image

Kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini

KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini. Kazi za protini mwilini:- Kujenga mwili; Kupona kwa vidonda na majeraha Kutengeneza antibody (kinga za mwili) Kutengeneza hemoglobin (chembechembe zaseli nyekundu za damu) Kutengeneza enzymes zinatumika katika kumeng;enya chakula Kutengeneza homoni Kuthibiti kichakati na shughuli za ndani ya seli Huhusika katika kutengeneza tishu (nyama na misuli) ndani ya mwili Nywele, kope, nyusi, vinyweleo na kucha hutokana na rotini  

 

1. Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.  

 

2. Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.  

 

3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.  

 

4. Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.  

 

5. Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.  

 

6. Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha. 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1684


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mfuno wa damu na makundi manne ya damu na asili yake nani anayepasa kutoa damu?
Posti hii inakwenda kukujuza kuhusu makundi manne ya damu, asili yake, maana ya antijeni na antibody, pia utajifunza kuhusu mfumo wa Rh. Mwisho utajifunza watu wanaopasa kutoa damu. Soma Zaidi...

Utaratibu wa lishe kwa wagonjwa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wagonjwa Soma Zaidi...

Umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa wajawazito na wanaonyonyesha
Post hii inahusu umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha. Ni hatua ya kupima Mama akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha ili kuepuka hatari ya kumwambikiza mtoto Soma Zaidi...

Madhara ya ulevi
Poshi hii inahusu madhara ya ulevi.Utegemezi wa pombe kwa kawaida humaanisha kuwa mtu anatumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna masuala kuhusu kupoteza udhibiti. Soma Zaidi...

Huduma ya kwanza kwa mgonjwa aliyepata ajali ya kichwa
Ajali ya kichwa na ajali inayotolewa kwenye sehemu mbalimbali za kichwa, ambavyo husababishwa madhara kwa aliyepata ajali hiyo Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEKUNYWA SUMU
Maisha ya mtu yanaweza kuwa hatarini ama kupotea mara moja baada ya kunywa sumu. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyeng'atwa na nyuki
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko Soma Zaidi...

Njia za kutumia Ili kuepuka tatizo la kupungua kwa damu
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa tatizo na kuishiwa damu, kuishiwa damu ni tatizo linolowakumba watu wengi na kusababisha matatizo mengi Soma Zaidi...

Malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele.
Posti hii inahusu zaidi malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele zake, ni sababu ambazo upelekea kumsafisha mgonjwa nywele kama tutakavyoona hapo chini. Soma Zaidi...

Aina za kuungua
Post hii inahusu Aina za kuungua, kuungua ni Hali ya kubabuka kwa ngozi ya mwili na kusababisha madhara mbalimbali Soma Zaidi...

Kazi za mifupa mwilinj
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa mifupa mwilini, mifupa ni mojawapo ya tushy zilizounganika na ufanya kazi kubwa kwenye mwili. Soma Zaidi...