image

Kazi za vitamini B mwilini Na upungufu wa vitamini B mwilini

vitamini B vipo katika makundi mengi kma aB1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. Makala hii itakwenda kukutajia kazi kuu za Vitamini B katika miili yetu

Kazi za vitamini B mwilini Na upungufu wa vitamini B mwilini

Kama tulivyoona kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-

 

B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.

 

B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.

 

B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo
 

B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.

 

B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.
 

B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1295


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa Soma Zaidi...

Vyakula kwa wagonjwa wa sukari na utaratibu wao wa lishe
Post hii inakwenda kukufundisha utaratibu wa lishe kwa wagonjwa wenye kisukari pamoja na vyakula salamakwao. Soma Zaidi...

Vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo, ni vyakula ambavyo upunguza makali kwenye uti wa Mgongo. Soma Zaidi...

Faida za kula parachichi
Somo Hili linakwenda kukuletea faida za kula parachichi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Zabibu
Soma Zaidi...

VYANZO VYA VYAKULA VYA MADINI NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kazi ya Piriton
Posti hii inahusu zaidi kazi ya Piriton katika kutibu mzio au akeji ni dawa ambayo kwa lingine huitwa chlorpheniramine Maleate. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kutumia maembe kiafya.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maembe kiafya, tunajua wazi kuwa maembe ni tunda ambalo lina umuhimu kwenye afya na uwa na vitamini C kwa hiyo tunapaswa kujua faida zake kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin C
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin C Soma Zaidi...

Faida za kula parachichi
Somo hili litakwenda kukueleza na kukuelimisha kuhusu umuhimu wa kula parachichi kiafya Soma Zaidi...

Faida za pilipili
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za pilipili Soma Zaidi...

Vyakula vya wanga na faida zake
Soma Zaidi...