picha

Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke

Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi.

Zifuatazo Ni Dalili za Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke PID.

Mwanamke atakundulika kuwa na PID Kama akiwa na Dalili zifuatazo;

1.maumivu makali ya tumbo hasa chini ya kitovu. Kutokana na Maambukizi yaliyoenda kuathiri via vya Uzazi .

 

2.kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu ya rangi ya maziwa mgando. Uchafu huu hutokana na bacteria ambao hushambulia sehemu za shingo ya uzazi, nyuma ya mfuko wa Uzazi, na mirija ya uzazi na ndio maana hupelekea kutoa uchafu.

 

3.kupata homa za Mara kwa Mara. Kwasababu ya Maambukizi hayo yaliyoenda kuathiri kwenye Uzazi wa mwanamke pamoja na maumivu hupelekea kupata homa za Mara kwa mara.

 

4.kupata Hali ya kichefuchefu au kutapika. Hii Ni kwasababu mwanamke anaweza kukosa hedhi au hedhi kujirudia kwa mwezi pamoja na uchafu unayotengenezwa na hao bacteria hupelekea kupata kichefuchefu au kutapika.

 

5.kupata maumivu wakati wa kukojoa. Maambukizi haya hufanya sehemu hizo kuwa na michubuko hivyo husababisha mtu akikojoa kupata maumivu.

 

6.kutokwa na Damu wakati wa kujamiina. Damu hizi hutoka pia kwa sababu ya michubuko iliyotokea Ndani na ndio maana akijamiina anaweza Kutokwa na Damu.

 

7.kupata maumivu ya mgongo. Ni kwasababu ya Maambukizi yanayoathiri via vya Uzazi Kama shingo ya uzazi, nyuma ya mfuko wa Uzazi, na mirija ya uzazi ndio hupelekea kupata maumivu ya mgongo.

 

8.kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa au kujamiina.hii pia Ni kwasababu ya michubuko iliyotokea Ndani na iliyosababisha na Mashambulizi ya bacteria hao.

 

9.wakati mwingine Kutokwa na usaha ukeni. Uchafu ukizid na Hali hii hupelekea kutoa usaha kwa sababu ya kukosa matibabu na kukaa na Ugonjwa huu kwa muda mrefu.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/01/13/Thursday - 11:44:46 am Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 1661

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 web hosting    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Dalili za kujifungua hatua kwa hatua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa

Soma Zaidi...
Dalili za ongezeko la homoni ya estrogen

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi.

Soma Zaidi...
Kazi ya metronidazole

Posti hii zaidi kazi ya Dawa ya metronidazole katika kutibu Minyoo, ni aina ya Dawa ambayo imetumiwa na watu wengi wakaweza kupona na kuepukana na minyoo. Zifuatazo ni baadhi ya kazi za metronidazole.

Soma Zaidi...
Sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

Posti hii inahusu zaidi sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hili ni tatizo ambalo uwapata akina Mama wengi wanapomaliza kujifungua kwa hiyo tutaweza kuziona sababu zinazosababishwa na tatizo hili.

Soma Zaidi...
Malengo kwa Akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba.

Posti hii inahusu zaidi malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, ni malengo ambayo yametolewa ili kuweza kusaidia mtoto azaliwe vizuri na mambo mengine kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Mambo ambayo mama anapaswa kujua akiwa mjamzito

Posti hii inahusu zaidi mambo anyopaswa kujua akiwa mjamzito. Ni mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama akiwa mjamzito.

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kulia

Soma Zaidi...