Kuelekea bonde la uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

KUELEKEA BONDE LA UOKOZI

Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi. Alikwenda kwa muda wa dakika 30-50 na akatua kwenye bonde lenye milima. Alipotua nikajifungua na kwawoga alishituka na kuniacha pale. Nikaondoka kwa haraka na kujificha asijeniona. Muda haukupita roc alikamata nyoka mkubwa sana na kumkata vipande. Alimla na kuondoka na kipande. Alipoondoka na mimi nikatoka mafichoni pale na kuanza kuchunguza eneo lile na kujua vipi nitatoka pale.

 

Nilipochunguza zaidi eneo lile nikagungua ni bonde lililopochini sana na limezungukwa na milima mirefu yenye mawe. Ni bonde ambalo katu mtu asingeweza kutoka. Mchana mzima nilikuwa nikitafuta pa kutokea lakini bila mafanikio. Japo nilikuwa najishauri kuwa bora hapa kuliko kule kisiwani. Usiku ulipoingia nilijificha kwenye mapango na kulala. Usingizi haukuja kabisa kwa woga. Kwani uksiku nyoka walokuwa wakiogopa mchana kuliwa na roc walikuwa wakitoka kutafuta chakula.

 

Muda wote nilikuwa nikimuomba Mungu dua aniokoe na wadudu wabaya usiku ule. Mwenyezi Mungu alinilinda na ulipofika asubuhi nikaendelea na uchunguzi wangu wa eneo lile. Kwa ghafla nilishituliwa na kishindo nyuma yangu. Nilipogeuka nikakuta ni kipande kikubwa cha nyama. Nyama. Hapa nikakumbuka hadithi ya zamani sana juu ya bonde la wawinda madini. Wazee wetu walikuwa wakitusimulia kuwa kuna watu wanawinda madini kwa kutumia nyama. Yaani wanatupa nyama kwenye bonde lenye madini, kisha nyama ile inaganda vipande vya madini na pindi ndege wanapokuja kuchukua nyama ile ambayo ina madini yaloganda kutoka bondeni huwakimbiza ndege wale na wanapoidondosha wanachukua madini.

 

Pale nikawa nawaza huende hii ikawa ndio njia pekee ya mimi kutoka pale. Nikawa naangalia kama nitaona mtu lakini sikuweza kuona kwani juu ni mbali sana. Basi nikaamza kuokota madini mapande makubwa makubwa. Eneo lile lilikuwa na madini mengi na makubwa yalokuwa waziwazi. Niliokota almasi na dhahabu kwa wingi pamoja na madini mengine. Nilipomaliza nikayafunga kwa uzuri sana na kuanza kutengeneza mpango wa kutoroka pale nilipofungwa.

 

Kwakuwa mapande ya nyama yalokuwa yakitupwa yalikuwa ni makiubwa sana, nikachagua lile kubwa zaisi na kujifunga nali na kujificha kwenye kanzu yangu. Baada ya muda ndege mkubwa sana alikuja ndege aina ya eagle. Ndege yule ana watoto hivyo alichagua pande kubawa na kuondoka nalo. Pande hili ndo lile ambalo nipo. Alinipeleka mpaka kwenye kitundu chake. Na haukupita muda watu wengi wakatokea na kuanza kumtisha ndege yule na kunidondosha mimi na nyama ile.

 

Kumbe wale wawinda madini kila mmoja alikuwa na kitundu chake, hivyp walishangaa baada ya nyama anatoka na mtu. Niliwasimulia yote yalonopata. Walinipa pole lakini kwa kuwa nilikuwa na madini mengi sana yule mwenye kitundu chake nilimwambia achukue kiasi anachotaka na akachukua pande moja tu. Kisha akaniachia mengie, nikawagawia na wenzie. Tulikaa eneo lile kwa muda wa wiki tukiwinda madini na baada ya hapo tukaanza kurudi baghadadi, kwa kuwa na wale walikuwa wakiishi bafhdad ila hatukuwa tukijuana kwa kuwa ni wa mji mwingine.

 

Njiani tulipita misitu mikubwa na yakutisha, tulipishana na manyoka wakubwa sana hata tukafika ufukweni na nikauza baadhi ya madini yangu kwenye kisiwa cha Balrora. Nikanunua pale bidhaa kadhaa na zawadi za kupeleka nyambani. Siku tatu baadae tulipanda jahazi la kuelekea baghadad na tulipofika kwanza nikaanza kutoa sadaka na zaka mali zangu na nikawasimulia ndugu zangu yote yaloniptata. Walinipongeza sanana na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunirudisha salama.

Nilikusanya watu na kufanya dua na kutoa sadaka zaidi kama ni shukrani yangu kwa msaada alonipa mwenyezi Mungu hata akanirudisha salama. Niliamua sasa kutofanya biashara nyingine za baharini na kuanza biashara ndogo ndogo. Nilifanya hivi kwa muda wa miezi sita, huku nikawa nafatilia habari za wasafiri. Muda wote huo sikusikia ajali yeyote na walikuwa wakinisifia faida walokuwa wakizipata. Nilivutiwa zaidi na nikasahau machungu yote yalonipata. Nikaamua kuanza safari ingine ya tatau.

 

Baada ya kumaliza hadithi hii Sinbad wa baharini akampatia Sinbad mbeba mizigo kiasi cha pesa kama ni fidia ya kupoteza muda wake wa kazi na kusikiliza hadithi yake. Kisha akamuahidi kesho awahi ili ajepata yalomkuta safari ya tatu. Akawaambia watu wote walokuwa pale kuwa kesho wawahi maana safari hii amekutwa na mengi ya kustaajabu. Basi watu wote wakatawanyika pale na Sinbad wa baharini akaingia ndani kwake.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 570

Post zifazofanana:-

KAMA UNASUMBULIWA NA FANGASI
Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye. Soma Zaidi...

Namna za kujilinda na fangasi ukeni
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuepuka fangasi za ukeni, ni njia ambazo usaidia kuepuka madhara ya fangasi za ukeni. Soma Zaidi...

Dawa za kifua kikuu.
Post hii inahusu zaidi dawa zinazotumika kutibu kifua kikuu, dawa hizi zimegawanyika kwa makundi makubwa mawili na kila kundi na dawa zake, watu wengine utumia kundi la kwanza na wengine utumia kundi la pili kufuatana na jinsi mwili wa mtu ulivyopokea Ain Soma Zaidi...

Nafasi ya Elimu katika uislamu
Je ni ipi nafasi ya Elimukatika dini ya uislamu? Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la tano (5)
Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...

Dalili za kipindupindu na njia za kujilinda na kipindupindu.
Post hii inazungumzia zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindu.kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu anaitwa vibrio cholera.mdudu huyu hushambulia utumbo mdogo na kusababisha madhara mengi. Soma Zaidi...

Namna ya kumsaidia mtoto mwenye UTI
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI. Soma Zaidi...

Kazi ya Piriton
Posti hii inahusu zaidi kazi ya Piriton katika kutibu mzio au akeji ni dawa ambayo kwa lingine huitwa chlorpheniramine Maleate. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa vericose veini
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini Soma Zaidi...

Hadithi ya mfalme na waziri wake
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...