Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Kwa nini mwanaadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mwanaadamu yeyote hawezi kuishi bila ya dini hata kama atadai kuwa hana dini kwa sababu zifuatazo;
Maana halisi ya dini.
Dini ni utaratibu wa maisha anaofuata mwanaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku kibinafsi na kijamii.
Umbile la mwanaadamu ni la kidini.
Umbile la mwanaadamu limefungamana na kanuni na sheria za maumbile yote yanayomzunguka.
Rejea Quran (30:30), (3:83).
Vipawa alivyotunukiwa mwanaadamu.
Tofauti na wanyama na viumbe wengine, mwanaadamu ametunukiwa vipawa vya ziada vifuatavyo;
Akili na Ufahamu wa hali ya juu.
Vinamsaidia kufikiri na kutafakari mambo yanayomhusu yeye mwenyewe na mazingira yanayomzunguka.
Utambuzi binafsi (self-consciousness).
Humuwezesha kuhusianisha yeye na mazingira (viumbe) yanayomzunguka.
Uwezo wa kujielimisha na kuelimika.
Elimu ni nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuyamudu mazingira kwa ufanisi.
Uhuru wa kufanya atakalo.
Mwanaadamu amepewa vipaji, elimu na ujuzi, ilivimuwezeshe kubainisha njia sahihi ya kufuata katika maisha yake ya kila siku.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 web hosting 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Lengo la kuletwa mitume
Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere..
Soma Zaidi...Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).
Soma Zaidi...(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini
Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.
Soma Zaidi...Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele).
Soma Zaidi...KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.
Soma Zaidi...