KUSIMAMISHA SWALA ZA FARADH KATIKA NYAKATI ZA DHARURA.


image


Kipengele hichi tutajifunza namna ya kusimamisha swala ukiwa safarini na vitani na nguzo zake.


6.4.Kusimamisha Swala za Faradh katika nyakati za Dharura.

-   Swala imepangiwa muda maalumu, isiswaliwe nje ya muda wake ila kwa udhuru wa kisheria.

-   Hapana ‘kadha’ (kulipa swala) au kuswali swala nje ya wakati wake bila dharura kisheria.

     Rejea Qur’an (4:103), (2:286), (2:185), (5:6).

 

  • Swala ya Mgonjwa
  1. Ameruhusiwa kutayammamu iwapo hawezi kutumia maji.

      Rejea Qur’an (4:43) na (5:6).

 

2. Kama mgonjwa hajimudu kujitwaharisha kwa maji au tayammamu na hana mtu wa kumsaidia, basi atatayammamu kwa ishara na kuswali kwa ishara (kifikra) pia.

      Rejea Qur’an (5:6).

 

3. Mgonjwa anaruhusiwa kuswali akiwa amekaa na kuelekea Qibla kama anaweza, na atarukuu na kusujudu kwa kukaa au kwa ishara jinsi atakavyoweza.

 

4. Iwapo hawezi kukaa basi ataswali akiwa amelala kwa ubavu akiwa ameelekea Qibla kama anaweza, vinginevyo ataelekea popote na kulala chali au kulala vyovyote awezavyo.

 

5. Mgonjwa anaruhusiwa kuchanganya swala na kuzifupisha kama msafiri kulingana na hali ya ugonjwa na mazingira yake.

  • Swala ya Msafiri

-     Muislamu akiwa safarini anawajibika kutekeleza swala kama ifuatavyo;

      Rejea Qur’an (5:6), (4:101) na (2:238-239).

  1. Anaruhusiwa kutayammamu kama maji yatakosekana au hakuna uwezekano wa kuyatumia ndani ya kipando. Kutayammamu kunafaa kwa kutumia ukuta wa chombo cha usafiri pia.

 

2. Anaruhusiwa kupunguza swala zenye rakaa 4 na kuswali rakaa mbili mbili ambazo ni Adhuhuri, Alasir na Ishaa tu.

 

3. Pia msafiri ameruhusiwa kuunganisha swala 2, Adhuhur na Alasir, Magh’rib na Ishaa tu kwa kuziswali muda mmoja, kwa kuzitanguliza muda wa swala ya mwanzo (Jamu’ Taq’diim) au kuzichelewesha na kuziswali muda wa swala inayofuata (Jamu’ Ta’akhiir)

 

4. Pia msafiri anaruhusiwa kuswali huku akiwa anatembea au anaendelea na safari kwenye kipando chake.

 

  • Kusimamisha Swala Vitani

Kusimamisha swala ya faradh katika uwanja wa vita ni kama ifuatavyo;

Rejea Qur’an (4:102-103).

 

-     Askari wagawanyike katika makundi mawili, ambayo yataswalishwa jamaa na imamu mmoja.

 

-     Swala itafupishwa kama ilivyo katika swala ya safari, kwa kuswaliwa rakaa mbili yenye rakaa 4.

 

-     Kundi moja litaanza kuswali na imamu likiwa na silaha zao na jingine likiwa katika ulinzi.

 

-     Imamu ataswali rakaa moja ya mwanzo na kundi la mwanzo, na watakaponyanyuka rakaa ya pili, kila askari atamalizia rakaa ya pili kivyake haraka na baada ya kutoa salaam atarudi kuchukua nafasi ya ulinzi.

 

-     Imamu atabakia amesimama katika rakaa ya pili mpaka kundi la pili litakapounga jamaa nyuma yake ndipo ataendelea kumalizia rakaa yake ya pili.

 

-     Imamu atakapomaliza rakaa ya pili atatoa salaam na kila askari atasimama na kivyake kumalizia rakaa ya pili haraka na kutoa salaam pia.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mwenendo wa mwenye kunuia hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maadui wakubwa wa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Aina za hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Funga za Sunnah na namna ya kuzitekeleza
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...

image Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

image Maswali juu ya dini anayostahiki kufuata mwanadamu
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat
Nguzo za uislamu, masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Udhaifu wa mtazamo wa makafiri juu ya dini dhidi ya mtazamo wa uislamu
Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Madhumuni ya dola ya uislamu
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...