Kazi ya Dawa ya salbutamol

Kazi ya Dawa ya salbutamol

Posti hii inahusu dawa ya salbutamol na kazi yake ya kutibu ugonjwa wa Asthma, ni dawa mojawapo ambayo imetumia na watu wengi na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo zifuatazo ni kazi ya Dawa hii ya salbutamol katika kutibu Asthma.

Kazi za Dawa ya sulbutamol.

1. Sulbutamol ni dawa ambayo usaida katika kutibu Asthma na matatizo yote yanayohusiana na mfumo wa hewa, ufanya kazi yake kwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya kubanwa kifua na Asthma, ufanya kazi hiyo kwa kuifanya mishipa au misuli ya kwenye mfumo wa hewa kulainika na kufanya hewa kupita kwa urahisi, tukumbuke kwamba kama mgonjwa amebakwa na kifua misuli ya kwenye kifua mara nyingi huwa imebana na kumfanya mgonjwa kuumia na kupumua kwa shida kwa hiyo kwa kutumia sulbutamol misuli ya mgonjwa ulainika naye upumua kawaida.

 

2. Pia hii dawa uwezo kuwa kwenye mifumo mbalimbali , inaweza kuwa kwenye hali ya vidonge, au kwenye mfumo wa maji ambayo utumiwa sana na watoto, na pengine inaweza kutumiwa kwa kumpulizia mgonjwa kama anaumwa kupitia mdomoni au kwa maelezo zaidi wataalamu wa afya ndio wanaweza kukupatia utaratibu kadri ya hali halisi ya mgonjwa.

 

3. Dawa hii uweza kutumiwa ila si kwa watu wote hasa wale walio na Mzio au akeji na dawa hii hawapaswi kuitumia na mtu akitumia dawa hii hapaswi kutumia dawa yoyote ya maumivu hasa hasa Asprin. Na pia dawa hii inapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa watu wenye matatizo ya moyo na  presha kwa sababu dawa inaweza kupandisha presha juu na mapigo ya moyo yanaweza kwenda kwa mbio, kwa hiyo kabla ya kutumia dawa hii mgonjwa anapaswa kupima presha kwanza na mapigo ya moyo ili tusije kuleta matatizo mengine zaidi.

 

4.Tunapotumia dawa hii tunategemea kupata maudhi madogo madogo kama vile mapigo ya moyo kwenda kwa mbio, maumivu ya kichwa, kupata usingizi kwa shida na pengine presha kubwa juu hii ni kwa sababu ya mishipa ya damu ambayo imeingiliwa na dawa usababisha mishipa ya damu kupitisha damu kwa haraka zaidi, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wakiona hayo yote wasishangae ni sehemu ya kawaida ya matokeo ya dawa.

 

5 . Kwa upande wa watoto wadogo wanapaswa kupewa 0.1mg kila baada ya maasaa manne na kwa watu wazima wafuate utaratibu wa daktari  na kwa wanawake wenye mimba inabidi wapewe kwa njia ya kuvuta tu kwa sababu njia nyingine zinapelekea kuwepo kwa matatizo ya moyo hasa kwa akina mama. Kwa hiyo dawa hii ni ya muhimu sana na imewasaidia watu wengi na tusitumie kiholela Bali tusikilize ushauri wa daktari na wataalamu wengine wa afya.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views: 9474

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Dawa ya kutibu fangasi wa kwenye mdomo na kinywa

Zipo dawa nyingi ambazo hufahamika katika kutibu fangasi kwenye mdomo ama kinywa. Miongoni mwa dawa hizo hapa nitakuletea baadhi yao. kama wewe pia unasumbuliwa na fangasi wa mdomo basi post hii itakusaidi sana.

Soma Zaidi...
Dawa za mapunye

Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za maounye

Soma Zaidi...
Ijue Dawa ya lignocaine

Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya kutibu kikohozi inayoitwa expectorant

Post hii inahusu zaidi dawa aina ya expectorant katika matibabu ya kikohozi,ni dawa ambayo usaidia au uzuia kikohozi kuendelea kutokea.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya mucolytic dawa ya kutibu kikohozi

Post hii inahusu zaidi dawa ya mucolytic katika kutibu kikohozi kwa watu wazima na watoto.

Soma Zaidi...
Fahamu tiba ya jino

Post hii inahusu zaidi tiba ya jino,ni tiba ya kawaida kwa watu walio na matatizo ya meno, kwa kawaida tunafahamu kwamba jino huwa halina dawa ila dawa yake huwa ni kungoa lakini Leo nawaletea habari njema kwamba jino sio kungoa tena ila Kuna tiba ambayo

Soma Zaidi...