KWANINI LENGO LA ZAKAT NA SADAQAT HALIFIKIWI KATIKA JAMII YETU


image


Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)


Kwa nini lengo la Zakat na Sadaka halifikiwi katika jamii yetu?


Pamoja na zakat na sadaka kutolewa na baadhi ya waislamu lakini malengo yake hayafikiwi, zifuatazo ni baadhi ya sababu;

1. Wengi watoao zakat na sadakat hawajui lengo lake halisi.
2. Waislamu wengi wanatoa zaka na sadaka kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio utakaso.
3. Waislamu wengi hawatoi zakat kabisa.
4. Waislamu wengi licha ya kuwa na mali na uwezo wa kutoa zakat na sadaka lakini hawatekelezi au kuhimiza wengine katika kutoa mali zao pia. Rejea Quran (2:2-3).
5. Wengi watoao zakat na sadakat hawatekelezi masharti ya utoaji.
6. Pamoja na matajiri wachache kutoa zakat na sadaka, lakini bado hutoa kwa ria, masimbulizi, adha na kuleta uadui na fitna katika jamii. Rejea Quran (2:264).
7. Zakat na sadaka haikusanywi na kugawanywa kijamii.
8. Utoaji na ugawaji wa zakat na sadaka umekuwa unafanywa kila mtu kivyake, bila mpango maalumu wa kukusanya na kugawa kwa wanaostahiki.
9. Wengi watoao zakat na sadakat chumo lao ni la haramu.
10. Ingawa waislamu wengi hutoa zakat na sadaka, lakini lengo na matunda yake hayafikiwi kutokana na chumo lao kuwa haramu.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Aina za tawafu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Funga za Sunnah na namna ya kuzitekeleza
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Tofauti kati ya hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kukusanywa na kuhifadhiwa kwa quran
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Fiqh.
Kipengele hichi tutajifunza chimbuko la fiqh na maana ya figh. Soma Zaidi...

image Sifa au vigezo vya dini sahihi
Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...