image

Kiasi Cha mkojo kisichokuwa cha kawaida.

Hii posti inahusu zaidi sifa za mkojo usio wa kawaida,ukiona mkojo wa namna hii unapaswa kwenda hospitalini kwa matibabu au vipimo vya zaidi.

Kiasi Cha mkojo kisicho Cha kawaida

1.kiasi Cha mkojo , 

Kuna wakati mwingine kiasi Cha mkojo ubadilika na kuwa mwingi au kidogo, ikiwa kiasi Cha mkojo kinaongezeka kuliko kawaida inawezekana ikawa ni shida ya sukari mwilini hii hali ya mkojo kuwa mwingi huitwa polyuria  na pengine kiasi Cha mkojo kuongezeka inawezekana mtu ametumia dawa kama vile frusemide,au lasix, potassium citrate na digitalis hizi ni dawa ambazo uongeza kiwango Cha mkojo.

 

2.Na Kuna wakati mwingine kiasi Cha mkojo kinapungua hii kwa kitaalamu huitwa Oliguria kiasi Cha mkojo kinapungua ndani ya maasaa ishilini na manne hili tatizo utokea zaidi kwa watu wenye matatizo kwenye nephroni, matatizo ya moyo, na watu wale wenye ugonjwa wa kuishiwa maji  iwapo mtu anaona dalili hizi za kuona kiasi kidogo Cha mkojo anapaswa kwenda hospitalini kupima.

 

3. Kuna wakati mwingine mkojo ukosa kabisa na figo linakuwa halitoi kabisa mkojo,hii ni hatari kwa sababu kunakuwepo na matatizo kwenye nephroni au kwenye figo au pengine damu inashindwa kusafili mpaka kwenye figo na usababisha kutokuwepo kwa mkojo kwa mtu, hii hali ikitokea ndani ya maasaa ishilini na manne mgonjwa  Inabidi apelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi.

 

4 Tunapaswa kujua kuwa kitendo Cha mkojo kukosa ndani ya maasaa ishilini na manne ni tofauti na Ile hali ya mtu kusikia mkojo lakini akawa anashindwa namna ya kupitisha kwa Sababu maalumu kwa hiyo tunapaswa kumhudumia mgonjwa ambaye anakosa mkojo na kunywa anakunywa kila kitu kama kawaida.

 

5. Kwa hiyo tukiona kitendo Cha mtu kukojoa mara kwa mara, au kukojoa kidogo,au kushindwa kukojoa kabisa tujue kuwa sio dalili nzuri kwa sababu mkojo unachujwa kutoka sehemu mbalimbali za mwili Ili kuondoa sumu mwilini, kwa hiyo sumu isipoondolewa shida nyingine zinaweza kutokea kwenye mwili wa binadamu na kusababisha madhara mengine makubwa,kwa hiyo tunapaswa kudhibiti hali hii mapema.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1004


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu, kama mtu amepoteza fahamu Kuna mambo muhimu yanapaswa kuangaliwa kwa makini kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Zijue kazi za uke (vagina)
Uke ni sehemu ambayo imo ndani ya mwili wa mwanamke, sehemu hii ufanya kazi mbalimbali hasa wakati wa kujamiiana, kubarehe na kujifungua kwa mama. Soma Zaidi...

Namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi Soma Zaidi...

Aina za vidonda
Posti hii inahusu zaidi Aina mbalimbali za vidonda kwenye mwili wa binadamu, ni vidonda ambavyo utokea kwenye mwili wa binadamu kwa Aina tofauti. Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO
Soma Zaidi...

Upungufu wa vyakula na madhara yake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula Soma Zaidi...

Faida za tumbo katika mwili wa binadamu
Posti hii inahusu zaidi faida za tumbo,tumbo ni sehemu ya mwili ambayo ushughilika na kutunza chakula, Soma Zaidi...

Huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Post hii inahusu zaidi tiba na huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri. Soma Zaidi...

Njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu. Soma Zaidi...

nina upungufu wa damu HB 4 niko nyumban maana hispitali nimeruhusiwa ila nina kizungu zungu
Nina shida. Soma Zaidi...

Faida za seli
Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

Namna ya kutunza nywele za mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi. Soma Zaidi...