KIAPO CHA SULTANI


image


Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela


KIAPO CHA SULTANI.

Hapo zamani sana katika nchi za Uajemi , china na hindi kulitokea sultani aliyefahamika kwa kuwa na upendo kwa watu wake na nguvu pia ya kijeshi na kuitawala. Watu wake walimpenda sana na yeye aliwapenda. Sultani huyu alikuwa na watoto wawili ambao ni Shahriyar ambaye ndiye mkubwa na mwingine ni Shahzanam ambaye ndiye mdogo.

 

Watoto hawa pia walitambulika kwa ushujaa walio nao na uhodari katika mambo mbalimbali, hususan katika fani ya kupanda farasi. Sultani huyu alipofariki utawala wake akamwachia mwanaye mkubwa ashike madaraka yake. Na mwanae mdogo akabakia anatawala maeneo mengine katika utawala wa baba yake. Huyu mdogo akaelekea maeneo ya Samarkand na huyu mkubwa akabaki palepale.

 

Sultan Shahriyar alikuwa na mke wake aliyempenda sana kwa muda mrefu. Hakuwahi kuamini kama itaweza kutokea sikumoja akamsaliti. Ilitokea sikumoja akamkuta mkewake anazini na mtumwa wake. Kitendo hiki kilimuuma sana na akamuuwa mkewe na yule mtumwa. Kutokea hapo akaapa kutokumwamini mwanamke yeyote duniani. Na kitendo hiki kilimfanya ajiwekee utataratibu mpya wa maisha nao ni kuoa kila siku mke mpya na kisha humuuwa ifikapo asubuhi.

 

Hivyo mambo yakawa kama hivi kila siku jioni bibi harusi mpya mwanamwari huolewa na na ikifika asubuhi huuliwa. Kitendo hiki kiliendelea kwa muda mpaka watu wakawa wanaogopa. Ikiwa nyumba moja watu wanalia kwa kufiwa na bint yoa nyumba nyingine hufanyika harusi. Sultani alikuwa na waziri wake maalum ambaye alikuwa amepewa kazi hii ya kumletea mfalme wanawari na kutekeleza amri ya kuwauwa kila ifikapo asubuhi.

 

Waziri huyu aliyepewa kazi hii alikuwa na watoto wawili aliyewapenda sana, mmoja aliitwa Schehra-zade ambaye ndiye mkubwa na Dinar-zade ambaye ndiye mdogo. Schehra-zade alipata upendo mkubwa kutoka kwa baba yake. Alipewa taaluma mbalimbali za matibabu, sanaa, kuandika, masimulizi , kazi za mikono na nyingine nyingi. Ukiacha mbali na taaluma hizi pia alijulikana kwa uzuri wake ulioaminika kuwashinda wanawake wote katika nchi hiyo. Mabinti wawili hawa walipendana zaidi kila mmoja.

 

Ilitokea siku moja katika mazungunzo waziri mkuu akiwa na mabinti zake wanaongea Schehra-zade alitowa ombi kutoka kwa baba yake ambalo lilionekana kumshangaza sana.

“baba ninaombi ila niahudi kwanza kuwa utanitekelezea” alizungumza Schehra-zade kumwambia baba yake. “naahidi nitalitekeleza kama lipochini ya uwezo wangu” alisikika waziri mkuu akimjibu binti yake.

“ninataka kukomesha tabia ya kikatili ya sultani kuuwa mabint” mmmmhhh mwanangu kipenzi, vip utaweza kumaliza tabia hii ya sultani wetu? Ni maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kati ya waziri na mwanae. “baba ninataka unipeleke mimi kwa sultani niwe mkewe” alizungumza Schehra-zade. Mwanangu unafahamu fika kuwa ukuolewa punde tu ifikapo asubuhi nitaamriwa nikuuwe” alizungunza waziri kwa masikitiko makubwa.

 

Schehra-zade aliendelea kusisitiza ombi lake la kutaka kuolewa na sultani ili akamalize tabia yake ya kuuwa mabinti. Waziri nae hauacha kumsihi mwanae asithubutu kijiingiza kwenye matatizo haya makubwa. Wazii akawa anamwambia mwanae “ hivi mwanangu unataka nikufanye kitugani mpaka uachane na msimamo wako huo? Au unataka yakupate yalompata mke wa mfugaji?” kwa shauku Schehra-zade akauliza “kwani baba ni kitu gani kilimpata mke wa mfugaji” mmmmhh.. Ni habari kubwa lakini nitatakusimulia hadithi yake” alizingumza waziri na kuanza kusimulia hadithi hii



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Hadithi iliyosimuliwa na kijakazi wa sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi ya jini na mfanya biashara
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki. Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, baada ya kijana wa kiume wa binti mfalme kuoa yule ndugu yake baba anafanya sherehe kubwa na wake wenza wamepata habari kwamba kijana wa kiume wa mfalme ameoa ndugu yake wakaamuru kunyamaza ili waje watoe siri siku ya kuapishwa kwa mfalme. Soma Zaidi...

image USALITI (sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara. Soma Zaidi...

image Hadithi ya mke na kasuku
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo. Soma Zaidi...

image Nje ya jumba la kifahari la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...