MAANA YA MIRATHI KATIKA UISLAMU


image


Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake.


Maana ya Mirathi
Mirathi katika Uislamu ni kanuni na taratibu alizoziweka Allah (Sw) katika kuwagawawia na kuwarithisha familia na jamaa, mali aliyoiacha marehemu. Qur'an inabainisha kuwa, mtu anapofariki dunia, mali yote aliyochuma hurithiwa na Allah (Sw), kisha Yeye huigawa na kuwarithisha watu wanaostahiki, katika uwiano wa haki na uadilifu.ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu na subirini. Ardhi ni ya Mwenyezi Mungu, anamrithisha amtakaye katika waja wake; na mwisho (mwema) ni kwa wamchao. (7:128)

 

na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu (5 7:10) Ukweli huu unajitokeza pia katika dua ya nabii Zakaria alipomuamba Allah (Sw) amjaalie mtoto. Nabii Zakaria alimwomba Mola wake akasema: Mola wangu! Usiniache peke yangu na Wewe ndiwe mbora wa wanaorithi (21:89)

 


Mwanamke ana haki ya kurithi
Katika kugawanya na kuirithisha mali kwa wahusika, Allah (Sw) hakumnyima mwanamke haki ya kurithi akiwa mtoto, mke au mama. Wote wanawake na wanaume wanamafungu maalumu Ia kurithi katika mali aliyoiacha marehemu.

 

"Wanaume wana sehemu katika mali wanayoyachuma wazazi na jamaa walio karibu. Na wanawake (pia) wanayo sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa walio karibu. Yakiwa kidogo au mengi. (Hizi) ni sehemu zilizofaradhishwa (na Allah (s.w))" (4:7)

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake. Soma Zaidi...