image

Kazi za virutubisho vya protini mwilini

Somo hili linakwenda kukuletea kazi za virutubisho vya protini mwilini

KAZI ZA VIRUTUBISHO VYA PROTINI MWILINI

 

 

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini.

 

1.Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.

 

2.Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.

 

3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.

 

4.Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.

 

5.Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.

 

6.Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 753


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Faida kuu 10 za kula matunda na mboga mwilini - kwa nini ni muhumu kula matunda?
Makala hii inakwenda kukutajia sababau kuu 10 ambazo zinaonyesha umuhimu wa kula matunda kiafya. kwa nini kiafya unashauriwa ule matunda na mboga mara kwa mara? Soma Zaidi...

Faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito, kuna kipindi ambacho wanawake wakati wa ujauzito uchaguza vyakula mbalimbali kuna ambao wanaweza kutumia vitunguu saumu na kupata faida kubwa Soma Zaidi...

Faida za kula Zabibu (grape)
faida za kula tunda zabibu kwa ajili ya afya yako Soma Zaidi...

Namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa matumizi mbalimbali
Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu. Soma Zaidi...

Faida za kula Tufaha (epo)
Tufaha ni katika matunda adimu na matamu, je unazijuwa faida zake kkiafya? Soma Zaidi...

Matunda yenye vitamini C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matunda yenye vitamin C kwa wingi Soma Zaidi...

Faida za uyoga mwekundu
Posti hii inahusu zaidi faida kuhusu uyoga mwekundu ni uyoga unaopatikana katika sehemu mbalimbali na pia kuna waliofanikiwa kupandikiza na kuweza kuvuna ila uyoga huu una siri mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Faida za kula passion
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula passion Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula nyama
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula mihogo
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo Soma Zaidi...

Zabibu (grapefruit)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za zabibu Soma Zaidi...

Chakula cha minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya minyoo Soma Zaidi...