KUMUAMINI MALAIKA WA MWENYEZI MUNGU...


image


Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)


  1. Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
  • Maana: Malaika ni viumbe walioumbwa kutokana na nuru.

 

  • Sifa za Malaika:

- Ni viumbe wa kiroho wenye mabawa.

- Ni viumbe wasio na matashi ya kimwili (kula, kunywa, kulala, n.k.)

- Hawana hiari katika kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w).

- Ni vimbe wasio na jinsia.

- Ni viumbe walioumbwa kutokana na Nuru.


 

  • Kazi za Malaika.

            Zifuatazo ni baadhi tu ya kazi za baadhi ya Malaika.

  1. Kuleta Wahyi (ujumbe) kwa wanaadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Malaika Jibril ndiye mhusika mkuu wa kupeleka wahyi kwa mitume na manabii.

Rejea Qur’an (81:19-20), (16:2) na (11:69-73).

 

  1. Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika amali zake nzuri na mbaya.

Kila mtu anakundi la malaika nyuma na mbele yake kumlinda na mambo yaliyo nje na uwezo wake. Pia kuna malaika wa kulia anayeandika mema na wa kushoto anayeandika maovu ya mtu.

Rejea Qur’an (82:1-12), (50:17-18) na (13:11).

 

  1. Kuwaombea Waumini maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Hawa ni malaika ambao huzunguka katika makundi ya waumini anapotajwa ndani yake Mwenyezi Mungu (s.w) au kusomwa Qur’an Tukufu.

Rejea Qur’an (40:7), (42:5) na (17:78).

 

  1. Kuwasaidia waumini katika vita vya kupambana na maadui wa Allah (s.w).

Pindi waumini wanapopigana katika kusimamisha haki, Mwenyezi Mungu (s.w) huteremsha malaika kuwasaidia.

Rejea Qur’an (3:123-126) na (8:12).

 

  1. Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia mipaka.

Watu waovu waliopindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) wakaonywa muda mrefu na wasionyeke huangamizwa na malaika maalum.

Rejea Qur’an (11:81-83).

 

  1. Kutoa roho za viumbe.

Malakul-Maut ndiye mhusika mkuu na wengineo katika kutoa roho za viumbe.

Rejea Qur’an (32:11).

 

  1. Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho za wafu kaburini.

Malaika wanaohusika na kazi hii ni Munkar na Nakir.

 

  1. Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama.

Mipulizo ya Parapanda katika kufisha na kufufua viumbe siku ya Qiyama itafanywa na malaika Israfil.

Rejea Qur’an (39:68).

 

  1. Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi.

Hili kundi jingine la malaika watakaofanya kazi hiyo siku ya Qiyama.

Rejea Qur’an (41:30-32) na (39:73).

 

  1. Kuwasimanga na kuwaadhibu watu waovu motoni.

Kuna kundi la malaika watakaokuwa wanaadhibu watu waovu motoni. Mlinzi mkuu wa milango ya moto ni Malaika Maalik.

Rejea Qur’an (25:22), (74:26-30) na (43:77).

 

  1. Kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w).

Kuna kundi la malaika maalum kwa kazi hii tu.

Rejea Qur’an (40:7).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Walio katika hatari ya kupata magonjwa ya ngono
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye liski ya kupata magonjwa ya ngono, ni watu wanaofanya mambo yanayosababisha kupata magonjwa ya ngono. Soma Zaidi...

image Maana ya kuamini malaika katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mikataba ya aqabah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu za kutokubalika kwa vitabu vilivyotumwa kuwa muongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu zama hizi
Soma Zaidi...

image Maana ya kusimamisha swala
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mtazamo wa makafiri juu ya dini
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kusimamisha swala za faradh katika nyakati za dharura.
Kipengele hichi tutajifunza namna ya kusimamisha swala ukiwa safarini na vitani na nguzo zake. Soma Zaidi...

image Kutoa vilivyo vizuri
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)..
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...