Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

-    Maandalizi (mafunzo) haya yalikuwa ya Kiil-hamu ambayo hata Muhammad mwenyewe na jamii haikujua kuwa anaandaliwa, na yalikuwa kama ifuatavyo;

 

  1. Kuzaliwa katika kabila tukufu la Kiqureish ambalo ni kizazi cha Nabii Ibrahim (a.s) kupitia kwa Nabii Ismail (a.s).

Rejea Qur’an (2:129).

 

  1. Kupewa jina la Muhammad na babu yake lililo na maana sawa na ‘Ahmad’- Mshukuriwa, alilotabiriwa nalo katika Injili, na Qur’an pia.

   Rejea Qur’an (61:6).

 

  1. Malezi bora aliyopata kupitia Mama yake mzazi, Bi Halimah, babu yake Abdul-Muttalibu na Ami ya Abu Talibu pamoja na kuwa alikuwa yatima.

Rejea Qur’an (93:6).

 

  1. Tabia yake njema isiyo na mfano kuanzia utotoni hadi utuuzima wake kutoathiriwa na kila aina ya ubaya.

Rejea Qur’an (68:4).

 

  1. Ndoa yake Muhammad (s.a.w) na Bi Khadija bint Khuwailid, aliiandaa Allah (s.w) ili kumuwezesha Muhammad kuitumikia jamii hata kabla ya utume.

Rejea Qur’an (93:8).

 

  1. Kuchukia kwake maovu na kujitenga pangoni ili kutafuta msaada ulio nje ya uwezo wa kinaadamu baada ya kufanya jitihada mwisho wa uwezo wake.

   Rejea Qur’an (93:7) na (94:1-3).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1198

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana: