Kazi za vitamin B na makundi yake

Kazi za vitamin B na makundi yake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take

KAZI ZA VITAMINI B NA MAKUNDI YAKE

Vitamini B ni moja kati ya vitamini ambavyo vinahitajika sana mwilini. Athari yeyote ya upungufu wa vitamini hivi inaweza kuonekana moja kwa moja kwenye miili yetu. vitamini B vimegawanyika katika makundi mengi sana ikiwemo B1, B2, B3, B5, B6, B7, B9 na B12. je ungependa kujuwa kazi za vitamini hivi kulingana na aina zake. Endelea na makala hii upate kujifunza kazi za vitamini B.

 

Kazi za vitamini B kulingana na kila kundi la vitamini B

Basi tambuwa kuwa kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-

 

1. B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.

 

2. B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.

 

3. B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo

 

4. B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.

 

5. B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.

 

6. B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.

 

Kazi za vitamini B kwa ujumla

Kwa ujumla vitamini B vina kazi nyingi kama ulivyojifunza hapo juu. Kazi hizi tunaweza pia kuziweka katika ufupisho ufuatao. Lengo la kufupisha ni kukuwezesha msomaji kukumbuka kwa wepesi kazi za vitamini B. Kazi hizo ni kama zifuatazo:-

1. Husaidia mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema

2. Huhitajika kwa ajili ya uzalishaji wa nishati (nguvu) mwilini

3. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mwilini

4. Husauidia katika utengenezwaji wa hemoglobin hizi ni chembechembe katika seli nyekundu za damu

5. Husaidia katika kuchakata DNA

6. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya na kukomaa kwa seli

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 3215

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 ai web app     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEKUNYWA SUMU

Maisha ya mtu yanaweza kuwa hatarini ama kupotea mara moja baada ya kunywa sumu.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kulingana na tatizo

Posti hii inahusu sana mambo ya huduma ya kwanza ambayo huduma ya kwanza inapatikana au inatolewa na mtu yeyote katika jamii .

Soma Zaidi...
Dalili za sumu ya pombe

hatari matokeo ya kunywa kiasi kikubwa cha pombe kwa muda mfupi. Kunywa pombe haraka kupita kiasi kunaweza kuathiri kupumua kwako, mapigo ya moyo, halijoto ya mwili na kunaweza kusababisha Coma na kifo.

Soma Zaidi...
Athari ya kutotibu maambukizi ya kwenye kibofu cha mkojo

Post hii inahusu zaidi athari za kutotibu maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo, nimatazito yanayoweza kutokea iwapo ugonjwa huu hautatibika.

Soma Zaidi...
Madhara ya chakula kutosagwa vizuri tumboni.

Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni.

Soma Zaidi...