Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.
Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha.
Yafuatayo Ni maandalizi ya Mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia;
1.kuwepo na usafiri ; mama anapo hudhurua clinic hufundishwa dalili za Hatari hivyo ujauzito sio kitu Cha kushtukiza hvyo unatakiwa kujipanga ili kutafuta usafiri mapema .
2.mtu atakayebaki nyumba; husaidia kulinda nyumba na familia iliyobaki pia na kuangalia usalama wa hapo nyumbani.
3.mtu wa kumsindikiza; mama anapoenda kujifungua awe na msaidizi kwa ajili ya kuenda kumsaidia na msindikizaji huyu awe anajiweza ili aweze kumsaidia mama pale atakapohitajika msaada wake.
4. Vifaa vya kujifungulia; Kawaida mama akiwa anahudhuria cliniki hupewa mwongozo wa kila kitu hivyo anatakiwa awe na vifaa kwa ajili ya kujifungulia ,na vifaa hivyo Ni Kama vile
1. karatasi aina ya nailoni kwaajili ya kutandikia kitanda anachojifungulia mama ili kuepusha kuchafua mazingira.
2. mipira ya Kuvaa mikononi (gloves) hizi hutumika wahudumu wanapokua wanamuhudumia mama akiwa anajifungua.
3. Kiwembe Cha Upasuaji hutumika kukatia kitovu kilichounganisha Mtoto na kondo la nyuma ili kutenganisha pia kukatia nyuzi wakati mama anaposhonwa Kama akiwa amechanika.
4. kibanio Cha kitovu (clamp) hutumika kubania kitovu kikitenganishwa ili kisitoe Damu.
-5. vitenge au khanga ; ambazo hutumika kumfunikia mtoto,kutandikia kwenye nailoni,mama kujifungua na nguo hizi zisiwe mpya ziwe Ni khanga zilizotumika.
6. malapa ambayo atavaa mam anapotaka kwenda kuoga,kufanya mazoezi maana hawezi kutembea bila kitu mguuni.
7. beseni (dishi) au ndoo ndogo hutumika kuwekea ndoo chafu pia kiafa hiki hutumika mama kunisaidia wakati anakaribia kujifungua maana hauruhusiwi kwenda chooni.
8. sabuni na mafuta ya mama
9. Pamba kubwa na nyuzi za upasuaji
10. pedi kubwa za mama ambapo akijifungua anaweza kuitumia Ila so lazima maana mama anaweza kuitumia khanga.
11. vifaa vya Mtoto Kama vile soksi, bebshoo,pampasi,kofia,mafuta ya Nazi ili vimpatie Mtoto joto pia na leso laini kwaajili ya kumfutia Mtoto.
5.fedha; mama na familia kiujumla wanatakiwa kujipanga kwa matumizi ya hela pale zitakapohitajika wawe nazo.
Mwisho; mama mjamzito anapohudhuria kliniki hupewa mwongozo wote na swala la ujauzito sio la kushtukiza Ni kitu ambacho kipo wazi hivi mama au familia unatakiwa kujipanga na maandalizi.
Mwisho; mama mjamzito anapojigundua tu kuwa ana mimba anatakiwa awahi cliniki kwaajili ya kupewa eleimu juu ya kujikinga,Mambo Hatari kujua na vifaa na Mambo mengine mengi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba
Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba,Ni mambo ya kuzingatia ili mama akija kubeba mimba awe mzima kimwili, ki afya na kisaikolojia na hivyo hivyo Mtoto atakayezaliwa atakuwa salama.
Soma Zaidi...Sababu za mbegu za kiume kuwa dhaifu
Posti hii inahusu zaidi sababu za mbegu za kiume kuwa dhaifu, hali hii uwatokea wanaume wengi kwa sababu mbalimbali za kimaisha ambazo ufanya mbegu za kiume kuwa dhaifu na kusababisha madhara makubwa zaidi kwa sababu wanaume wengi ushindwa kujiamini kwa h
Soma Zaidi...Sababu za kupata hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi mmoja
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi mmoja, mara nyingi kuna Watu ambao huwa wanalalamika kwa sababu ya kupata hedhi za mara kwa mara kwa mwezi mmoja.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito.
Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisukari wakati mama akiwa mjamzito.na yafuatayo ni Mambo hatari yanayotokea wakati Mama akiwa na ujauzito.
Soma Zaidi...Je dalili ya kuuma tumbo huanza baada ya wiki ngapi Toka mwanamke apate ujauzito?
Maumivu ya tumbo ni moja katika dalili za ujauzito. Maumivu wanawake wengi hushindwa kujuwa kuwa ni ujauzito ama laa. Na hii ni kwa sababu kwa wanawake wengi maumivu ya tumbo ama changu ni jalivya kawaida kwao.
Soma Zaidi...