KUAMINI MITUME WA MWENYEZI MUNGU


image


Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu


  1. Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).

-    Mitume ni wanaadamu wanaume walioteliwa ili kuwaongoza na kuwa mifano bora ya kuigwa kwa watu (ummah) wao katika kutekeleza ujumbe wao.

 

  • Idadi kamili ya mitume wote wa Mwenyezi Mungu (s.w) haijulikani, bali waliotajwa ndani ya Qur’an ni 25.

Rejea Qur’an (10:47), (6:83-86)

Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.23.

 

  • Sifa za Mitume.
    1. Ni watu walizaliwa, walioa, walikula, waliugua, walikufa, n.k. kama binaadamu wa kawaida isipokuwa Nabii Adamu (a.s).
    2. Walikuwa na kila tabia njema, wakweli, waaminifu na wenye huruma.
    3. Walikuwa na upeo wa Elimu wa hali ya juu kuliko watu wote enzi zao kwa sababu kuletewa kwao wahayi.
    4. Walikuwa Wacha-Mungu wa hali ya juu kuliko watu wote.

 

  • Kazi za Mitume.
  1. Kufahamisha na kufundisha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w) na sifa zake. Qur’an (21:25), (16:36).
  2. Kufahamisha mambo ya ghaibu (Akhera) kama Moto, Pepo, Kiyama, Hisabu, Maisha ya Barzaq (kaburini) n.k. 
  3. Kufundisha njia sahihi ya maisha anayoiridhia Mwenyezi Mungu inayopelekea kunusurika na adhabu zake. Qur’an (3:164).
  4. Kusaidiana na wafuasi wao katika kuamrisha mema na kuondosha maovu katika jamii.
  5. Kuonya kutokana na adhabu na kubashiria mema kwa wafanyao mema.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Lengo la funga linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Haki za binadamu kwa ujumla (basic human rights)
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Funga za Sunnah na umuhimu wake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kumuamini mwenyezi Mungu (S.W)
Nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Madhumuni ya dola ya uislamu
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maana ya kuamini malaika katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Msonge wa uongozi na siasa katika serikali ya kiislamu mafinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa. Soma Zaidi...