Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu lishe salama kwa mjamzito
LISHE SALAMA KWA MJAMZITO:Kwa ufupi ni kuwa mjamzito na anayenyonyesha wanatakiwa wapewe lishe kamili iliyokuwa na virutubisho vyote. Haata hivyo ni vyema kuzingatia nukuu za hapo chini. Wanaonyonyesha na wajawazito wanahitaji kupata vyakula vyenye viinilishe vya kutosha ili kuwezesha ukuaji wa mtoto tumboni , utengenezwaji wa maziwa na kwa ajili ya afya zao wenyewe.
Vyakula vya protini vinahitajika kwa mkiwango kikubwa ili kuwezesha mwili wa mama kujenga misuli vizuri , tishu katika mwili wake na mwili wa mtoto aliye tumboni. Utengenezwaji wa maziwa , usafirishwaji wa damu na ukuaji wa viungo vya mama na mtoto unahitaji protini. Hivyo wamama hawa wapewe protini kwa wingi.vyakula vya protini ni kama:-A.NyamaB.MayaiC.MaharagweD.SamakiE.MaziwaF.Pia kwenye nafaka na baadhi ya mboga za majani na matunda.
Vyakila vya folic asid na vitamini B vinahitajika kwa ajili ya kuwezesha kupunguza tatizo la kushindwa kujifunguwa kwa njia ya kawaida. Vyakula vya madini ya kashiam(calcium) ni muhimu kwa ukuwji wa mifupa ya mtoto aliye tumboni na kuimarika mwili wa mama pia. Kwani mjamzito asipopewa madini haya mtoto atatumia madini yaliyomo kwa mama na kumfanya mama awe na mifupa dhaifu katika kipindi hiki.
Madini ya chuma ni muhimu katika utengenezwaji wa damu, halikadhalika mtoto anahitaji madini haya ili ayatumie katika wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Madini ya zink ni muhimu katika kuwezesha kujifunguwa.(progression of labour) na ukuaji salama wa mtoto aliyoko tumboni.
Wamama wajawazito wapewe vyakula vyenye kambakamba (dietary fiber}. Hivi vitamuwezesha kutopata tatizo la kukosa choo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1400
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitau cha Fiqh
Faida za kiafya za kula Maini
Soma Zaidi...
UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula karanga
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...
Vitamini na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi vitamini mbalimbali na kazi zake kwenye mwili,vitamini ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama ifuayavyo. Soma Zaidi...
Nini maana ya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini Soma Zaidi...
Faida za kula Papai
Okoa afya yako kwa kula tunda papai, kwa hakika hutajuta, papai lina virutubisho vingi Soma Zaidi...
Chungwa (orange)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula chungwa/orange Soma Zaidi...
Fahamu vitamini K na kazi zake, vyakula vya vitamini k na athari za upungufu wake
kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini. Soma Zaidi...
KITABU HA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...
Vyakula vya protini na kazi zake
Hapa utajifunza kuhusu kazi za protini mwilini na vyakula vipi vina protini kwa wingi Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Mihogo
Soma Zaidi...
Vyakula vilivyo hatari kwa afya ya meno
Vyakula hivi vinaweza kuwa na hatai kwenye afya ya meno ama kuharibu kabisa meno. Soma Zaidi...