image

Kiungulia na tiba zake kwa wajawazito.

Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.

Kiungulia na tiba zake kwa wajawazito.

1. Kwanza kabisa kiungulia uwapo wanawake wajawazito wakiwa kwenye wiki kuanzia ya thelathini mpaka arobaini,hali huu utokea kwa sababu progesterone homoni inalegeza cardiac sphincter za tumboni  na kusababisha acid kurudi kwenye oesophagus na kusababisha kiungulia, kwa hiyo wajawazito walipatwa na hali kama hizi hawapaswi kuogopa au kuwa na wasiwasi wajue kuwa ni kitu cha kawaida utokea na uisha tu baada ya kujifungua. Na pia wauguzi wanapaswa kuwaambia wazi wajawazito ili watambue Dalili kama hizi wakati wa ujauzito.

 

2. Hili kupunguza hali hii ya kiungulia wanawake wenye mimba wanapaswa kuepuka  kuinama kwa mda mrefu  wakati wanapokuwa wanafanya kazi zao za kila siku, kwa hiyo wanapaswa kujua hali yao kwa hiyo ni vizuri kufanya kazi wakiwa wamesimama pindi wakisikia hali ya kiungulia au wanaweza kuwekewa kiti au meza wakati wa kufanya kazi kama vile kuosha vyote na kufua wakafanya wakiwa wamesimama na pia wote waliowazunguka wanapaswa kujua hali huu na kuwasaidia akina mama wajawazito ili waweze kufanya kazi zao bila kuinama.

 

3. Kama hali ya kiungulia imezidi sana wajawazito wanapaswa kula chakula kidogo kidogo kwa siku ili kuepuka hali ya kupata kiungulia kwa mfano anaweza kula saa mbili, saa nne, saa sita, saa nane, saa kumi, saa kumi na mbili na kuendelea mpaka mda wa kulala, kwa kufanya hivyo anaweza kuepuka kupata kiungulia mara kwa mara, nimesema hivyo kwa sababu kuna akina mama wajawazito wanaopata kiungulia cha hali ya juu sana kuliko wengine na pia watu wa karibu wanapaswa kujua hili na kuona kuwa ni hali ya kawaida na kuendelea kumjali Mama katika kupambana na hali yake ya mda mfupi tu.

 

4. Pia wanawake wajawazito wanapaswa kulala wakiwa na mito ya kutosha ili kuepuka kiungulia na pia wajawazito kama hawajalala na mito ya kutosha wanaweza kuteseka sana wakati wa usiku au mda wowote wa kupumzika kwa hiyo wauguzi na wataalam wengine wa afya wanapaswa kumweleza mama huduma hii ya kutumia mito ili kupunguza kuwepo kwa kiungulia na pia watu wa karibu wa Mama mjamzito wanapaswa kuhakikisha kuwa Mama anapata mito kadiri ya uhitaji.

 

5. Pia hali huu ya kiungulia ikizidi hata kama ni kawaida kwa wajawazito wanaweza kwenda hospitalini, kwa maana kuna dawa ambazo utibu ugonjwa huu dawa hizi ni kama vile  anti acid na sawa nyingine kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya, kwa hiyo tunapaswa kuwaambia ukweli pale hali ikizidi wajawazito wanapaswa kwenda hospitalini kupata dawa za kuwatuliza hali zao.

 

6. Kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa wanawake wenye mimba Upata magonjwa madogo madogo kama kiungulia na wanapaswa kupata huduma za muhimu kwao kwa hiyo jamii inapaswa kuwaelewa na kuwahudumia kwa kadiri inavyowezekana na kuwa pamoja nao kwa sababu haya matatizo madogo kama kiungulia ni ya mda tu na Mama akijifungua yanapotea mara moja.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/12/Wednesday - 05:49:08 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 680


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Matibabu ya vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu. Soma Zaidi...

VIDONDA VYA TUMBO NA ATHARI ZAKE
Soma Zaidi...

Dalili za vidonda vya tumbo, matibabu na dawa zake, sababu za kutokea kwake
Utajifunza chanzo cha vidonda vya tumbo, dalili zake, dawa na matibabu yake pamoja na njia za kujilinda na vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Dalili za presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka Soma Zaidi...

Vijuwe vidonda vya tumbo na madhara yake.
Madonda ya tumbo ni ugonjwa unaotokana na kuwepo kwa vidonda kwenye Koo, tumboni na kwenye utumbo mdogo Soma Zaidi...

Dalili za hatari kwa mtoto aliyezaliwa
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mtoto aliyezaliwa, ni dalili ambazo ujitokeza tu mtoto anapozaliwa kwa hiyo dalili hizi zinapaswa kuzuiwa ili zisilete madhara makubwa. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa Ugumu wa kumeza (dysphagia)
Ugumu wa kumeza (dysphagia) inamaanisha inachukua muda na bidii zaidi kuhamisha chakula kutoka kwa mdomo wako hadi kwenye tumbo lako. Ugumu wa kumeza unaweza pia kuhusishwa na maumivu. Katika baadhi ya matukio, kumeza inaweza kuwa haiwezekani. Ugumu w Soma Zaidi...

Matibabu ya VVU na UKIMWI
Somo Hili linakwenda kukuletea matibabu ya VVU/UKIMWI Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa gonoria (gonorrhea)
UGONJWA WA GONORIA NA DALILI ZAKE (GONORRHEA)Gonoria (gonorrhea) ni katika maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono. Soma Zaidi...

Dalilili za Ngozi kuwa kavu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ngozi kuwa kavu si mbaya, lakini inaweza kusumbua na isipendeze, ikitengeneza mistari laini na Mikunjo. Soma Zaidi...

Dalili za maumivu yanayosababishwa na mtiririko mdogo wa Damu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maumivu yanayosababishwa na mtiririko mdogo wa damu, kwa kawaida wakati wa mazoezi. Wakati mwingine huitwa upenyo wa vipindi, hali hii kwa ujumla huathiri mishipa ya damu kwenye miguu, lakini upenyo unaweza kuathiri mi Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ugonjwa huu uaribu zaidi kwenye mifupa na sehemu nyingine ambazo zinakaribia kwenye mifupa Soma Zaidi...