picha

Kazi za vitamini B na vyakula vya vitamini B

Makala hii inakwenda kukuletea kazi za vitamini B, pia tutajwenda kuona makundi ya vitamini B na kazi za kila kundi. Pia makala hii inakwenda kukufundisha vyanzo na vyakula vya vitamini B. Utajifunza pia kazi kuu za vitamini B kwa ujumla wake.

KAZI ZA VITAMINI B NA MAKUNDI YAKE

Vitamini B ni moja kati ya vitamini ambavyo vinahitajika sana mwilini. Athari yeyote ya upungufu wa vitamini hivi inaweza kuonekana moja kwa moja kwenye miili yetu. vitamini B vimegawanyika katika makundi mengi sana ikiwemo B1, B2, B3, B5, B6, B7, B9 na B12. je ungependa kujuwa kazi za vitamini hivi kulingana na aina zake. Endelea na makala hii upate kujifunza kazi za vitamini B.

 

 

Kazi za vitamini B kulingana na kila kundi la vitamini B

 

 

Basi tambuwa kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-

 

 

B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.

 

 

 

 

B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.

 

 

 

 

B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo

 

 

 

 

B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.

 

 

 

 

B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.

 

 

 

 

B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.

 

 

Kazi za vitamini B kwa ujumla

Kwa ujumla vitamini B vina kazi nyingi kama ulivyojifunza hapo juu. Kazi hizi tunaweza pia kuziweka katika ufupisho ufuatao. Lengo la kufupisha ni kukuwezesha msomaji kukumbuka kwa wepesi kazi za vitamini B. Kazi hizo ni kama zifuatazo:-

 

1. Husaidia mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema
2. Huhitajika kwa ajili ya uzalishaji wa nishati (nguvu) mwilini
3. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mwilini
4. Husauidia katika utengenezwaji wa hemoglobin hizi ni chembechembe katika seli nyekundu za damu
5. Husaidia katika kuchakata DNA
6. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya na kukomaa kwa seli

 

 

VYAKULA VYA VITAMINI B.

 

Kwa kuwa umesha jifunza kazi za vitamini B kulingana na makundi yake. Je ungependa kujuwa ni wapi unaweza kupata vitamini B? Sehemu hii utajifunza vyakula ambavyo husaidi kutupatia vitamini B. Vyakula hivyo ni kama:-

1. Nyama
2. Mapalachichi
3. Mboga za majani
4. Mimea jamii ya karanga
5. Alizeti
6. Mayai
7. Pilipili
8. Ndizi
9. Viazi
10. Maharagwe na kunde
11. Nafaka kama mchele, mtama na mahindi

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021-06-05 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1664

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Vyakula vya vitamin B

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamin B

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuboresha afya ya meno

Katika post hii utakwenda kujifunza vyakula unavyopasa kul ili kuboresha afya ya meno yako. Pia utajifunza vyakula vilivyo hatari kwa afya ya meno yako.

Soma Zaidi...
MATUNDA YENYE VITAMINI C KWA WINGI

Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula samaki

Posti hii itakwenda kukupa faida za kula samaki kwenye mwili wako.

Soma Zaidi...
Faida za kula magimbi (taro roots)

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi

Soma Zaidi...
Faida za kula Pilipili

Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana

Soma Zaidi...
Faida za majani ya mstafeli

Posti hii inahusu zaidi faida za majani ya mstafeli,ni majani ambayo utibu magonjwa mbalimbali hasa saratani, kwa hiyo tunapaswa kuyatumia ili tuweze kupata matibabu ya kansa mbalimbali.

Soma Zaidi...
Faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito

Posti hii inahusu zaidi faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito, kuna kipindi ambacho wanawake wakati wa ujauzito uchaguza vyakula mbalimbali kuna ambao wanaweza kutumia vitunguu saumu na kupata faida kubwa

Soma Zaidi...