Maana ya kuamini malaika katika maisha ya kila siku

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Zifuatazo ni athari za muumini wa kweli juu ya imani ya malaika katika kila kipengele cha maisha ya kila siku;

 

Kwanza, imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na viumbe wake hasa wale wasioonekana kama Malaika, majini, n.k.

Rejea Qur’an (37:149-154), (43:16-19) na (21:26-27).

 

Pili, imani juu ya malaika huchochea mja kufanya ibada kwa bidii na kujiepusha na maovu na machafu ili kupata cheo kama malaika au zaidi. 

 

Tatu, imani juu ya malaika pia humfanya mtu kuepuka kufanya maovu popote alipo na muda wowote kwa kujua kuwa yupo pamoja na malaika.

 

Nne, Mja anapoamini kuwa malaika huandika na kuhudhurisha vitendo vyake kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kufanya mema zaidi na kuepuka maovu kadri ya uwezo wake.

 

Tano, Muumini anapoamini kuwa malaika humuombea maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kuzidisha mema na kuepuka maovu kadri awezavyo ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu (s.w) zaidi.

Rejea Qur’an (17:13-14) na (18:49).Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/15/Saturday - 07:46:47 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1689


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Tanzu (makundi) za hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Je, mtu anaweza kusoma quran akiwa amelala?
Kusoma Qur'an kuna faida kubwa kwa Muislamu, kwanza kunampatia thawabu, kunatoa nuru maisha yake, mwili wake na kumlinda na mashetani na watu wabaya. Quran ni dawa na pozo kwa magonjwa. Thawabu za Qur-an hulipwa kwa kila herufi. Quran pia huja kutet Soma Zaidi...

Maana ya zakat
Nguzo za uislamu,kutoa zakat na sadaqat (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Aina za tawafu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...

Maana ya muislamu.
Kwenye kipengele hichi tutajifunza ni nani muislamu. Soma Zaidi...

Mafunzo kutokana na vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hatua za Kuzuia Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na mirija ya uzazi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na hatua za kujikinga na Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na kwenye mirija ya uzazi Soma Zaidi...

Kuchimbwa upya kwa kisima cha Zamzam
Sura na historia ya mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 3.Hapa utajifunza kuhusu kufukuliwa kwa kisima cha Zamzam baada ya kufukiwa muda mrefu. Soma Zaidi...

Kusimamisha swala.
Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala. Soma Zaidi...