Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye tumbo la uzazi la Mama pindi anapobeba mimba, ni mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke anapobeba mimba kama ifuatavyo.
Mabadiliko kwenye Tumbo la Mama anapobeba mimba.
1.Mama anapobeba tu mimba tumbo la uzazi linakomaa na kuwa na mazingira ya kumpatia mtoto chakula na mazingira kwa ajili ya kukua kwa mtoto, hii utokea pale ambapo mimba ukomaliza kutungwa tu tumbo la uzazi uandaliwa kwa ajili ya kutunza mimba iliyotungwa na namna ya kulisha mimba iliyotungwa kwa miezi Tisa mpaka pale mtoto anapozaliwa.
2.Baada ya Mimba iliyotungwa kutoka kwenye milija ambapo mimba utungiwa kwa kitaalamu huitwa follapian tube mimba ushuka mpaka kwenye tumbo la uzazi hapo placenta utengenezwa na kumalizika kwa mda wa wiki Kumi, na kazi za hiyo placenta ni kusafilisha hewa Safi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kusafirisha chakula kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, hewa chafu kutoka kwa mtoto kwenda kwa Mama na pia kuzuia sumu kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
3.Sehemu ya ndani ya tumbo la uzazi ambayo kwa kitaalamu huitwa myometrium kwa kusaidia a na homoni ambayo huitwa ostrogen usaidia kukomaa kwa misuli ambayo IPO ndani ya tumbo, hiyo misuli ukua na kukomaa kwa ajili ya kutunza mtoto.
4. Kiwango Cha uzito wa tumbo la uzazi uongezeka kutoka kwenye hali ya kawaida ambayo ni 60gm kama mwanamke Hana mimba mpaka 1000gm ikiwa mwanamke ana mimba, kwa hiyo hiki ni kiwango kikubwa kutoka 60gm mpaka 1000gm kwa hiyo sehemu ya tumbo la uzazi inabidi kuandaliwa vizuri Ili kuweza kumtunza vyema mtoto.
5. Size ya mlango wa kizazi nayo ubadilika kutoka kwenye hali ya kawaida ambayo ni 7.5 mara 5 mara 2.5 mpaka 30 mara 22.5 mara 20 in cm. Tunaona size kabla mama hajabeba mimba ni tofauti kabisa na baada ya kubeba mimba kwa hiyo Mama anapaswa kuangaliwa kwa namna ya pekee kwa sababu ya Mzigo Mzito aliubeba.
6. Na pia kwenye mlango wa uzazi mishipa ya damu unaongezeka Ili iweze kusambaza damu vizuri kwa Mama na mtoto na pia kuweza kufanya kazi ya placenta vizuri Ili damu kwa mtoto na Mama iweze kutosha kwa kiwango kinachohitajika kwa hiyo Mama akiwa na Mimba mishipa ya damu uongezeka kwa namba na idadi Ili kusambaa kwa damu ya kutosha kwa Mama na Mtoto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki, kliniki nisehemu ambayo mtoto hupelekwa Ili kujua maendeleo ya mtoto akiwa chini ya umri wa miaka mitano
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.
Soma Zaidi...Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu njia safi za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni.
Soma Zaidi...Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na hatua za kujikinga na Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na kwenye mirija ya uzazi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi,kwa kawaida tumesikia akina mama wengi wanalalamika kuhusu kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi na wengine hawajui sababu zake kwa hiyo sababu zifuatazo ni za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
Soma Zaidi...