image

Kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi

Somo Hili linakwenda kukueleza sababu za kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi

KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)

? Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika. Na mradhi mengine kama malaria na homa ya bonde la ufa. Lakini kuna jambo linaumiza sana fikra za wasomaji. “kama mbu wanaweza kuambukiza maradhi hayo ya virusi, sasa ni kwa nini mbu hawezi kuambukiza HIV?”

? Kwa hakika swali hili linasumbua fikra za watu wengi sana. Tafiti nyingi za kisayansi zimefanywa ili kuthibitisha majibu sahihi na kuwaridhisha waulizaji. Ukweli ni kuwa mbu katu hawezi kueneza HIV. Na huu ni ukweli ambao haupingiki katu, lakini sasa ni kivipi?. katika makala hii nitakueleza jibu la swali hili katika namna tatu:-

? Mdomo wa mbu una sehemu kuu 6, katika hizo 6 nne hutumika kutoboa ngozi ya mwili wa kiumbe anachotaka kunyonya damu. Na sehemu 2 zilizobakia ni kwa ajili ya kunyonya damu. Katika sehemu 2 hizo mojawapo ni kunyonya damu na nyingine ni kupeleka mate kutoka kwenye mwili wa mbu na kuelekea kwenye mwili wa kiumbe kinachonyonywa damu. Mate haya hutumika kwa kuifanya damu isigande.

? Hivyo basi kitu ambacho kinatoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu ni mate ya mbu tu, na si damu, kwani damu haiwezi kutoka kutoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa. Tafiti zinaonesha kuwa mate kati hayawezi kuambukiza ukimwi, hata yawe ya mtu. Hivyo basi hata kama mate ya mbu yataingia kwa mbu kati hayawezi kuambukiza ukimwi kkama amebeba virusi.

? Virusi vya HIV vikifika mwilini mwa mbu vinaliwa na kupotea kabisa. Virusi vya HIV ili viendelee kuzaliana vinahitaji kupata T seli (T cell), lakini mbu hana seli aina hii. Hivyo virusi vinapofika kwa mbu, vinaliwa pamoja na damu na kupotea kabisa. Kwa sababu hii hakuna uwezekano wa virusi vya HIV kuingia kwenye mate ya mbu ambayo ndio huenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu. Hii inaonyesha kuwa katu HIV haiwezi kusambazwa kwa mbu.

? hata kama virusi vya HIV vitaweza kuingia kutoka kwa mbu kwenda kwa kiume kinachonyonywa damu (japo jambo hili haliwezekani) hakua uwezekano wa kuambukiza HIV. Tafititi zinaonyesha kuwa ili damu ama mate ya mbu yasambaze HIV inahitajika ang’ate si chini ya mara milioni 10. Jambo hili kisayansi haliwezekani. Pia kummeza mbu aliyebeba HIV HAIWEZEKANI KUSAMBAZA HIV. Haka akipasukia kwenye jeraha la mtu katu damu yake haiwezi kuambukiza HIV.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-29     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 812


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Maana ya afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya afya Soma Zaidi...

Athari za mkojo mwilini.
Posti hii inahusu zaidi athari za mkojo mwilini, kwa kawaida tunafahamu kwamba mkojo ni matokeo ya mkusanyiko wa uchafu wa maji maji yanayokusanyika kutoka mwilini ikiwa mkojo umebaki mwilini usababisha madhara mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Roghage/ vyakula vya kambakamba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya roghage Soma Zaidi...

Huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizu Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kupanda
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kupanda Soma Zaidi...

Imani potofu juu ya chanjo.
Post hii inahusu zaidi Imani potofu juu ya chanjo kwa watoto na akina Mama, ni baadhi ya Imani waliyonayo watu juu ya chanjo. Soma Zaidi...

Huduma ya kwanza kwa mwenye uchafu kwenye sikio.
Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio. Soma Zaidi...

Nini husababisha kizunguzungu?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu Soma Zaidi...

Zijuwe athari za vidonda mwilini
Posti hii inahusu zaidi athari za kutotibu vidonda, hizi ni athari mbalimbali ambazo zinaweza kutokea ingawa kama vidonge haujatibiwa au vimetibiwa kwa kuchelewa. Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya mwili.
Posti hii inahusu zaidi sababu ya kuwepo kwa maumivu ya mwili kwa sababu tunaweza kuhisi maumivu kwenye sehemu za mwili kwa sababu mbalimbali kama tutakavyoona hapo chini Soma Zaidi...

Zijue dalili za upungufu wa maji mwilini
Posti hii inaelezea kuhusiana na upungufu wa maji mwilini Soma Zaidi...