Post hii itakufundisha maana ya neno sunnah katika Uislamu. Pia utajifunza maana ya neno hadithi katika uislamu
Maana ya Sunnah:
Kilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Hivyo ukisema "Sunnat Muhammad (s.a.w)" ina maana ya mwenendo au tabia au mila aliyokuwa akiifuata Mtume Muhammad (s.a.w) katika maisha yake ya kila siku. Na ikisemwa, "Sunnatullah" kama ilivyotumika katika Quran, ina maana ya desturi au kawaida au mila ya Allah (s.w) katika kufanya mambo ya Uungu wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: “Hii ni kawaida (sunnah) ya Allah (ya kuwaadhibu wakorofi) iliyokuwa kwa waliopita zamani, hutapata mabadiliko katika kawaida (sunnah) ya Allah." (33:62).
Kisheria, sunnah ni mwenendo au matendo ya Mtume (s.a.w) ambayo ni sehemu ya Utume wake. Waislamu wanalazimika kuyaiga na kuyafuata katika uendeshaji wa maisha yao ya kila siku ili kupata radhi za Allah (s.w). Mwenendo wa Mtume (s.a.w) haukutokana na matashi yake bali ulikuwa ni wahyi kutoka kwa Allah (s.w) kama inavyothibitika katika Qur-an: “Na hazungumzi (Muhammad) kwa matamanio ya nafsi yake.Isipokuwa (anayozungumza ni) wahyi uliofunuliwa kwake." (53:3-4)
Kiutendaji, sunnah ya Mtume (s.a.w) ni yale matendo ya msingi aliyoyafanya, aliyoyaagiza na yaliyofanywa mbele yake asiyakemee au kuyakataza.
Maana ya Hadith:
Kilugha: maana ya Hadith katika lugha ya Kiarabu ni jambo jipya au kitu kipya", hutuba, taarifa, maelezo au mapokezi. Katika Qur-an neno "Hadith" limetumiwa kwa maana hizi kama ilivyo katika aya ifuatayo: Basi simulizi gani baada ya hizi (simulizi za Qur-an) wataziamini?" (77:50) Kisheria, Hadith za Mtume (s.a.w) ni simulizi (mapokeo) au taarifa juu ya yale yote aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuufundisha Uislamu kinadharia na kimatendo au juu ya yale yaliyotendwa mbele yake akayakataza au akayaridhia au maelezo juu ya mwenendo na tabia ya Mtume (s.a.w). Ifuatayo ni mifano ya Hadith za Mtume (s.a.w):
(i)Maelezo au maelekezo ya Mtume (s.a.w)
Amesema Mtume (s.a.w) "Mwenye kumueleza mwenzake jambo la kheri anapata malipo sawa na mtendaji wa kheri hiyo."
(ii)Vitendo vya Mtume (s.a.w).
Amesema Bibi Aysha (r.a): "Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali swala ya Dhuha rakaa nne na mara nyingine huzidisha atakazo."
(iii) Kukubali (kuridhia)
Amesema Bibi Aysha (r.a): "Mtume (s.a.w) aliwapeleka askari kwenye vita, kiongozi wao alikuwa akipendelea sana kusoma suratul- Ikhlasi katika swala. Waliporejea waliripoti kwa Mtume (s.a.w) jinsi Imamu wao alivyokuwa anafanya, Mtume (s.a.w) akasema: "Muulizeni kwanini alifanya hivyo." Wakamuuliza naye akajibu kwamba suratul- Ikhlas ni sifa za Mwenyezi Mungu na yeye anapenda kuzisema. Mtume (s.a.w) akasema: "Mwambieni kwamba na yeye Mwenyezi Mungu anampenda."
(iv) Sifa au Mwenendo wa Mtume (s.a.w)
"Amesema Sayidna Ali (r.a), Mtume (s.a.w) alikuwa mwenye elimu, mpole na mkarimu. Mwenye kumuona Mtume (s.a.w) huvutiwa naye na kumfuata."
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1505
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
DUA ZA KUONDOA WASIWASI
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Soma Zaidi...
kujiepusha na uongo na sifa za uongo
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Soma Zaidi...
Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 6: ubainifu wa halali na haramu
Post hii inakwenda kukupa tahadhari juu ya mambo ya halali na mambo ya haramu. Soma Zaidi...
Al-Arba uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 7: Nasaha katika dini
Post hii itakufundisha umuhimu wa nasaha katika dini Soma Zaidi...
MAANA NA FADHILA ZA KUOMBA DUA
DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Soma Zaidi...
hadithi ya 8
عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى ?... Soma Zaidi...
ADHKAR NA DUA
ADHKARI MBALIMBALI NA DUA Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari. Soma Zaidi...
HADITHI 40 ZA IMAM NAWAW AROBAIN AN-NAWAWIY
Soma Zaidi...
NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA. Soma Zaidi...
WACHA KILE ULICHO NA SHAKA NACHO NA FANYA USICHO NA SHAKA NACHO
عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ الْحَسَنِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ سِبْطِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم وَرَيْحَانَتِهِ رَضِيَ اللَ... Soma Zaidi...
ZIJUWE NAMNA ZA KUZUIA HASIRA, NA MADHARA YA HASIRA
28. Soma Zaidi...