image

Kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao

KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO

Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Akaunti kuhakiwa inamaana kuna mtu amelogin kwenye akaunti yako bila ya ruhusa yako ama bila ya kumpatia neno la siri. Facebook imeweka njia kadhaa kuhakikisha kuwa akaunti za watu zipo salama muda wowote.

 

Two-factor authentication ni katika njia mujarabu ambazo facebook wameweka ili kulinda akaunti za watumiaji wake. Kwa kutumia njia hii hata kama mtu anaijuwa password yako (neno la siri) hataweza kuingia kwenye akaunti yako ya facebook mpaka awe na laini yako ambayo namba yeke umeisajili facebook.

 

Njia hii inaongeza tabaka lingine la usalama wa akaunti yako ya facebook. Baada ya kuingiza neno la siri kwenye akaunti yako ya facebook, facebook watakutumia code (namba sita) kwenye laini yako ulioisajili facebook. Namba hizo utaziingiza kwenye kibox na ndipo utaruhusiwa kuingia kwenye akaunti.

 

Kuanza kutumia  njia hii ingia kwenye setting, kisha security and login kisha Two-Factor Authentication. Utatakiwa kuingiza namba ya simu na maelekezo machache yatafuata. Utalogout kisha utalogin tena ili kuthibitisha huduma kama ipo tayari.

 

Njia hii itasaidia sana kwa wale ambao tayari password zao kuna watu wanazifahamu. Hata kama mtu anaijua password TROJAN) yako katu hataweza kuingia kwenye akaunti yako mpaka awe na laini yako. Karibia mitandao mingi inatumia njia hii ikiwemo google, linkedin, github na mingine mingi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 828


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO
Namna ya kutunza betri yako iweze kudumu kwa muda mrefu Soma Zaidi...

Nini maana na Trojan na ni zipi athari zake kwenye kompyuta ama simu
Soma Zaidi...

EPUKA MALWARE (VIRUSI, WORM NA TROJAN UKIWA MTANDAONI)
Malware ni neno pana na watu wengi si wenye kulitumia. Soma Zaidi...

KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Soma Zaidi...

Chanzo cha matatiza ya simu/kompyuta
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Utafanyaje ili blog yako ionekane Google, Big, Yandex ama yahoo?
Post hii inakwenda kukufundisha kwa ufupi jinsi ya kuifanya blog yako, ama post za kwenye blog yako ziweze kupatikana kwenye search Engine kama Google, Bong, yandex na yahoo. Soma Zaidi...

Njia rahisi ya kudownload video YouTube
Posti hii inakwenda kukuelekeza kuhusu njia rahisi ya kudownload video YouTube Soma Zaidi...

SIRI
Hii ni game ya maandishi bila ya kutumia vioneshi (graphics). Soma Zaidi...

Kufungua program nyingi kwa wakati mmoja
Posti hii inakwenda kukuelekeza njia za kufungua program nyingi kwa wakati mmoja Soma Zaidi...

Utunzaji wa betri la kifaa chako
Posti hii inakwenda kukupa elimu kuhusu utunzaji wa betri la kifaa chako Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

Maana ya legacy contact katika Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya legacy contact katika facebook Soma Zaidi...