image

Kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito faida na hasara zake

KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO

 

Hili ni swali ambalo wengi ya wajawazito wanajiulizaga. Kwa ufupi hakuna shida yeyote kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito, bila kujali hatua ya ujauzito. Unaweza kuzungumza na daktari kuhusu swala hili, ila usiwe na shaka kabisa. Tafiti zinaonyesha kuwa endapo mwanamke akifika kileleni akiwa katika ujauzito ni jambo jema kwa afya yake na afya ya mtoto na afya ya ujauzito. Najuwa maneno haya machache hayawezi kumaliza kiu ya maswali yako. Sasa hebu tuone mabo kadhaa.

 

1.Kwa baadhi ya wanawake wanapata maumivu wanaposhiriki tendo hili wakiwa wajawazito. Yes hii huweza kutokea kwani kzunguruko wa damu umeongezeka maeneo ya chini na kufanya maeneo hayo yawe na hisia nyingi sana. Hii inaweza kuleta hali ya kuumia kwa mjamzito wakati wa kuingia kwa uume. Wajitahidi wakati wa tendo hili kutumia muda mwingi kujiandaa, pia spidi upungue, na tendo lisifanyike kwa nguvu kama siku za kawaida.

 

2.Kuna baadhi ya wanawake wanajikuta uke wao umepunguza hali ya kubana yaani wanahisi unabwebwea. Ukweli ni kuwa kutokana na ongezeko la majimaji mwanamke anaweza kuhisi kuwa ule mnato na msuguano aliouzoea haupo. Hali hii inaweza kuwapunguzia hamu ya tendo baadhi ya wanawake.

 

3.Kwa baadhi ya wanawake majimaji yanakuwa mengi kiasi cha kuhisi kumkosesha raha mwenziwake. Hii hutokea baada ya msisimko kuzidi ama kwa sababu kuna mabdiliko ya homoni. Kama hali ni hii hakuna budi kuvumiliana.

 

4.Mkao wowte unaweza kutumika maadamu hautakandamiza tumbo la mama. Hapa wawe makini sana hasa ujauzito ukiwa mkubwa wasijelibana tumbo. Mkao wa ubavu ubavu na inayofanana na namna hiyo inaweza kuwa ni mizuri. Zungumza na daktari atakupa maelekezo vyema

 

5.Je kushiriki tendo kunaweza kusababisha ujauzito kutoka? Hapana si kweli kabisa. Ujauzito hauwezi kutoka eti kwa kushiriki tendo la ndoa.

 

6.Baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa mjamzito anaweza kuona damu ama kutokwa na damu. Hii pia sio tatizo. Ila kama itakuwa inatoka kwa wingi vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

 

7.Kwa baadhi ya wanwake inafikia wakati hahisi chochote anaposhiriki tendo na anakosa hamu kabisa ya kushiriki. Hili sio tatizo kubwa anaweza kumuona daktari kwa maelezo zaidi.

 

8.Kama atahisi dalili zifuatazo ni vyema kumuona daktari:A.Maumivu makali zaidi yasiyovumilikaB.Damu nyingiC.Kushindwa kupumuwa vyema





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2384


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mambo yanayopunguza nguvu za kiume
Posti hii inaelezea kuhusiana na nguvu za kiume zinavyopungua na Ni Mambo gani yanayofanya zipungue Soma Zaidi...

Madhara ya mwili kushindwa kutengeneza projestron ya kutosha
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo mtu anaweza kupata ikiwa mwili utaeweza kutengeneza progesterone ya kutosha. Soma Zaidi...

Dalili za saratani kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa Soma Zaidi...

Dalili za Utasa wa wanaume
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Utasa wa Mwanaume hutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume, utendakazi usio wa kawaida wa manii au kuziba kwa manii ambayo huzuia utoaji wa mbegu za kiume. Magonjwa, majeraha, matatizo ya kiafya sugu, u Soma Zaidi...

Samahani nauliza mjamzito akiwa na presha140/90 Kuna madhara?
Presha ya kupanda hypertension huweza kuzumbuwa watu kwa jinsia zote, na umri wote. Wajawazito pia wamekuwa wakisumbuliwa na presha hii mara kwa mara. Soma Zaidi...

mimi mara ya mwisho kubleed ilikuwa tareh 3/9 nilisex tarehe 4 je ni kwel nna mimba maana hadi sasa sijableed au ni kawaida tu
Je unaijuwa siku yako hatari ya kupata mimba. Na itakuwaje kama tayari umebeba mimba changa. Nakala hii inakwenda kukushauri machache kuhusu maswali haya. Soma Zaidi...

Sababu za za ugumba kwa Mwanaume
Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa Mwanaume, ni sababu ambazo umfanye mwanaume ashindwe kumpatia mwanamke mimba. Soma Zaidi...

dalili za mimba baada ya tendo la ndoa na changa ndani ya wiki moja
Utajifunza dalili za mwanzoni za mimba changa kuanzia wiki moja baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA: kumwaga mbegu mapema
Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika. Soma Zaidi...

Dalili za awali za mimba endapo tu mwanamke ametoka kukutana kimwili na mwanaume
Habari! Soma Zaidi...

Aina za uvimbe kwenye kizazi.
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za uvimbe kwenye kizazi, uvimbe unatokea kwenye kizazi ila utofautiana kulingana na sehemu ambazo uvimbe huo umepata. Soma Zaidi...

Maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Utajifunza sababu za kuweo kwa maumivu ya uume wbaada ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa. Soma Zaidi...