Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti kama maiti ni ya kike na asimame sawa na mabega kama maiti ni ya kiume.Iwapo maiti zinazoswaliwa ni zaidi ya mmoja zipangwe moja mbele ya nyingine .Maiti za kiume zikiwa karibu na Imamu.

 

3.Wanaomfuata Imamu wasimame kwenye mistari yenye idadi ya witri; 1, 3, 5, 7, n.k.
4.Baada ya kusimama hivyo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
(i)Nia - nia ya kumswalia maiti iliyo mbele huwekwa moyoni (si lazima kutamka).
(ii)Kisha nia hii huambatanishwa na Takbira ya kwanza - Takbira ya kawaida ya kuanzia swala - nayo ni kusema: Allahu Akbar.
(iii)Imamu na Maamuma watasoma Suratul Fatiha kimya kimya.
(iv)Baada ya kuimaliza Suratul- Fatiha Imamu atasema tena Allahu Akbar na Maamuma watafuatisha hivyo hivyo - bila ya kuinua mikono.
(v)Imamu na Maamuma watamswalia Mtume (s.a.w) kimya kimya kama ilivyo katika tahiyyatu ya mwisho ya swala ya kawaida.
(vi)Baada ya kumswalia Mtume, Imamu atasema tena - Allahu Akbar na Maamuma watafuatisha hivyo hivyo kimya kimya bila ya kuinua mikono.
(vii)Kisha kimya kimya maiti huombewa dua yoyote ile katika zile alizotufundisha Mtume (s.a.w). Moja kati ya dua hizo ni hii iliyosimuliwa na Abu Hurairah na kupokelewa na Maimamu wa hadith - Ahmad, Abu Daud, Timidh na Ibn Majah.

 


(viii) Baada ya dua hii imamu atasema tela Allahu Akbar na maamuma watafanya vivyo hivyo bila ya kunyanyua mikono.

 

(ix) Waombewe dua waislamu wote dua ifuatayo inaweza kutumika:

 


"Rabbana ighfir lanaa wali-ikhwaaninal-lladhiina sabaquuna bil-iiman, walaa taj-'al fii quluubinaa ghilal-Lilladhiina aamanuu, Rabbanaa in-naka ra-ufur-rahiim"

 

“... Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia (kufa) katika Imani (ya Kiislamu). Wala usijaalie katika nyoyo zetu uadui kuw afanyia Wa is lamu wenzetu. Mola wetu! Hakika wewe ni Mpole sana, mwenye Rehma mno”. (59:10)
(x) Baada ya dua hii itatolewa Salaam ya kumaliza swala na ni bora kuirefusha kidogo kuliko ile ya swala ya kawaida kwa kusema: "As-salaamu 'alaykum warahmatulllahi wabarakaatuh.

 

Amani iwe juu yenu na Rehma za Allah na Baraka zake.

 


Swala ya maiti pia inaweza kuswaliwa kwa ghaib, yaani bila ya kuwa na jeneza mbele. Mtume (s.a.w) mara kadhaa katika maisha yake, aliongoza swala ya maiti wa mbali na karibu waliokwisha zikwa kama tunavyofahamishwa katika Hadith zifu atazo:

 


Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuw a Mtume wa Allah (s.a.w) alitoa habari za kifo cha Najashi (Mfalme wa Uhabeshi) kwa watu katika siku aliyokufa, akaenda nao katika sehemu ya kuswalia, akafanya mistari pamoja nao kisha akapiga takbira nne (yaani akaongoza swala ya Jeneza). (Bukhari na Muslim).

 


Ibn Abbas (r.a)amesimulia kuw a Mtume wa Allah alipita karibu na kaburi alimozikwa maiti usiku uliopita. Akauliza: Ni wakati gani alizikwa? Walijibu: Usiku uliopita. Akauliza: Kwa nini hamkunifahamisha? Walijibu: Tulizika katika giza la usiku. Kwa hiyo hatukupenda kukuamsha usingizini. Kisha alisimama na tukaunda mistari nyuma yake akaiswalia maiti ile. (Bukhari na Muslim).

 


Kusindikiza Jeneza
Baada ya maiti kuswaliwa jeneza litaongozwa kuelekea kaburini. Inatakiwa Waislamu walisindikize jeneza; wasiliweke mpaka likalishwe chini. Pia Mtume (s.a.w) ametuamrisha kusimama tutakapoona jeneza likipitishwa:

 


Jabir (r.a) amesimulia: Wakati Jeneza lilipokuwa linapita, Mtume (s.a.w) alisimama nasi pia tukasimama pamoja naye. Tukauliza: Ewe Mtume wa Allah! Hakika huyo ni Myahudi. Akasema: “Hakika kifo ni tishio. Kw a hiyo w akati wote mtakapoona Jeneza likipita simameni”.(Bukhari

 

Maandamano ya mazishi yawe kimya kimya.Kumsindikiza maiti kwa muziki na vilio ni haramu.


 


‹ Nyuma      › Endelea           Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/15/Monday - 09:23:27 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1358


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Al-Arba-uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 5: kujiepusha na uzushi katika dini
Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini Soma Zaidi...

Swala ya ijumaa, nguzo zake, sharti zake na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali. Soma Zaidi...

Zijuwe sunnha 9 za swala
Post hii inakwenda kukufundisha sunnah 9 za swala. Sunnah hizi ni zile ambazo ukiziwacha swala yako haibatiliki. Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swwla ya dhuha na faida zake
Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swala ya haja
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Swala ya kuomba mvua swalat istiqaa na jinsi ya kuiswali.
Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala. Soma Zaidi...

Faida za kuswali swala za sunnah
Posti hii inakwenda kukufundisha kuhush swala za sunnah. Soma Zaidi...

Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...