image

Kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi

Posti hii inahusu zaidi sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi, kwa kawaida kondo la nyuma huwa nyuma ya mlango wa kizazi ila Kuna wakati kondo la nyuma ujishikisha mbele ya mlango wa kizazi.

Sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa mtoto akija kuzaliwa utanguliza kichwa na kutoka kwenye tumbo la Mama ila Kuna wakati mwingine kondo la nyuma ndilo utangulia na kufuatia mtoto hii ni hatari kwa mtoto kwa Sababu hii kesi kama haijakutana na myaalamu wa kuzalisha mtoto anaweza kufia tumboni kwa hiyo ni vizuri kumtambua dalili na kumsaidia mama akaweza kujifungua salama.

 

2. Sababu ya kutanguliza kondo la nyuma badala ya mtoto pengine nikwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi in kwenye mfuko wa kizazi kwa hiyo kondo la nyuma uweza kujishikisha sehemu ambayo Haina maambukizi na kusababisha kondo la nyuma kutangulia mapema wakati mtoto anapozaliwa.

 

3. Kuwepo kwa makovu kwenye mfuko wa uzazi.

Pengine kwenye mfuko wa kizazi panakuwepo na jeraha na jeraha hilo kwa wakati mwingine uwa kwenye sehemu ambayo kondo la nyuma linapasaw kujishikiza kwa hiyo ujishikiza sehemu yoyote ambayo ni tofauti na sehemu ya kawaida.

 

4. Kuwepo kwa upasuaji ambao umefanyika kabla ya mimba haijatungwa na yenyewe usababisha kuwepo kwa kitendo cha kondo la nyuma kujishikiza chini ya mlango wa kizazi na kusababisha madhara makubwa wakati wa kujifungua.

 

5.  Mwonekano wa tumbo la uzazi kutokuwa la kawa, Kuna wakati mwingine tunaweza kumwona mtu yupo anatembea na ameumbika kawaida kwa nje ila ukija kuangalia kwa ndani mfuko wa uzazi ni tofauti na wengine kwa kitaalamu huitwa abnormally of uterus, kwa hiyo kama hauko kawaida usababisha kondo la nyuma kujishikiza sehemu yoyote isiyokuwa ya kawaida na kusababisha kondo la nyuma kutangulia mtoto.

 

6. Kwa kawaida kuja kumtambua kuwa Mama ana tatizo hili ni kufuatana na ujuzi wa muuguzi kwa sababu Mama anakuwa na uchungu kawaida na sifa zote za kujifungua ila shida kilichotangulia ndicho hakieleweki, kwa hiyo hali hii ikigundulika ni vizuri kumpeleka mama hospital Ili kuweza kumsaidia zaidi maana kama hakuna huduma mtoto anaweza kufia tumboni





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2495


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Dalili za Maambukizi na Uvimbe katika mirija ya uzazi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi na uvimbe katika  mirija ya uzazi. Mara nyingi hutumiwa sawa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupa nyonga (PID), ingawa PID haina ufafanuzi sahihi na inaweza kurejelea magonjwa kadhaa ya njia ya juu ya uzazi Soma Zaidi...

Sababu za mwanamke kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa
Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Soma Zaidi...

Mimba kutoka kabla ya umri wake
Posti hii inahusu zaidi kuhusu kwa mimba kutoka kabla ya mda wake,ni kitendo ambacho mimba utoka kabla ya wiki ishilini na na nane. Soma Zaidi...

MAJIMAJI YA UKENI, PIA MIWASHO YA UKENI, FANGASI WA UKENI, UCHAFU UNAOTOKA UKENI, SARATANI AU KANSA YA KIZAZI
Soma Zaidi...

Madhara ya tumbaku na sigara
Post hii itakwenda kuangalia madhara ya tumbaku na sigara anayoweza kuyapata mvutaji Soma Zaidi...

Jifunze kuhusu Protini, Fati, Wanga na kazi zao mwilini na vyakula vinavyopatikaniwa kwa wingi
Soma Zaidi...

Fahamu Faida za Uzazi wa mpango
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za Uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango ni huduma ambazo hutoa chaguo kwa familia kuwa na idadi ya watoto wanaotaka katika muda maalum, wanahisi na mbinu iliyoamuliwa. Soma Zaidi...

Je kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo?
Nimesoma makala yenu, sasa nina swaliJe kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo? Soma Zaidi...

Mimba huonekana katka mkojo baada ya muda gan tangu itungwe
Kipimo cha mimba kwa mkojo kimekuwa kikitumika sana kuangalia ujauzito. Kipimo hiki kinapotumika vibaya kinaweza kukupa majibu ya uongo. Kuwa makini na ujue muda sahihi. Soma Zaidi...

Namna ya kutunza joto la mtoto mara tu baada ya kuzaliwa.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kutunza joto la mtoto mara tu anapozaliwa,tunajuwa wazi kuwa Mama anaweza kujifungulia sehemu yoyote ile kabla hajafika hospitalini kwa hiyo mtoto anapaswa kuwa na joto la mwili la kutosha i Soma Zaidi...

Zifahamu fibroids (uvimbe kwenye via vya uzazi)
Posti hii inahusu zaidi fibroids au uvimbe kwenye via vya uzazi hasa hasa utokea kwenye tumbo la uzazi ambapo kwa kitaalamu huitwa uterusi, uvimbe huu ulitokea watu wengine huwa hawawezi kutambua Dalili zake mapema kwa hiyo leo tunapaswa kujua Dalili zake Soma Zaidi...

Mabadiliko ya uzito kwa mjamzito
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya uzito kwa mjamzito, hii ni hali ya kubadilika kwa uzito kwa Mama akiwa na Mimba Soma Zaidi...