Kumuamini mwenyezi Mungu..

Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

  1. NGUZO ZA IMANI
    1. Kumuamini Mwenyezi Mungu (S.W).

Makafiri wa zamani na wa zama hizi wakiwemo Charles Darwin, Friedrich Engles, n.k wanadai kuwa imani ya uwepo wa Mungu Muumba dhana tu haina dalili yeyote. Miongoni mwa hoja (madai) zao wanazotoa ni hizi zifuatazo;

 

  1. Mwenyezi Mungu hayupo kwa sababu haonekani na wala hadirikiki kwenye milango ya fahamu. Rejea Qur’an (17:90-92). 

Milango ya fahamu kama vile macho katika kumuona, pua katika kumnusa,     masikio katika kumsikia, ngozi  katika kumhisi au kumgusa pia, n.k.

 

Udhaifu wa hoja hii,

Milango ya fahamu ina udhaifu mwingi sana na kikomo pia, kama vile macho au pua huweza kuona au kunusa vitu vilivyo karibu tu na visivyokuwa na kizuizi, kuna vitu vingi vinavyotuzunguka lakini hatuvioni kama upepo, sauti, n.k.

 

  1. Mwenyezi Mungu amefanywa kuwepo na wanadamu kutokana fikra na mawazo duni na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Hii ni baada ya mwanaadamu kushindwa kutatua matatizo katika mazingira yake na hivyo kuibukia kujiundia muingu.

 

Udhaifu wa hoja hii,

Historia inaonyesha kuwa hakuna zama mwanaadamu aliishi bila ya ujuzi wa kukabiliana na mazingira yake, Mwanaadamu wa kwanza kuumbwa alipewa ujuzi (elimu) ya kukabilana na mazingira yake na hatimaye kushushiwa muongozo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wake. 

Rejea Qur’an (2:31,38).


 

  1. Hapana Mungu Muumba bali vitu vyote vimetokana na mabadiliko ya kimaada.

Wanadai kuwa maumbile na viumbe vyote vinatokana na mabadiliko kidogo kidogo ya kimaada (evolution) baada ya muda mrefu kupita kutoka hali moja kwenda nyingine. Mfano binaadamu kutoka pweza, mjusi, sokwe na hatimaye mtu kamili.

   

Udhaifu wa hoja hii,

Nadharia hii haina ushahidi wowote wa kisayansi, kiuchunguzi na utafti bali ni dhana tu aliyoibuni Darwin ili kupotosha uhalisia na ukweli juu ya chanzo cha maumbile. Hadi leo hii hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuthibitisha nadharia hii.  

 

  1. Kama Mungu Muumba yupo, ni ipi nasaba (ukoo) yake au ametokana na nini?

Makafiri wa zamani na sasa wanasingizia kutoamini kuwepo Mungu kwa kuwa hawajui nasaba, ukoo au asili yake anatokana na nani au na nini.

       

Udhaifu wa hoja hii, 

Kwa kutumia mantiki, Muumba wa vitu vyote ndiye chanzo na asili ya vitu vyote.    Hivyo ni lazima asiwe na nasaba, mwanzo au mwisho pia. Na asitokane na vitu au maumbile yale.

Rejea Qur’an (112:1-4).

 

  1. Vitu havikuumbwa bali vimetokea kwa bahati nasibu (by chance) na vitatoweka kwa bahati nasibu pia muda wake ukifika.

Makafiri wa zamani na sasa wanadai kuwa asili ya maumbile yote yametokana na bahati nasibu (by chance), hivyo vitatoweka kama vilivyoibuka.

       

Udhaifu wa dai hili,

Hakuna uwezekano wa kuwepo maumbile bila ya Muumbaji na msimamizi mwenye ujuzi na uwezo wa hali ya juu na mtegemewa wa kila kitu, kwani  kila kitu kinachoonekana kimeumbwa na kimewekwa kwa lengo maalum.

 

Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa sababu zifuatazo;

Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo. 

Rejea Qur’an (4:165).

 

Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni kustahiki adhabu.

Rejea Qur’an (3:190), (30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).

 

Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe wao.

 

Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur’an kuwa faradhi ya kwanza kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa ardhini.

 

Tano, Maana ya neno “imani” ambalo lina maana ya ‘kuwa na yakini moyoni pasina shaka’ yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake. 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1581

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali

Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu?

Soma Zaidi...
Udhaifu wa mtazamo wa makafiri juu ya dini dhidi ya mtazamo wa uislamu

Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini

Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.

Soma Zaidi...
Elimu Yenye Manufaa

Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.

Soma Zaidi...
Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote

Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)

Soma Zaidi...
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu

Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu

Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?

Soma Zaidi...