Kiwango cha juu cha Androgen

Posti hii inahusu zaidi homoni ya androgen, ni homoni ambayo imo kwa wanaume na ikizidi kwa kiwango chake inaweza kuleta shida kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo homoni hii inaweza kuleta shida iwapo ikiongezeka kwa kiasi kikubwa.

Kiwango cha juu cha homoni ya Androgen.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa homoni hii ya androgen ni homoni ambayo imo kwa wanaume na inapaswa kuwa sawia kabisa Ili kuweza kufanya kazi zake vizuri, ila ikiongezeka inaweza kuleta madhara Katika udharishaji kwa hiyo ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa aina hii ya homoni inakuwa sawa kabisa Ili kuweza kufanya kazi yake vizuri na kwa ufasaha kabisa, ila Kuna dalili mbalimbali zinaziweza kutokea ikiwa homoni hii imekuwepo kwa kiwango kikubwa kwenye mwili wa binadamu.

 

2. Kuwepo kwa vipele vyekundu na vyeusi vikiandamana na chunusi  hasa hasa usoni  na pia ngozi uonekana kuwa na mafuta mengi sana mwilini , kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizo ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kutoa ushauri na kumalizana na tatizo.

 

3. Hali hii ikitokea kwa mwanamke usababisha mwanamke kuota ndevu na vinyweleo vingi kwenye  mikono  na miguuni, kwa hiyo ndio maana unaweza kukuta akina Mama wenye ndevu na vinyweleo vingi kwenye mikono na miguuni na pia wengine wanakuwa na sauti ya kiume, hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa wingi wa homoni ya androgen ambayo inapaswa kuwa kwa mwanaume kwa wingi kuliko kwa mwanamke.

 

4. Kuwepo kwa nywele nyepesi .

Watu wengine unakuta nywele zao zinakuwa nyepesi kuliko kawaida kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango cha juu cha homoni ya estrogen.

 

,5. Kuwepo kwa ugumba.

Kwa sababu hii homoni inapaswa ku balanced Ili kuweza kuruhusu uzalishaji kutokea ila ikiwa juu uzalishaji unakuwa WA shida 

 

6. Kuwepo kwa uvimbe kwenye via vya uzazi.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na uvimbe kwenye via vya uzazi hali hii inasababishwa na kuwepo kwa kwa kiwango kikubwa cha homoni ya androgen.

 

7. Pamoja na Dalili zote hizi sio dalili zote ni kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya androgen kwa hiyo vipimo ni muhimu kabisa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/03/Sunday - 10:48:28 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1016


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-