Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Lengo la Funga linavyofikiwa.
Lengo kuu la funga ni kumuandaa mja (muislamu) kuwa mcha-Mungu (2:183). Na lengo hili hufikiwa kama ifuatavyo;
Funga humzidishia mfungaji imani na uadilifu.
Kufunga ni ibada ya siri, anayejua ni mfungaji na Muumba wake tu, hivyo hufunga ili apate radhi na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Funga humzidishia mja nidhamu na utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Mja akiwa amefunga huwa mtiifu kwa kufuata amri na kuacha makatazo ya Mwenyezi Mungu na kuchunga vilivyo masharti na nguzo zote za funga.
Rejea Quran (2:168) na (2:172).
Funga humzoesha mja kudhibiti matashi ya nafsi na kimwili.
Funga humuepusha mja na tabia za kinyama kama kula, kunywa, kujamii bila sababu ya msingi, na kumjenga kiroho na kiutu ili kuwa na hadhi yake.
Rejea Quran (25:43-44) na (2:30-31).
Funga humuwezesha mja kuwahurumia wanaadamu wenzake.
Funga hujenga huruma na mapenzi kwa kule mfungaji kukaa na njaa na adha yake, hivyo hujifunza kuwahurumia wasiokuwa nacho na wenye matatizo.
(34:12-13) na (49:13).
Funga humpatia mfungaji afya (siha).
Kwa mfungaji kukaa na njaa muda mrefu, huuwezesha mwili kupumzika na kuondoa malimbilkizo ya vyakula tumboni ambayo ni sumu kwake.
Funga huwafanya Waislamu kuwa Ummah mmoja.
Hii ni kwa sababu funga imefaradhishwa kwa waislamu wa rika na jinsia zote, maskini na matajiri pia, wote hutekeleza amri hii bila ubaguzi wowote.
Rejea Quran (49:13).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJifunze mengi kuhusu dini hapa
Soma Zaidi...Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Katika kipengele hiki tutajifunza nguzo za uislamu.aina tano za nguzo za uislamu,dhana ya nguzo za uislamu,lengo na umuhimu wa nguzo za uislamu
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha.
Soma Zaidi...