image

Kuzika-namna ya kuzika hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Kuzika.

 

-    Waislamu (watu) wataongozana nayo mpaka kaburini kimya kimya.

-    Jeneza lisitanguliwe na watu (msafara).

-    Haitakiwi watu kukaa kabla ya jeneza kukalishwa chini.

 

-    Kaburi liwe pana na kina cha kutosha, mtu kuweza kusimama na kunyoosha mkono kama kuna uwezekano.

-    Kisha lichimbwe shimo dogo (mwana ndani) upande wa Qibla ndani ya kaburi.

-    Urefu na ukubwa wa kaburi unategemea na ukubwa wa maiti.

 

  1. Waingie watu kaburini kwa idadi ya witiri; 3, 5, 7, n.k.
  2. Jeneza liwekwe upande wa kaburi itakapokuwa miguu ya maiti.
  3. Maiti itolewe na kutanguliza kichwa kuelekea kaburini.
  4. Wapokeaji kaburini watamuweka magotini mwao ili kufungua kamba kichwani, tumboni na miguuni. Pia watafunua shavu la kulia ili liguse ardhini (mchanga) atakapolazwa ndani ya mwana-ndani.

 

  1. Maiti italazwa katika mwana-ndani kwa ubavu wa kulia na kuelekezwa Qibla. Wakati wa kuilaza ni sunnah kusema, 

Kama ilivyosimuliwa na Ibn Umar (r.a) kuwa, Mtume (s.a.w) alipokuwa akizika alikuwa akisema: 

        “Bismillaah wabilahi wa’alaa millati Rasuulullaahi”         

        Tafsiri:

“Kwa jina la Allah na kwa uwezo wa Allah na kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume wa Allah.” (Ahmad, Tirmidh, Ibn Majah).

 

  1. Maiti ipindishwe miguuni na kichwani ili uso na miguu iweze kugusa kuta za mwana-ndani. Kifua, tumbo na sehemu za katikati zibinuliwe nyuma kidogo.

 

  1. Maiti iwekewe mawe au udongo nyuma ya kichwa na miguu isibinuke. Pia ni sunnah kusoma aya za Qur’an (2:1-5) au (2:285-286).

 

  1. Baada ya maiti kulazwa na kusomewa aya hizi, ifunikwe kwa ubao na kama kuna matundu ya kupitisha udongo pazibwe kwa majani.

 

  1. Kabla kaburi halijafunikwa, vitupiwe viganja vitatu vya udongo, na kila tupo unasoma aya ya Qur’an (20:55).

                      (katika ardhi) tutakutoweni mara nyingine.

 

  1. Kaburi lijazwe udongo mpaka lijae na kuinuliwa kiasi cha shiburi moja na kuwekewa alama miguuni na kichwani au kupanda miti mibichi.

-  Ni vizuri kumiminia maji juu yake ili kuepusha vumbi kupeperushwa na upepo.  

- Ni haramu kujengea kaburi kwa namna yeyote ile, kukaa juu   yake, kuwasha taa

   juu yake na kuielekea wakati wa kuswali.

‘Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza kuyajengea makaburi   au kuyajengea nyumba juu yake au kukaa juu yake’. (Muslim)

 

Abu Marsad Al-ghafariyyi ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 

     “Msikae juu ya makaburi na wala msiswali kwa kuyaelekea.” 

                    (Muslim)

 

        -  Baada ya kuzika Mtume (s.a.w) alikuwa akisimama na kusema: 

            “Muombeeni msamaha ndugu yenu na muombeeni awe

                na kauli thabiti kwani sasa anaulizwa”

 

        -  Ni sunnah baada ya mazishi kuwapa mikono wafiwa na kuwausia subira

            Rejea Qur’an (2:155-156).

        -  Pia haifai kusema (kusengenya) mabaya ya marehemu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1255


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Lengo la kusimamisha swala kwa mwanadamu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la kusimamisha swala. Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Soma Zaidi...

Maswali juu ya haki na uadilifu katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Aina za swala..
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mambo anayofanyiwa mtu anayekaribia kufa
Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut Soma Zaidi...

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu
Soma Zaidi...

Mifano na namna ya kurithisha
Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi. Soma Zaidi...

Ni watu gani wanaopewa Zaka
Soma Zaidi...

Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...

Kumkafini (kumvisha sanda maiti)
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...