picha

Maana ya legacy contact katika Facebook

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya legacy contact katika facebook

NINI MAANA YA LEGACY CONTACT KATIKA FACEBOOK?

Facebook hawana mpango wa kufunga akaunti ambazo hazijatumiwa kwa muda mrefu, haijalishi akaunti ni ya marehemu ama yupo hai. Kama hutaki akaunti yako ya facebook kuna njia moja tu nayo ni kuifuta. Hata hivyo mchakato huu inachukuwa kuanzia siku 114 yaani siku 14 za akaunti kuwa haipo active na aiku 90 za kuthibitisha kufuta akaunti hii.

 

Kwa waliofariki akaunti zao zitabakia milele ama mpaka facebook wakibadili sera ya kutofunga akaunti zilizotumika. Wakati mwingine akaunti za waliofariki zinatumiwa vibaya, hivyo unaweza kuchagua nini kifanyike utakapo fariki, aidha akaunti yako ifungwe ama ibakie kama ya kumbukumbu.

 

Kufanya haya yote mawili unatakiwa umchague mtu atakayefanya haya. Na mtu huyu itamchagua ukiwa hai. Mtu huyu anatambulika kama LEGACY CONTACT. Legacy contact ni friend kwenye akaunti yako ya facebook ambaye imemchagua kuwa ndiye utampa madaraka ya kuweza kuomba akaunti yako ya facebook ifungwe pindi utakapo fariki, ama akaunti yako iwe ni akaunti ya kumbukumbu yaani memorization account.

 

Mtu huyu hataweza kulog in kwenye akaunti yako. Yaani hataweza kuona taarifa zako za siri hata moja. Yeye atakuwa na madaraka kama:

1. Kuomba akaunti yako ifungwe ama iwe ya kumbukumbu2. Kubadili profile picture ama profile cover picture.3 .Kukubali friends request chache kutoka katika watu wa familia4. kuzuia ni picha zipi ziweze kuonea na ni nani aweze kuziona5. kuzuia watu wasidownload picha zako ana kama utamruhusu kupitia legacy ataweza kudownload yeye tu.6. kuondoa tag kama kuna mtu amekutag

 

Memorization accountKama legacy wako ameomba akaunti yako isifungwe bali iwe memorization account basi itakuwa na sifa hizi

1. Haitaonekana kwenye ukurasa mkuu wa facebook

2. hata mtu akisach jina halitakuja

3. waliokuwa friend ndio watakaoweza kuona akaunti tu.

4. Ni akaunti kwa ajili ya kumbukumbu kwa ndugu na jamaa

5. Facebook wataweka lebo karibu na profile picture kuonyesha kuwa huyu amefariki

6. Hautaweza kutumiwa meseji akaunti hii

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Teknolojia Main: Post File: Download PDF Views 1187

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 web hosting     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Yanayoathiri betri yako

Somo hili linakwenda kukuletea mambo yanayo athiri betri lako

Soma Zaidi...
UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO

Namna ya kutunza betri yako iweze kudumu kwa muda mrefu

Soma Zaidi...
Kurudisha data zilizo potea

Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta..

Soma Zaidi...
Nini Chanzo

Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta..

Soma Zaidi...
Matumizi ya OCR katika simu yako

Somo Hili linakuleteq mafunzo ya OCR katika simu yako

Soma Zaidi...
NINI HATMA YA FACEBOOK BAADA YA KUFA KWAKO? nini kitatokea kwenye akaunti yako ya fesibuku (facebook)

Facebook hawana mpango wa kufunga akaunti ambazo hazijatumiwa kwa muda mrefu, haijalishi akaunti ni ya marehemu ama yupo hai.

Soma Zaidi...